Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804
Showing posts with label Habari za kitaifa na kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Habari za kitaifa na kimataifa. Show all posts

Saturday, August 8

Babake mtoto Mpalestina aliyechomwa, ameaga











Babake mtoto wa kipalestina aliyechomwa moto hadi akafa juma lililopita na walowezi wa kiyahudi katika maeneo yaliyokaliwa ya ukingo wa magharibi (West Bank) ameaga dunia.

Sa'ad Dawabsheh ameaga dunia katika hospitali ya Soroka iliyoko Israeli.

Babake mtoto Mpalestina aliyechomwa moto akafa ameaga dunia 


Bwana Dawabsheh alipelekwa Israeli ilikupata matibabu baada ya kuungua katika shambulizi
lililoteketeza mtoto wake mchanga wa mwaka mmoja u nusu.

Shambulizi hilo lililotekelezwa na walowezi wa Kiyahudi lilimuacha bwana Dawabsheh mke wake na mwana wao mwenye umri wa miaka 4 wakiuguza majereha mabaya.

Mke wake bi Riham na mwana wao Ahmad bado wako katika hali mahututi.

Nyumba yao ilichomwa moto katika shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na walowezi wa kiyahudi 

Shambulizi hilo lililotokea mwisho wa mwezi Julai liliibua hasira miongoni mwa Wapalestina na wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu ambao waliilaumu Israeli kwa kukosa kuwajibikia
usalama wa Wapalestina mikononi mwa Walowezi wa kiyahudi.

Wakati wa shambulizi hilo,Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon alitaka wale waliohusika kwenye shambulizi la kumchoma mtoto Mpalestina katika eneo linalokaliwa na Israel la ukingo wa magharibi kufikishwa mbele ya sheria.

Kifo cha mtoto huyo kiliibua hasira na maandamano 

Waziri mkuu wa Israel Benjamin aliahidi kuwa wale waliotekeleza kitendo hicho alichokitaja kuwa cha kigaidi wangechukuliwa hatua za kisheria.
Netanyahu alielezea mshangao wake kutokana ni kile alichokitaja kuwa mauaji ya kikatili alipowatembelea wazazi wa mtoto huyo na nduguye hospitalini.
Afisa wa Palestina, Ghassan Daghlas, alisema walowezi wa Israil, walichoma moto nyumba nyengine katika kijiji cha Duma hii leo, lakini hakuna mtu aliyeumia vibaya.
Umoja wa Mataifa unasema walowezi wa Israil wamefanya mashambulio kama 120 mwaka huu, katika Ufukwe wa Magharibi uliokaliwa.
 

 
 
Read more »

Hali ni tete Kabul mabomu yameua watu 41
















Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani anaongoza kikao maalum cha usalama baada ya mashambulizi 
kadha ya kujitolea muhanga yaliyopelekea watu 41 kufa.
Mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, umekumbwa na milipuko kadhaa



Miongoni mwa maeneo yaliyolengwa ni chuo cha maafisa wa polisi, ambapo mtu mmoja aliyekuwa amevalia sare za polisi alijilipua na kuwaua zaidi ya watu 25.
Washambuliaji hao pia walivamia kituo cha wanajeshi wa shirika la kujihami la NATO kilichoko karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa.



Inadaiwa kuwa wawili kati ya washambuliaji hao waliuawa.
Mapema siku ya Ijumaa lori moja lililokuwa limetegwa bomu lililipuka karibu na afisi za serikali na kuwaua watu 15.



Rais Ashraf Khan alisema kuwa mashambulizi hayo yalikuwa ni lengo la Wapiganaji wa Kiislamu wa Taliban kujaribu kuwasahaulisha watu misukosuko inayokumba kundi lao kufuatia tangazo la juma lililopita kuwa mwanzilisi wa kundi hilo,Mullah Omar,alifariki



Read more »

