Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804
Showing posts with label mada. Show all posts
Showing posts with label mada. Show all posts

Wednesday, September 24

Jumatano, Septemba 24, 2014


Jumatano, Septemba 24, 2014
Leo ni Jumatano tarehe 28 Dhulqaada 1435 Hijria sawa na 24 Septemba 2014.
Miaka 36 iliyopita katika siku kama hii ya leo, vikosi vya usalama vya utawala wa Baath wa Iraq vikishirikiana na utawala wa Shah viliizingira nyumba ya Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu huko Najaf. Kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliokuwa nao na utawala wa Shah, utawala wa zamani wa Iraq ulimtaka Imam Khomeini asifanye mahojiano na waandishi wa habari, kutoa taarifa, kuhutubia wala kuzungumzia hali ya mambo ya Iran dhidi ya utawala wa Shah. Imam Khomeini aliwajibu kwa kusema kuwa: "Natatekeleza wajibu wangu wa kisheria popote pale nitakapokuwa." Baada ya hapo, serikali ya wakati huo ya Iraq, ikamlazimisha Imam Khomein kuondoka Iraq na hatua hiyo ikaandaa uwanja wa hijra ya kihistoria ya Imam Khomeini ya kuelekea Paris, Ufaransa na kupamba moto utangulizi wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Siku kama ya leo miaka 40 iliyopita, Guinea Bissau ilitangaza uhuru wake kutoka kwa mkoloni Mreno. Guinea Bissau iligunduliwa mwaka 1446 na Mwana Mfalme Henry aliyekuwa akitawala Ureno pamoja na wenzake na kuwa koloni la nchi hiyo. Guinea Bissau ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la Guinea Ureno, ilikuwa miongoni mwa vituo vya biashara ya utumwa ya wazungu katika karne za 17 na 18. Na hatimaye ilipofika mwaka 1974, Ureno ikakubali kuwa huru nchi ya Guinea Bissau. Guinea Bissau iko kaskazini magharibi mwa Afrika na katika pwani ya bahari ya Atlantic.
Na tarehe 28 Dhilqaada miaka 1075 iliyopita mwanazuoni wa Kiislamu Abul Qasim Tabarani, alifariki dunia katika mji wa kihistoria wa Isfahan nchini Iran. Tabarani alikuwa miongoni mwa wanazuoni mashuhuri wa hadithi wa karne ya nne Hijria na alifanya safari katika nchi nyingi za Kiislamu kwa ajili ya kukusanya hadithi za Mtume (saw). Alianza kufundisha na kulea wanafunzi wengi baada ya utafiti na uchunguzi wa miaka 33.
Tabarani ameandika vitabu vikubwa vitatu vya hadithi kwa majina ya Al Muujamul Kabiir", al Muujamul Wasiit na al Muujamus Swaghir.

Alkhamisi, 26 Septemba, 2014





Alkhamisi, 26 Septemba, 2014
Leo ni Alkhamisi tarehe 20 Dhilqaada 1434 Hijria sawa na tarehe 26 Septemba 2013.
Miaka 51 iliyopita katika siku kama ya leo mfumo wa kisultani huko Yemen ya Kaskazini ambao viongozi wake walikuwa wakijiita Imam, ulibatilishwa. Katika siku hiyo Kanali Abdallah Salal alifanya mapinduzi ya kijeshi na kuhitimisha mfumo wa Kisultani na kuasisi mfumo wa jamhuri nchini humo. Baada ya mapinduzi hayo Muhammad Badr aliyekuwa mfalme wa mwisho wa Yemen alianzisha vita dhidi ya utawala mpya wa nchi hiyo kwa uungaji mkono wa Saudi Arabia. Katika upande mwingine Rais Gamal Abdel Nasser wa Misri alituma wanajeshi wa nchi hiyo huko Yemen ili kumsaidia Abdallah Salal katika vita hivyo. Hata hivyo baada ya kupita miaka minne ya vita, pande husika katika vita hivyo zilifikia mapatano na wafuasi wa Imam Badr wakatupilia mbali madai yao ya awali.
Miaka 106 iliyopita katika siku kama ya leo New Zealand inayopatikana mashariki mwa Australia ilipata uhuru. Mwaka 1769 kisiwa cha New Zealand kilikuwa koloni la Uingereza. New Zealand ilizidi kukoloniwa katika karne ya 19 sambamba na kuingia nchini humo wahamiaji wengi wa Kiingereza.
Na siku kama ya leo miaka 125 iliyopita Thomas Stearns Eliot maarufu kwa jina la T.S Eliot, mwanafasihi na mshairi maarufu wa Kiingereza alizaliwa. Mwaka 1922 Eliot alipata umashuhuri kwa kuchapisha diwani ya mashairi aliyoipa jina la "Ardhi Iliyoharibiwa". Mshairi huyo ameandika vitabu vingi vinavyoakisi hisi yake ya kushikamana na kufuata mafundisho ya dini.
Miongoni mwa vitabu vya Thomas Stearns Eliot ni 'Vita Visivyokuwa na Maana', 'Msitu Mtakatifu' na 'Jinai Kanisani



