Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, December 4

Jumatatu, Desemba Mosi, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Jumanne, Novemba 25, 2014Leo ni Jumatatu tarehe 8 Safar mwaka 1436 Hijiria, inayosadifiana na tarehe Mosi Disemba mwaka 2014 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 1401 iliyopita, aliaga dunia Salman Farsi, mmoja kati ya maswahaba wakubwa wa Bwana Mtume (SAW). Salman alikuwa Muirani wa kwanza kuingia katika dini ya Kiislamu na kukubali mafundisho ya Nabii Muhammad (SAW). Salman Farsi alifanya jitihada kubwa za kujipamba kwa maadili mema, takwa na ucha-Mungu hadi kuwa miongoni mwa maswahaba wa karibu wa Mtume.  Bwana Mtume Mtukufu (SAW) anamtaja Salman Farsi kuwa miongoni mwa Ahlubaiti wake. Swahaba huyo mwema alikuwa bega kwa bega na Mtume Mtukufu katika vita vya kutetea Uislamu. Swahaba huyo aliendelea kuwa karibu na Ahlulbait wa Mtume (SAW) baada ya mtukufu huyo kuaga dunia.
Miaka 117 iliyopita  muwafaka na leo, yaani tarehe Mosi Disemba mwaka 1897 Miladia, ulitiwa saini mkataba wa kihistoria mashuhuri kwa jina la mkataba wa "Kutokuweko Mapigano" kati ya Italia na mojawapo ya jamhuri ndogo zaidi duniani kwa jina San Marino, ambayo inazungukwa na Italia kusini mwa bara Ulaya. Kwa mujibu wa mkataba huo, Jamhuri ya San Marino iliahidi kutoishambulia Italia na Italia pia kuahidi kuheshimu uhuru wa nchi hiyo ndogo.
Miaka 189 sawa na leo, Muungano wa kihistoria wa nchi za Ulaya ulisambaratika baada ya kujiengua utawala wa Kikaitsar (Tsarist) wa Russia katika muungano huo. Baada ya kuanguka kwa utawala wa Napoleon, muungano huo ukaunda Congress ya Vienna, kati ya tawala za Russia, Austria na ufalme wa Pros na serikali hizo zikaafikiana kwamba nchi zilizo chini ya utawala wa muungano huo na katika uhusiano wa kimataifa zifuate misingi ya dini ya Kikristo.
Na katika siku kama ya leo kila ifikapo tarehe Mosi mwezi Disemba kila mwaka, nchi mbalimbali duniani huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Ukimwi. Kuweko Siku ya kimataifa ya Ukimwi kulifikiriwa kwa mara ya kwanza mwezi Agosti mwaka 1987 na James W.Bunn na Thomas Netter, maafisa wawili wa habari wa Kitengo cha Kimataifa cha Kupambana na Ukimwi cha Shirika la Afya Duniani (WHO) huko Geneva Uswisi. Maafisa hao wawili waliwasilisha wazo hilo kwa Dakta Jonathan Mann, Mkurugenzi wa Shirika la UNAIDS na baadaye akakubali pendekezo hilo, na kuliidhinisha. Na hatimaye akaafiki siku ya kwanza ya kimataifa ya Ukimwi iadhimishwe duniani kote tarehe Mosi Disemba mwaka 1988. Kuanzia wakati huo kila mwaka siku ya kimataifa ya Ukimwi huadhimishwa duniani kote kila ifikapo tarehe Mosi Disemba.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com