Wednesday, March 25

Majaribio ya kombora la balestiki nchini Marekani

Majaribio ya kombora la balestiki nchini Marekani

Jeshi la Anga la Marekani limetangaza kuwa limefanyia majaribio kombora la balestiki linaloweza kuvuka mabara na kwamba majaribio hayo ni ujumbe kwa walimwengu kuhusu uwezo wa silaha za nyuklia wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Anga la Marekani, kombora la Minuteman-III lilifanyiwa majaribio mapema Jumatatu katika kituo cha Jeshi la Anga cha Vandenberg huko California. Taarifa ya Jeshi la Anga la Marekani imesema: Majaribio hayo ya kombola la balestiki la nyuklia yanaonesha picha ya wazi kwa walimwengu kuhusu uwezo wa kombora ya Minuteman-III ambalo linaweza kulenga mahala popote.
Kwa kutilia maanani kwamba Jeshi la Anga la Marekani haliwezi kutumia makombora ya Peace Keeper kwa mujibu wa makubaliano ya silaha ya START II (Strategic Arms Reduction Treaty), kombora la Minuteman-III  litakuwa kombora pekee la balestiki linaloweza kuvuka mabara la jeshi la Marekani. Kombora hilo linavishwa kichwa cha silaha ya nyuklia aina ya W87 ambacho kina uwezo mkubwa wa uharibifu. Majaribio hayo yamefanyika sambamba na mazoezi ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na majeshi ya shirika la NATO huko Ulaya mashariki.
Inaonekana kuwa kwa majaribio ya kombora hilo la nyuklia, jeshi la Anga la Marekani linafuatilia malengo kadhaa.
Kwanza ni kuwa Marekani inataka kuonesha misuli na uwezo wake wa silaha za nyuklia kwa wapinzani wake wakubwa hususan Russia. Katika kipindi cha miaka kama miwili iliyopita jeshi la Russia limefanya majaribio mtawalia ya makombora yanayoweza kuvuka mabara (Intercontinental Ballistic Missile au IBM) na hata kurusha makombora kama hayo kwa kutumia nyambizi. Kwa msingi huo Marekani ilikuwa ikinyemelea fursa ya kukabiliana na majaribio hayo ya silaha za nyuklia ya Russia.
Suala la pili ni kushadidi mivutano baina ya Russia na NATO huko Ulaya Mashariki ambako kumezifanya pande hizi mbili zijizatiti kwa silaha na majeshi katika eneo hilo na katika Bahari Nyeusi. Kwa msingi huo Marekani inataka kumuonesha adui wake yaani Russia, kwamba iwapo mgogoro huo utaendelea inaweza kutumia silaha zake za nyuklia.
Marekani ni miongoni mwa wamiliki wakubwa zaidi wa silaha za nyuklia duniani na ndiyo nchi pekee ambayo hadi sasa imetumia silaha hizo kuua watu wa taifa jingine. Nchi hiyo kinyume na ahadi zake za kupunguza maghala yake ya silaha za nyuklia, ingali inastawisha na kupanua zaidi silaha hizo na kuzifanyia majaribio. Marekani pia inasasisha na kuziboresha zaidi silaha zake za zamani za nyuklia licha ya harakati za kimataifa za kupunguza silaha hizo husuan mkataba wa NPT unaosisitiza kupunguzwa na hatimaye kuangamizwa kabisa silaha hizo. Katika uwanja huo Washington imetenga bajeti ya dola bilioni 355 ambazo zitatumika kusasisha na kuboresha mitambo yake ya silaha na kuinua juu kiwango cha majaribio ya silaha za nyuklia. Vilevile Marekani imechukua hatua za kuboresha silaha na maghala yake ya zana za nyuklia barani Ulaya yakiwemo mabomu ya nyuklia ya B-61.
Kwa utaratibu huo, Washington, kinyume na mikataba ya kimataifa ya kuzuia uzalishaji wa silaha za nyuklia, inaendelea kuzalisha na kufanyia majaribio silaha za aina hiyo, suala ambalo linakiuka mkataba wa NPT. 
Read more »

Jumatano, Machi 25, 2015

  •  
  • Jumatano, Machi 25, 2015
Leo ni Jumatano tarehe 4 Jamadithani 1436 Hijria sawa na Machi 25, 2015.
Siku kama hii ya leo miaka 21 iliyopita, vikosi vya jeshi la Marekani ambavyo mwezi Disemba 1992 viliivamia Somalia kwa kisingizio cha kukomesha uasi nchini humo, hatimaye vililazimika kuondoka katika nchi hiyo baada ya kushindwa vibaya. Mwaka 1991 makundi mbalimbali ya Somalia yalimpindua dikteta wa nchi hiyo Muhammad Siad Barre. Hata hivyo makundi hayo yalishindwa kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya mseto na mkwamo huo wa kisiasa ukapelekea kuzuka vita vya ndani nchini humo. Marekani ilituma wanajeshi wake huko Somalia katika fremu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa ili kulinda maslahi yake nchini humo, kutokana na nafasi muhimu ya Somalia katika eneo la Pembe ya Afrika. Askari wa Marekani walikabiliwa na mapambano makali ya Wasomali na kupoteza askari karibu 100.


Tarehe 25 Machi miaka 40 iliyopita Mfalme wa wakati huo wa Saudi Arabia, Faisal bin Abdulaziz, aliuawa na mwana wa ndugu yake mwenyewe, Faisal bin Saaid bin Abdulaziz. Faisal bin Saaid alifanya mauaji hayo akilalamikia kupunguzwa kwa mshahara wake. Japokuwa hitilafu katika kizazi cha wafalme wa Saudi Arabia zimekuwepo siku zote na zimekuwa zikipamba moto mara kwa mara lakini mauaji ya Mfalme Faisal yalikuwa ya kwanza ya mfalme wa nchi hiyo kutokana na hitilafu kama hizo. Muuaji wa Mfalme Faisal pia alikatwa kichwa mbele ya umati wa watu tarehe 18 Juni mwaka 1975. Baada ya Faisal, Khalid mwana mwingine wa Abdulaziz alishika kiti cha ufalme wa Saudi Arabia.