Read more »

Uislamu Chaguo Langu


Msikiti mjini Tokyo, JapanMsikiti mjini Tokyo, Japan
‘Mvuto wa kimaanawi wa misikiti ya Waislamu ni jambo ambalo hatua kwa hatua lilinivutia kuelekea katika Uislamu. Nilihisi pia kuwa sauti ya adhana katika misikiti ilikuwa na mvuto wenye kunipa mwongozo kulekea katika uhakika.” Hiyo ni kauli ya Bi.Khaula Nakata. Mjapani huyo alifikia natija kuwa Uislamu ndiyo dini ya haki baada ya kupitia masaibu mengi ambayo hayangeweza kutabirika.  Kabla ya kuujua Uislamu Bi. Nakata anasema alikuwa hajawahi kutafakari kwa kina kuhusu Mwenyezi Mungu na wala hakuona udharura wa suala hilo. Anaendelea kusema kuwa: “Kila kitu kilikuwa kikienda vizuri katika maisha yangu na nilikuwa nikihisi kuwa mambo yote ni shwari kabisa na hivyo niliona kuwa simhitajii Mungu maishani. Lakini ghafla nilianza kuhisi kuwa maisha yangu yalikuwa ni ya kujikariri pasina kuwepo na mwelekeo maalumu. Nilifikia natija kuwa maisha yangu hayakuwa na maana. Hivyo nilianza kufanya utafiti kwa lengo la kufikia uhakika. Wakati nikiwa mwanafunzi wa chuo kikuu, wahubiri kadhaa walikuwa wakinitembelea nyumbani. Wakati huo kulikuwapo mwanamke mhubiri Mkristo ambaye alikuwa daima anakuja kunitembelea na kunifunza Injili. Pamoja na aliyonifunza lakini sikuweza kupata kile nilichokuwa nikifuata.”.
Bi. Khaula Nakata anaendelea kusema kuwa: “Baada ya muda, niliamua kufuata dini ya Kibudha. Katika mji wa Kyoto niliupokuwa nikiishi Japan kulikuwa na athari nyingi za kihistoria. Karibu na nyumba yangu kulikuwa na hekalu na hivyo nilikuwa nikienda hapo kila asubuhi kwa ajili maombi. Niliendeleza mkondo huo kwa muda wa miezi mitatu. Sikuchelewa hata siku moja kufika katika hekalu hiyo. Nilikuwa nikitafuta ukweli maishani. Ilikuwa ivugmu kwangu kuzingatia kwa kina wakati nikiomba dua. Hatimaye nilifikia natija kuwa yalimokuwa hatika hekalu la kibudha yalikuwa mbali na uhalisia wa mambo katika dunia.”
Katika kipindi hicho Bi. Khaula Nakata aliamua kuendeleza masomo ya juu nchini Ufaransa badala ya Japan. Mwislamu huyo kutoka Japan anabainisha hivi kuhusu moja ya sababu zilizompelekea kuikubali dini tukufu ya Kiislamu: 'Katika zama ambazo nilikuwa bado sijauchagua Uislamu, kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu wasichana wanaovaa Hijabu katika shule za Ufaransa na mjadala huo ungalipo. Wengi waliamini kuwa shule za serikali Ufaransa hazipaswi kujihusisha na itikadi za kidini za wanafunzi. Mimi pia wakati huo nikiwa kama mtu asiyekuwa Mwislamu, nilitafakakari na kujiuliza ni kwa nini wakuu wa shule wanachukua msimamo mkali kuhusu suala dogo kama vile mtandio wa wanafunzi.
Wasiokuwa Waislamu wamekuwa na dhana potofu kuwa wanawake Waislamu wanalazimishwa kutii sheria za Kiislamu na ndio sababu wanavaa Hijabu. Kwa msingi huo wasiokuwa Waislamu wamekuwa wakiitazama Hijabu ya wanawake Waislamu kama nembo ya dhulma na kudai kuwa uhuru wa mwanamke unapatikana tu kwa kutovaa Hijabu. Hii ni katika hali ambayo wanawake wengi wasiokuwa Waislamu duniani, baada ya kusilimu, hutazama uvaaji Hijabu kama sheria ya kimantiki ya dini. Mimi pia ni mfano wa wanawake hawa. Hijabu yangu si sehemu ya utambulisho wangu wa kijadi au kirangi wala haina maana ya kisiasa au kijamii; vazl la Hijabu yangu ni utambulisho wangu wa kidini. Nilipoamua kuikumbatia dini ya Kiislamu, kamwe sikudhani kuwa siku moja ningeweza kusimamisha sala tano kwa siku au ningeweza kulinda Hijabu yangu. Raghba na hamu yangu ya kuwa Mwislamu ilikuwa na nguvu kubwa kiasi kwamba sikuwa na wasiwasi kuhusu mabadiliko ambayo yalikuwa yanakuja.'