Na miaka 58 iliyopita mwafaka na siku hii ya leo mkataba wa kuasisi Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya au kwa jina jingine Soko la Pamoja la Ulaya ulisainiwa huko Roma mji mkuu wa Italia kati ya wawakilishi wa nchi mbalimbali za bara hilo. Jumuiya hiyo iliundwa kwa lengo la kuasisi umoja wa forodha kati ya nchi wanachama ili kufuta ushuru wa bidhaa na baada ya hapo, ubadilishanaji wa bidhaa, nguvu kazi, vitega uchumi na huduma nyinginezo pia ukawa huru kati ya nchi wanachama. Jumuiya hiyo ilikuwa utangulizi wa kuundwa Umoja wa Ulaya mwaka 1992.
Read more »

Monday, March 23

Mvua yasababisha vito vya watu 5 Dar es Salaam

Mvua yasababisha vito vya watu 5 Dar es Salaam  
 Hali tete inatawala katika jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania kutokana na mvua ya masika iliyonyesha kwa siku tatu na kusababisha vifo vya watu watano, huku nyumba nyingi zikiwa zimezingirwa na maji. Maeneo yaliyoathirika zaidi katika mji huo ni Buguruni kwa Mnyamani na eneo la Jangwani katika Manispaa ya Ilala, ambako nyumba nyingi na barabara zimeathirika. Sehemu nyingine za jiji la Dar es Salaam zimezingirwa na maji kutokana na kuziba kwa mitaro na mifereji, ikiwa ni athari ya utupaji taka ovyo na pia miundombinu duni. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), mvua kubwa zaidi zinatarajia kuendelea kunyesha mpaka siku ya Jumatano. Kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha, Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki jana aliongoza kikosi cha uokoaji katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ambako nyumba 250 zilizingirwa na maji, jambo ambalo vikosi vya uokoaji vililazimika kufanya kazi ya kuwanasua watu waliokuwa wamekwama katika nyumba zao. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa, hadi kufikia jana mvua hizo zilikuwa zimesababisha vifo vya watu watano, akiwemo mtu mmoja aliyesombwa na maji, mwingine aliyeangukiwa na ukuta na watatu ambao walinaswa na umeme baada ya nguzo ya umeme kuanguka Mbagala Mzambarauni katika Manispaa ya Temeke.
Read more »

Monday, February 2

nibaada ya kituo cha 100.0 iqra fm elimu na matendo kuto weka hewan kuto kwa sababu za  kifaa ufund kukosekama
nkinacho itwa filta kutua nchin tanzania na tayali kimesha fungwa ka mkao wa kula
Read more »

Thursday, December 4

Jumatatu, Desemba Mosi, 2014

Jumanne, Novemba 25, 2014Leo ni Jumatatu tarehe 8 Safar mwaka 1436 Hijiria, inayosadifiana na tarehe Mosi Disemba mwaka 2014 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 1401 iliyopita, aliaga dunia Salman Farsi, mmoja kati ya maswahaba wakubwa wa Bwana Mtume (SAW). Salman alikuwa Muirani wa kwanza kuingia katika dini ya Kiislamu na kukubali mafundisho ya Nabii Muhammad (SAW). Salman Farsi alifanya jitihada kubwa za kujipamba kwa maadili mema, takwa na ucha-Mungu hadi kuwa miongoni mwa maswahaba wa karibu wa Mtume.  Bwana Mtume Mtukufu (SAW) anamtaja Salman Farsi kuwa miongoni mwa Ahlubaiti wake. Swahaba huyo mwema alikuwa bega kwa bega na Mtume Mtukufu katika vita vya kutetea Uislamu. Swahaba huyo aliendelea kuwa karibu na Ahlulbait wa Mtume (SAW) baada ya mtukufu huyo kuaga dunia.
Miaka 117 iliyopita  muwafaka na leo, yaani tarehe Mosi Disemba mwaka 1897 Miladia, ulitiwa saini mkataba wa kihistoria mashuhuri kwa jina la mkataba wa "Kutokuweko Mapigano" kati ya Italia na mojawapo ya jamhuri ndogo zaidi duniani kwa jina San Marino, ambayo inazungukwa na Italia kusini mwa bara Ulaya. Kwa mujibu wa mkataba huo, Jamhuri ya San Marino iliahidi kutoishambulia Italia na Italia pia kuahidi kuheshimu uhuru wa nchi hiyo ndogo.
Miaka 189 sawa na leo, Muungano wa kihistoria wa nchi za Ulaya ulisambaratika baada ya kujiengua utawala wa Kikaitsar (Tsarist) wa Russia katika muungano huo. Baada ya kuanguka kwa utawala wa Napoleon, muungano huo ukaunda Congress ya Vienna, kati ya tawala za Russia, Austria na ufalme wa Pros na serikali hizo zikaafikiana kwamba nchi zilizo chini ya utawala wa muungano huo na katika uhusiano wa kimataifa zifuate misingi ya dini ya Kikristo.
Na katika siku kama ya leo kila ifikapo tarehe Mosi mwezi Disemba kila mwaka, nchi mbalimbali duniani huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Ukimwi. Kuweko Siku ya kimataifa ya Ukimwi kulifikiriwa kwa mara ya kwanza mwezi Agosti mwaka 1987 na James W.Bunn na Thomas Netter, maafisa wawili wa habari wa Kitengo cha Kimataifa cha Kupambana na Ukimwi cha Shirika la Afya Duniani (WHO) huko Geneva Uswisi. Maafisa hao wawili waliwasilisha wazo hilo kwa Dakta Jonathan Mann, Mkurugenzi wa Shirika la UNAIDS na baadaye akakubali pendekezo hilo, na kuliidhinisha. Na hatimaye akaafiki siku ya kwanza ya kimataifa ya Ukimwi iadhimishwe duniani kote tarehe Mosi Disemba mwaka 1988. Kuanzia wakati huo kila mwaka siku ya kimataifa ya Ukimwi huadhimishwa duniani kote kila ifikapo tarehe Mosi Disemba.
Read more »

Rwasa aitahadharisha serikali Burundi na machafuko

Rwasa aitahadharisha serikali Burundi na machafukoKiongozi wa chama cha upinzani cha FNL nchini Burundi ametahadharisha kuwa, taifa hilo linaweza kutumbukia kwenye ghasia na machafuko iwapo serikali haitowasikiza wadau katika siasa za nchi hiyo. Akizungumza kwenye mahojiano maalum na Idhaa hii, Agathon Rwasa amesema kuwa, mchakato wa kuandaa daftari la wapiga kura kupitia uandikishaji wa raia ni zoezi lililovurugika na ameitaka serikali kusitisha zoezi hilo mara moja. Rwasa amesema uchaguzi mkuu ujao unaweza kuwa nukta ya kuwaunganisha Warundi pamoja au kuwagawanya kwa kutegemea jinsi maandalizi yatakavyofanywa. Mkuu wa FNL amesema mustakabali wa siasa nchini Burundi unakumbwa na hatihati na kusisitiza kuwa serikali itabeba dhima iwapo machafuko yatatokea kutokana na upuuzaji wake wa hali ya mambo kwa hivi sasa.
Tayari muungano wa upinzani wa ADC-Ikibiri umejiondoa kwenye zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kufuatia dosari zilizojitokeza na kutishia kususia uchaguzi mkuu wa rais mwakani endapo serikali haitositisha zoezi hilo
Read more »

Yemen na ukwepaji jukumu la kulinda maisha ya wanadiplomasia wa Iran

Yemen na ukwepaji jukumu la kulinda maisha ya wanadiplomasia wa IranKatika kuendelea kujiri matukio yanayotokana na kutojali serikali ya Yemen kulinda maisha ya wanadiplomasia na majengo ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, makazi ya balozi wa Iran katika mji mkuu wa nchi hiyo Sana'a jana yalilengwa na shambulio la kigaidi. Kwa mujibu wa duru za Yemen watu wasiopungua watatu akiwemo mlinzi wa nyumba ya balozi ambaye ni raia wa Yemen waliuawa na wengine kumi na saba walijeruhiwa, baadhi yao wakiwa mahututi kutokana na mripuko wa gari lililotegwa bomu ndani yake ambalo lilikuwa limeegeshwa karibu na nyumba ya Sayyid Hassan Niknam, balozi wa Iran mjini Sana'a. Balozi wa Iran hakuwepo nyumbani kwake wakati wa shambulio hilo ambalo lilisababisha pia hasara kubwa kwa nyumba za jirani na magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu na mahali ulipotokea mripuko huo wa bomu. Kufuatia tukio hilo balozi mdogo wa Yemen hapa nchini alitakiwa kufika Wizara ya Mambo ya Nje hapa mjini Tehran. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya nchi za Kiarabu na za Kiafrika, Hussein Amir Abdolahian ameashiria kuitwa balozi huyo mdogo wa Yemen na kueleza kwamba Wizara ya Mambo ya Nje imetoa indhari na sisitizo kubwa kuhusu jukumu la serikali ya Yemen la kulinda usalama wa wanadiplomasia na majengo ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyoko mjini San’aa. Abdolahian ameongeza kuwa balozi mdogo wa Yemen amesisitiziwa kwamba matarajio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuona serikali ya Sana’a inachukua hatua za haraka za kumtambua, kumkamata na kumwadhibu mhusika au wahusika wa shambulio hilo la kigaidi. Shambulio la kigaidi la jana mbele ya makazi ya balozi wa Iran nchini Yemen limetokea katika hali ambayo kabla ya hapo wanadiplomasia wa Iran walishaandamwa na mashambulio kadhaa ya kigaidi ambapo katika kipindi cha karibu mwaka mmoja na nusu uliopita Nour Ahmad Nikbakht, Mwambata wa masuala ya uendeshaji wa ubalozi wa Iran nchini Yemen alitekwa nyara. Na kabla ya tukio la jana, mwanzoni mwa mwaka huu, Ali Asghar Asadi, mwanadiplomasia mwengine wa Iran aliuliwa wakati alipokuwa akikabiliana na magaidi waliokuwa wamedhamiria kumteka nyara. Licha ya ufatiliaji uliofanywa na maafisa wa Iran katika miezi ya hivi karibuni wa kutaka kujua hatima ya Nour Ahmad Nikbakht, Mwambata wa masuala ya uendeshaji wa ubalozi wa Iran mjini San’aa, hadi sasa viongozi wa Yemen hawajatoa jibu la kuridhisha juu ya suala hilo. Nayo Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilishawahi kumwita mara mbili balozi mdogo wa Yemen hapa nchini na kumweleza wasiwasi mkubwa ilionao Tehran juu ya hatima ya mwanadiplomasia wake huyo. Sambamba na hatua hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje Muhammad Javad Zarif alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen pembeni mwa mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, na akasisitiza tena juu ya jukumu ililonalo serikali ya Yemen la kuhakikisha mwanadiplomasia huyo wa Iran anaachiliwa huru haraka iwezekanavyo. Lakini mbali na wanadiplomasia wa Kiiran, wanadiplomasia wa nchi nyengine za kusini mashariki mwa Asia na wa nchi za Ulaya nao pia wamekuwa wakiandamwa na hujuma na mashambulio ya makundi ya kigaidi nchini Yemen. Hata hivyo badala ya viongozi wa serikali ya Yemen kufanya juhudi kwa ajili ya kuachiliwa huru mwanadiplomasia wa Iran aliyetekwa nyara na kuchukua hatua zinazotakiwa ili kulinda maisha ya wanadiplomasia, wamekuwa wakikwepa jukumu lao hilo na badala yake kuituhumu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ati inaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo. Ukweli ni kwamba moja ya sababu kuu za kukosekana amani na usalama nchini Yemen ni udhaifu wa serikali ya muda ya nchi hiyo wa kushindwa kudhamini usalama na kuzuia uingizwaji silaha na makundi yanayobeba silaha nchini humo. Katika hali kama hiyo badala ya serikali ya Yemen kufanya juhudi zaidi za kulinda usalama wa raia wake na wa raia wa kigeni walioko nchini humo inajaribu kukwepa jukumu lake hilo na kuyahusisha matatizo yake ya ndani na nje ya mipaka ya nchi hiyo… Read more »