Bi. Nakata Khaula anasema hivi kuhusu nama alivyosilimu na kuvaa Hijabu: 'Baada ya kusikiliza hotuba katika Msikiti wa Paris, nilifahamu faida za kuchunga vazi la Hijabu kiasi kwamba hata baada ya kuondoka msikitini, niliendelea kuvaa mtandio ambao nilikuwa nimeuvaa kwa ajli ya kuuheshimu msikiti. Hotuba hiyo ilinighirikisha katika aina fulani ya ridhaa ya moyoni. Hii ilikuwa ni hali ya kipekee ambayo nilikuwa sijawahi kuihisi. Kwa hakika hisia hiyo ilinifanya nisitake kuondoka msikitini bila mtandio. Mavazi hayo yangu hayakuzingatiwa na watu wakati huo kutokana na kuwa hali ya hewa ilikuwa ya baridi kali. Pamoja na hayo nilikuwa na hisia nzito iliyoniambia kuwa nilikuwa tofauti na wengine, nilipata hisia ya utakasifu na usalama.'
Ingawa kabla ya kusilimu Bi. Nakata Khaula aliitazama hijabu kama kizingiti, lakini leo yeye ni mwanamke ambaye anaheshimu kikamilifu vazi la Hijabu ya Kiislamu. Anayatazama mavazi yake kuwa yenye thamani ya kimaanawi na yanayoashiria imani yake ya kidini. Kuhusiana na hili hiyo anasema: "Kutokana na kuheshimu vazi la Hijabu ninapata furaha na ridhaa. Suala hili ni ishara ya kutii amri ya Mwenyezi Mungu na imani yangu. Hakuna tena haja ya kuitangaza itikadi yangu kwa sauti kubwa, kwa sababu vazi langu  linawabainishia wote imani yangu. Hijabu inawakumbusha watu kuwa Mwenyezi Mungu yupo na daima inanikumbusha kuwa mwenendo wangu unapaswa kuwa ule wa mwanamke Mwislamu. Ni sawa na maafisa wa polisi ambao wakiwa wamevalia sare zao za kazi, huwa waangalifu zaidi kwa hivyo mimi pia ninapovaa Hijab ninapata hisia zaidi ya kuwa Mwislamu.'
Bik Nakata pia anasema mbali na vazi la Hijabu, anavutiwa sana na Swala katika Uislamu. Anasema Swala ni amali ambayo inaimarisha imani ya mwanadamu. Bi. Nakata anasema baada ya kusilimu, wakati aliposwali na kusujudu kwa mara ya kwanza katika ardhi akimshukuru Allah SWT, hakuweza kuinua kichwa chake haraka kutoka kwenye sijda. Anasema kila mara anaposujudu imani yake inaimarika zaidi. Mjapani huyu aliyesilimu anasema alienda Misri kujifunza lugha ya Kiarabu ili aweze kuufahamu vizuri na kikamilifu zaidi Uislamu. Kuhusu uwezo wake wa kusoma Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kiarabu anasema: “Hivi sasa naweza kuisoma Qur’ani kwa umaridadi. Mbali na maudhui mbalimbali zinazojadiliwa katika kitabu hiki, mimi pia navutiwa na mtirikio wake wenye mvuto wa kipekee. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunineemesha na kunipa taufiki ya kuwa Mwislamu na nitajitahidi kuwafunza Wajapani Uislamu. Nataka nao pia wapate furaha kama niliyonayo katika Uislamu. Mimi ninaamini kuwa kwa kumwamani kikamilifu na kumtegemea Mwenyezi Mungu, kila tatizo lina weza kutatuliwa”
Read more »