Friday, November 21

Assad: Viwepo vita vya kimataifa dhidi ya magaidi

Assad: Viwepo vita vya kimataifa dhidi ya magaidiRais Bashar al-Assad wa Syria amesema kuwa, kuna udharura wa kuweko vita vya kimataifa dhidi ya magaidi. Rais Assad amesisitiza kwamba, kwa sasa eneo la Mashariki ya Kati linapitia kipindi nyeti mno lakini kile ambacho kitaainisha njia ya marhala hii ni kusimama kidete taifa la Syria. Ameongeza kuwa, mustakabali wa Mashariki ya Kati utaainishwa kwa kusimama kidete wananchi wa Syria katika kupambana na makundi ya kigaidi sambamba na himaya kwa taifa hilo ya nchi marafiki na Syria. Rais wa Syria amebainisha kwamba, ili ugaidi na makundi ya kigaidi vitokomezwe kuna haja ya kuweko vita vya kimataifa tena vyenye nia safi na ya dhati ya kupambana na ugaidi.
Rais Bashar al-Assad amesisitiza kwamba, taifa la Syria halitasalimu amri, bali litaendelea kupambana na makundi ya kigaidi katika nchi hiyo ambayo mbali na kuhatarisha usalama wa nchi yametenda jinai kubwa dhidi ya binadamu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Wakati huo huo ripoti kutoka Syria zinaonesha kuwa, jeshi la nchi hiyo limeendelea kupata mafanikio katika operesheni zake za kijeshi za kupambana na makundi ya kigaidi.
Read more »

Algeria yataka mahasimu wa Mali wakubaliane

Algeria yataka mahasimu wa Mali wakubalianeSerikali ya Algeria ambayo ni mpatanishi katika mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Mali na makundi ya waasi ya kaskazini mwa nchi hiyo imezitaka pande mbili hizo kutumia vyema fursa ya mazungumzo ya amani na kufikia makubaliano. Takwa hilo limetolewa na Ramtane Lamamra, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Algeria ambaye amesisitiza kwamba, pande hasimu za Mali zinapaswa kutumia vyema na kadiri ziwezavyo fursa ya mazungumzo ya amani. Amesema kuwa, mazungumzo ya amani ya Mali yanayoendelea katika mji mkuu wa Algeria Algiers yanapaswa kutumiwa vyema na pande hizo mbili hasimu na hivyo kutiliana saini makubaliano ya mwisho ya amani.
Duru ya nne ya mazungumzo ya amani ya Mali ilianza jana nchini Algeria ambapo duru mbalimbali za kisiasa zinazitaka serikali ya Bamako na makundi ya waasi kufanya juhudi ili kufikia makubaliano ya mwisho ya amani. Kutofikiwa mazungumzo kati ya pande mbili kumezitia wasi wasi nchi nyingi hasa zinazopakana na Mali ambazo zinahofia kupenya makundi ya waasi na kuingia katika nchi zao. Hivi karibuni Jeshi la Algeria liliimarisha usalama katika mpaka wake na Mali  ili kuzuia upenyaji na uingiliaji wa magaidi kutoka kwa jirani yake huyo.
Read more »

Mahmoud Abbas ataka kusitishwa jinai za Israel

Mahmoud Abbas ataka kusitishwa jinai za IsraelRais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amewaandikia barua shakhsia kadhaa wa kisiasa ulimwenguni akitaka kuweko uingiliaji kati wa haraka ili kukomeshwa hujuma na jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Quds inayokaliwa kwa mabavu.
Katika barua yake kwa Bani Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, John Kerry Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Sergey Lavrov Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia, Federica Mogherini Mkuu mpya wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya na Tony Blair Mjumbe wa Kamati ya Pande Nne ya Amani ya Mashariki ya Kati, Rais Mahmoud Abbas amewataka shakhsia hao kuulazimisha utawala wa Kizayuni wa Israel uhitimishe jinai zake dhidi ya wananchi wa Palestina. Aidha Mahmoud Abbas amewataka shakhsia hao kuiunga mkono azma ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kutambuliwa nchi ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967 mji mkuu wake ukiwa Baytul Muqaddas. Hayo yanajiri katika hali ambayo, katika siku za hivi karibuni utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na mashambulio yake dhidi ya Wapalestina na katika msikiti wa al-Aqswa huko Baytul Muqaddas.

Read more »

Wakimbizi wa Chad wanakabiliwa na hali mbaya

Wakimbizi wa Chad wanakabiliwa na hali mbayaShirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limeelezea wasi wasi wake mkubwa lilionao kuhusiana na hali mbaya wanayokabiliwa nayo wakimbizi wa Chad. Taarifa zaidi zinasema kuwa, baada ya kushadidi machafuko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, raia wengi wa Chad waliokuwa wakiishi nchini humo wamelazimika kuondoka nchini humo na kurejea 

nchini kwao. Aghlabu ya wakimbizi hao wamo katika kambi za wakimbizi zilizoko kusini magharibi mwa Chad. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu hali ya kibinadamu katika kambi hizo ni mbaya mno. Takribani raia elfu saba kati ya wakimbizi hao wana azma ya kurejea katika makazi yao huko mashariki mwa Chad. Ripoti ya 

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu inaeleza kuwa, licha ya kuweko ugawaji misaada kwa wakimbizi hao, lakini misaada hiyo haitoshi kukidhi mahitaji ya wakimbizi hao. Mbali na wakimbizi wa Kichadi waliorejea katika nchi yao, 


Chad kwa sasa inakabiliwa pia na wimbi la wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao wameikimbia nchi yao baada ya kushadidi machafuko na mapigano. Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba serikali ya Chad haina uwezo wa kifedha wa kudhamini mahitajio ya maelfu ya wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati walioko nchini humo.
Read more »

Rais wa Somalia: al-Shabab watasambaratishwa

Rais wa Somalia: al-Shabab watasambaratishwaRais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia ametangaza kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa 2014, kundi la wanamgambo wa al-Shabab litalazimika kuondoka katika maeneo na miji linayoidhibiti katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. Mtandano wa Habari wa al-Yaum Sab’i umemnukuu Rais Hassan Sheikh Mohamoud akisema kwamba, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba ujao jeshi la Somalia na vikosi vya kusimama amani vya Umoja wa Afrika AMISOM vitakuwa vimefanikiwa kuwafurusha wanamgambo wa al-Shabab na kuwalazimisha kuondoka katika maeneo wanayoyadhibiti.
 Rais wa Somalia ambaye kwa sasa yuko nchini Denmark alikokwenda kushiriki mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia amesema kuwa, wanamgambo wa al-Shabab watalazimika kurejea nyuma na kwenda katika vijiji vya mbali na hivyo mashambulio yao baada ya hapo yatakuwa ya hapa na pale. Rais Mohamoud amebainisha kwamba, serikali ya Somalia inafanya kila iwezalo ili kuhakikisha kwamba, hadi kufikia miezi mitatu ya awali ya mwaka ujao wa 2015 kusiweko  eneo lolote nchini humo ambalo linadhibitiwa na wanamgambo wa al-Shabab.
Read more »

Friday, November 7

Ban atakiwa kufuatilia jinai za utawala wa Bahrain

Ban atakiwa kufuatilia jinai za utawala wa BahrainChama cha upinzani cha al Wefaq nchini Bahrain kimemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon afuatilie jinai za utawala wa al Khalifa.  Sheikh Ali Salman, Katibu Mkuu wa chama hicho amesema, kukamatwa tena Nabil al Rajab na viongozi wengine wa upinzani wa Bahrain na kupigwa marufuku shughuli za chama cha la Wefaq ni sawa na kushindwa uchaguzi wa Bunge la nchi hiyo hata kabla ya kufanyika. Katika barua yake kwa Ban Ki-moon ameeleza kuwa, vikosi vya utawala wa Bahrain vinawatesa hadi kufa wapinzani huku kuvunjwa haki za binadamu na kukandamizwa watu likiwa ni jambo la kawaida nchini humo. Ameongeza kwamba, utawala wa Aal Khalifa mbali na kubomoa misikiti, umeshadidisha sera za ubaguzi wa kidini na kutumia gesi za sumu dhidi ya waombolezaji wa Imam Hussein (A.S).
Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha la Wefaq sambamba na kusisitiza kuendelea harakati za kimapinduzi za wananchi amemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ashughulikie jinai zinazofanywa na utawala wa Manama.
Read more »

Radiamali ya Wapalestina kwa hujuma za Wazayuni dhidi ya Masjid al-Aqswa

Radiamali ya Wapalestina kwa hujuma za Wazayuni dhidi ya Masjid al-Aqswa jumaa, 07 Novemba 2014 09:23

Kushtadi uvamizi na hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Masjid al-Aqswa ambazo katika siku za hivi karibuni zimechukua mkondo hatari zaidi kuliko huko nyuma, kumekabiliwa na radiamali za makundi ya Wapalestina katika uga wa kimuqawama na kisiasa. Katika mazingira kama haya, sanjari na malalamiko ya wananchi dhidi ya utawala wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu, makundi ya mapambano ya Palestina yamebainisha kwamba, muqawama na mapambano ndilo chaguo pekee la kuuhami na kuulinda msikiti wa al-Aqswa na uvamizi mtawalia wa utawala haramu wa Israel. Katika uwanja huo, siku ya Jumatano Khalid Mash’al, Mkuu wa Ofisi ya Kis iasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS alisisitiza kwamba, machaguo na mikakati yote ya kuuhami msikiti wa al-Aqswa inazingatiwa, lakini muqawama ndilo chaguo linaloongoza machaguo yote. Katika mazingira kama haya, balozi na mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa, amelitaka Baraza la Usalama la Umoja huo liushinikize utawala vamizi wa Israel ukomeshe vitendo vyake vya utumiaji mabavu huko Baytul Maqaddas na katika Masjid al-Aqswa, kibla cha kwanza cha Waislamu. Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano baada ya kikao cha faragha cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Riyadh Mansour alisema, wanachama 15 wa baraza hilo wanapaswa kuchukua msimamo wa kuitaka Israel ikomeshe harakati zozote zile za siasa za kichochezi na vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Wapalestina. Mwakilishi huyo wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, hatua ya Wazayuni wenye kufurutu ada wanaoingia na viatu katika msikiti wa al-Aqswa ni ya kichochezi na imekuwa ikipelekea kutokea rangaito, vurugu na mapigano. Ombi la Wapalestina kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuitaka asasi hiyo iingilie kati kuhusiana na uvamizi na vitendo vya kuuvunjia heshima msikiti wa al-Aqswa vinavyofanywa na Wazayuni linatolewa katika hali ambayo, vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu vinavyofanywa na utawala huo vimeshadidi mno katika eneo hilo takatifu, kongwe na la kihistoria, hali ambayo imepelekea mgogoro wa Palestina kuingia katika marhala hatari zaidi. Hapana shaka kuwa, hujuma na hatua za utawala vamizi wa Israel zimehatarisha amani na usalama wa kimataifa. Hii ni katika hali ambayo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lina jukumu la kushughulikia masuala kama haya limeamua kukaa kimya na kutochukua hatua yoyote ile ya maana. Hatua za utawala ghasibu wa Israel katika msikiti wa al-Aqswa mbali na kukabiliwa na malalamiko ya wananchi zimeandamwa pia na upinzani wa Waislamu katika pembe mbalimbali ulimwenguni. Katika anga kama hii, fikra za waliowengi ulimwenguni nazo zinafuatilia kwa hisia na unyeti maalumu duru mpya ya hujuma za Wazayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa na zinataka Baraza la Usalama lichukue hatua za maana dhidi ya utawala huo. Katika mazingira kama haya, Wapalestina wanataka kuchunguzwa haraka vitendo vya utawala bandia wa Israel katika Masjid al-Aqswa na kuchukuliwa hatua za maana na madhubuti za kusitisha hujuma za utawala huo ghasibu. Hii ni katika hali ambayo, ripoti zinaonesha kuwa, Marekani inapinga vikali kuzungumziwa suala la uvamizi wa Israel katika Masjid al-Aqswa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Jambo lililo wazi ni kuwa, katika hali ambayo utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea na hatua na hujuma zake huko Quds katika anga ya kimya cha jumuiya za kimataifa, hatua bora, ya maana na yenye taathira ni kuendelezwa muqawama sambamba na kushadidishwa mapambano ya wananchi dhidi ya utawala huo ghasibu; na huu ndio ukweli ambao umeashiriwa na Khalid Mash’al, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Matukio ya Palestina yanaonesha juu ya kuingia Wapalestina katika marhala mpya ya muqawama na mapambano dhidi ya utawala vamizi wa Israel. Katika mazingira kama haya, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaamini kwamba, uvamizi na hujuma za Israel dhidi ya msikiti wa al-Aqswa ni kitendo cha kuwasha moto ambao utawala huo ghasibu utatumbukia wenyewe
Read more »

Ijumaa, 07 Novemba 2014 09:23 Ijumaa, Novemba 7, 2014


Ijumaa, Novemba 7, 2014Leo ni Ijumaa tarehe 13 Mfunguo Nne Muharram 1436 Hijria sawa na tarehe 7 novemba 2014.
Siku kama ya leo miaka 58 iliyopita vita vya mfereji wa Suez vilimalizika baada ya uingiliaji kati wa Umoja wa Mataifa. Vita hivyo vilianza baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia jangwa la Sinai na kufuatia mashambulizi ya askari wa miavuli wa Uingereza na Ufaransa katika eneo la mfereji huo. Serikali hizo tatu zilizotajwa zilianzisha vita hivyo kufuatia hatua ya rais wa wakati huo wa Misri, Jamal Abdulnassir, kuutaifisha mfereji huo.
Miaka 147 iliyopita katika siku kama ya leo Madam Escudo Doska ambaye baadaye alikuwa maarufu kwa jina la Marie Curie alizaliwa huko Warsaw mji mkuu wa Poland. Baba yake alikuwa profesa wa fizikia na baadaye Madam Curie pia alielekea Paris, Ufaransa kwa ajili ya kuendeleza masomo yake katika taaluma hiyo hiyo ya baba yake. Madam Curie alifunga ndoa na Pierre Curie mwanafikizikia wa Ufaransa wakati alipokuwa masomoni katika Chuo Kikuu cha Sorbonne. Hatimaye mwanamama huyo alifanikiwa kuvumbua mada ya radium baada ya utafiti miaka mingi. Ni vyema kuashiria hapa kuwa Madam Curie alitunukiwa tuzo ya Nobel mara mbili katika taaluma za fizikia na kemia na aliaga dunia mwaka 1934.
Na siku kama ya leo miaka 36 iliyopita wananchi kote nchini Iran walifanya maandamano makubwa wakipinga kuja madarakani serikali ya kijeshi ya Jenerali Azhari aliyekuwa kibaraka wa utawala fasidi wa Kipahlavi. Katika maandamano hayo wananchi Waislamu wa Iran walitangaza azimio wakisema kuwa mabadiliko ya kimaonyesho na kubadilisha nafasi za vibaraka wa Marekani hakuwezi kuzuia mapambano yao kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiislamu. Siku hiyo pia Kiongozi wa harakati za Mapinduzi hayati Imam Khomeini alitoa ujumbe kwa mnasaba wa mauaji yaliyofanywa na utawala wa Shah dhidi ya wanafunzi wa vyuo vikuu akiwaambia wananchi kwamba: “Ninyi taifa shujaa, mumethibitisha kwamba vifaru, mitutu ya bunduki na mikuki imeota kutu na kwamba haiwezekani kukabiliana na irada ya chuma ya wananchi.”  
Read more »

Upinzani Zimbabwe wataka wabunge 18 wafukuzwe

Upinzani Zimbabwe wataka wabunge 18 wafukuzweChama cha Upinzani cha Zimbabwe cha Movement for Democratic Change (MDC) kimetaka kuwafukuza bungeni wawakilishi 18 ambao si wabunge tena wa chama hicho. Wabunge hao ni pamoja na Tendai Biti katibu mkuu wa zamani wa MDC na waziri wa fedha ambaye amefukuzwa  chamani na mkuu wa chama hicho Morgan Tsvangirai. Chama hicho kimeliambia bunge kuwa wawakilishi hao 18 ambao walichaguliwa kama wabunge wa MDC hawakiwakilishi tena chama hicho. Biti na wenzake walikuwa wakijaribu kumuuzulu Tsvangirai chamani kwa kushindwa kumuangusha Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe katika uchaguzi wa rais.
Mpasuko huo umekidhoofisha chama hicho cha upinzani kinachompinga Mugabe ambaye yupo madarakani tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru mwaka 1980.
 Wiki iliyopita Tsvangirai alichaguliwa tena bila kupingwa kukiongoza chama cha MDC.
Read more »

Waislamu 14,000 walazimishwa kuondoka Myanmar

Waislamu 14,000 walazimishwa kuondoka MyanmarMakundi ya kutetea haki za binadamu yamearifu kuwa, Waislamu wa jamii ya Rohingya wamelazimishwa kuondoka nchini Myanmar katika wiki 3 ziliopita kutokana mpango mpya wa serikali uliozusha mjadala. Kwa mujibu wa mpango huo unaoitwa Rakhine Action Plan, zaidi ya Waislamu milioni moja wa kabila la Rohingya watafukuzwa nchini humo iwapo watashindwa kuthibitisha kwamba familia zao zimeishi nchini Myanmar kwa zaidi ya miaka 60 iliyopita. Waislamu hao wa Mynamar pia wanaweza kufungwa jela kwa muda usiojulikana kwa mujibu wa mpango huo wa kibaguzi, ambao unawataka wakubali kupangwa tena kimakabila na kuandikishwa kuwa ni Wabengali au kufungwa jela.
 Makundi ya kutetea haki za binadamu yameitaka jamii ya kimataifa iishinikize serikali ya Myanmar kufuta mpango huo na kuutaja kuwa hauna maana yoyote zaidi ya kuthibitisha kuendelea ubaguzi wa rangi.
 Jamii ya Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakikabiliwa na ubaguzi, manyanyaso na kupuuzwa tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1948. Katika miaka miwli iliyopita Waislamu wengi wa Myanmar wameuawa huku zaidi ya laki na nusu wakikimbia makazi yao kutokana na mashambulizi yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali.
Read more »

Kesi za Ebola zaongezeka nchini Sierra Leone

Kesi za Ebola zaongezeka nchini Sierra LeoneUmoja wa Mataifa umetangaza kuwa kesi za maambukizi ya ugonjwa wa Ebola zimeongezeka nchini Sierra Leone huku nchi hiyo ikikabiliwa na tatizo la ukosefu wa vituo vya matibabu. Mpango wa Dharura wa Kukabiliana na Ebola wa Umoja wa Mataifa (UNMEER) umesema wiki hii kuwa, mfumuko wa ugonjwa wa Ebola umesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,060 nchini Sierra Leone huku maeneo yaliyoathiriwa zaidi yakiwa ya magharibi mwa mji mkuu Freetown.  Mpango huo aidha umesema, ukosefu wa vitanda katika vituo vya kutibu Ebola umesababisha familia kuangalia zenyewe wagonjwa majumbani, ambako waangalizi huwa hawana uwezo wa kutosha wa kujilinda wasiambukizwe virusi vya ugonjwa huo, na kwa sababu hiyo maambukizo yameongezeka.
Jumatano Shirika la Afya Duniani (WHO) liliripoti kuwa, idadi ya kesi za maambukizo ya Ebola zinaongezaka nchini Sierra Leone, ingawa ugonjwa huo umepungua katika nchi ya Liberia huku nchini Guinea maambukizo yakiwa ya wastani.
Read more »

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com