Sunday, September 21

TAFSIRI YA QURA'AN


Sura ya Al Furqan, aya ya 41-44 (Darsa ya 628)



Wasikilizaji wapenzi wa Darsa ya Qur'ani, Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh. Bismillahir Rahmanir Rahim. Hamdu na sifa zote njema zinamstahikia Allah SW, na rehma na amani zimshukie Mtume wake Mtukufu na Aali zake watoharifu. Kwa taufiki yake Mola Karima aliyetupa uhai na uzima tumekutana tena katika mfululizo mwengine wa Darsa ya Qur'ani. Hii ni darsa ya 628 na sura tunayoizungumzia hivi sasa ni ya 25 ya Al Furqan. Tunaianza darsa yetu hii kwa aya ya 41 na 42 ambazo zinasema:

وَإِذَا رَأَوْكَ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلاَّ هُزُوًا أَهَذَا الَّذِي بَعَثَ اللَّهُ رَسُولا

Na wanapokuona hawakufanyii ila kejeli tu, (kwa kusema): Ati huyu ndiye Mwenyezi Mungu aliyemtuma kuwa Mtume?

إِن كَادَ لَيُضِلُّنَا عَنْ آلِهَتِنَا لَوْلا أَن صَبَرْنَا عَلَيْهَا وَسَوْفَ يَعْلَمُونَ حِينَ يَرَوْنَ الْعَذَابَ مَنْ أَضَلُّ سَبِيلا

Kwa hakika alikuwa karibu kutupoteza tuiache miungu yetu, kama tusingelishikamana nayo kwa kuvumilia. Na karibu watajua watakapoiona adhabu, ni nani aliyepotea njia.
Aya tulizozitolea ufafanuzi kwenye darsa iliyopita zilizungumzia muamala wa washirikina kwa Bwana Mtume Muhammad SAW. Aya hizi tulizosoma zinaendelea kuzungumzia maudhui hiyo kwa kusema: wakati watu hao walipokuwa wakikutana na Bwana Mtume, badala ya kuyasikiliza maneno yake ya haki na ya mantiki, na kuyataamali na kuyatafakari maneno hayo, kitu pekee walichokuwa wakifanya ilikuwa ni kusema kwa kejeli na istihzai kwamba Mwenyezi Mungu ndo amemfanya mtu huyu awe Mtume wetu? Mtu ambaye hana mali wala cheo, na tangu utotoni mwake amekulia katika uyatima? Ikiwa sisi hatutoshikamana na masanamu yetu atatupotosha mara moja na kutuweka mbali na dini ya wazee wetu waliotutangulia.
Mwenyezi Mungu SW akayajibu maneno hayo yasiyo na mantiki wala nadhari ya waabudu masanamu kwa kusema: mtakapoziona ishara za adhabu, wakati huo ndipo mtapofahamu kama ni Mtume au nyinyi ndio mliokuwa katika upotofu! Hivi kweli mnamwita kuwa ni mtu aliyepotoka, Mtume ambaye ameishi pamoja nanyi kwa miaka na miaka, hali ya kuwa hamjawahi kuona chochote kwake yeye ghairi ya ukweli na uaminifu? Kisha nyinyi wenyewe ambao hamna hoja yoyote ya kukufanyeni muabudu masanamu ghairi ya kusema mnafuata dini ya waliokutangulieni, ndio mnajiona ni watu mlioongoka?
Baadhi ya mafunzo tunayopata kutokana na aya hizi ni kwamba wale ambao si wenye hoja na mantiki huwa hawana njia nyengine ya kufanya isipokuwa kuwakejeli na kutaka kuwadunisha waja wema wa Allah, na hii ndio mbinu ya kudumu ya makafiri. Funzo jengine tunalopata kutokana na aya hizi ni kuwa mtu mkaidi na mwenye ghururi hawi tayari kuikubali haki. Na ndiyo maana chanzo cha ukafiri na ukanushaji wa watu wengi ni ukaidi wao na si udhaifu wa hoja zinazotolewa na wafuasi wa tauhidi na Mola mmoja wa haki. Kadhalika tunajielimisha kutokana na aya hizi kwamba kusimama imara na kudumu katika njia ya haki ndilo jambo lenye thamani, si kuwa mshupavu katika njia ya batili ambako ni kuwa mkaidi na kufanya taasubu zisizo na msingi.
Ifuatayo sasa ni aya ya 43 ambayo inasema:

أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَهَهُ هَوَاهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلا

Je! Umemwona aliyeyafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake?
Aya hii inamhutubu Bwana Mtume kuwa washirikina na makafiri hawayakubali maneno yako kwa sababu hayaafikiani na hawaa, utashi na matamanio yao ya nafsi. Wao wanataka wafanye kila kile zinachotaka na kutamani nafsi zao wala hawajali uzuri na ubaya wa kitu hicho. Lililo muhimu kwao wao ni kukidhi matamanio ya kighariza, na si hata kile kinachofahamika na kukubaliwa na akili zao. Kwa hiyo wewe Mtume usiwe na tamaa kwamba watu walioamua kukinzana na akili, fitra na maumbile yao, watakubali kusikiliza na kuyakubali maneno yako na kuufuata uongofu unaowafikishia. Miongoni mwa mafunzo tunayopata kutokana na aya hii ni kwamba chanzo cha ukafiri na shirki ni kuabudu hawaa na matamanio ya nafsi na si mantiki na hoja za kiakili. Funzo jengine tunalopata kutokana na aya hii ni kuwa kiu ya kumjua Mungu imo ndani ya fitra na maumbile ya kila mtu, lakini baadhi ya watu hukosea katika kufikia kwenye misdaqi na kielelezo chake halisi ambacho ni Allah SW, Mola pekee wa ulimwengu. Aidha aya hii inatuonyesha kuwa imani huwa na thamani inapotokana na hiyari; na si kwa kulazimishwa na kutezwa nguvu. Kwa hivyo Mitume si mawakili na wasimamizi wa watu; na kwa hivyo hawawezi kutumia mbinu ya ulazimishiaji na utezaji nguvu kwa ajili ya kuwaelekeza watu hao kwenye njia ya uongofu.
Darsa yetu ya leo inahatimishwa na aya ya 44 ambayo inasema:

أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ إِنْ هُمْ إِلاَّ كَالأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلا

Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanatumia akili? Hao hawakuwa ila ni kama wanyama hoa tu; bali wao wamepotea zaidi njia.
Aya hii inamliwaza Bwana Mtume na waumini kwa kuwaambia kwamba msiudhike kwa maneno na mwenendo muovu wa washirikina na wala msiwasikitie bure watu hao kwa sababu wao hawazirejei akili zao ili waweze kuifahamu haki na wala hawana masikio ya kusikia, kuwafanya wawe tayari kusikiliza maneno ya haki na kuyakubali. Katika hali hiyo, wao ni mithili ya wanyama hoa wa miguu minne ambao si maneno ya wamiliki wao ambayo wanayafahamu, wala si hisi ambazo wanazo za kuwawezesha kuchukua uamuzi na kufanya jambo kutokana na hisi hizo. Ukweli ni kwamba kama tutalizingatia hilo kwa makini, wao ni watu waliopotea zaidi kuliko hata wanyama. Kwa sababu wanyama wanaishi namna hivyo kwa kutokuwa na nyenzo za hisi na ufahamu, na wala hawana uwezo wa kujitutumua zaidi ya vile walivyo. Lakini kinyume chake, wanadamu wamejaaliwa fitra na akili, na suhula na nyenzo za kuukuza uwezo wao wa kuelewa na kufahamu mambo lakini baadhi yao hawazitumii neema hizo. Katika kuamiliana na makafiri na wapinzani wa haki, Qur'ani tukufu inaonyesha kuwa na insafu kwa kueleza kwamba akthari ya watu hao wako hivyo lakini si wote, ili kupambanua hukumu ya wale wanaopotoka kwa kuhadaika na kudanganyika na wengineo wasiokuwa hao. Baadhi ya mafunzo tunayopata kutokana na aya hii ni kwamba wanyama hawana akili ya kufahamu na kupambanua baina ya jema na baya au kati ya haki na batili; lakini watu wanaopotoka, licha ya kujaaliwa kuwa na akili ima hawashughuliki kuitafuta na kuifahamu haki na batili au wanaijua haki ni ipi lakini wanaikengeuka na kuipa mgongo. Funzo jengine tunalopata kutokana na aya hii ni kuwa njia ya kuufikia uongofu ni kusikiliza wito wa haki na kuutafakari. Wahyi ni hoja na mwongozo wa nje ambao kama utapenya ndani ya sikio la mtu utakamilisha nafasi ya hoja ya ndani ambayo ni akili aliyopewa mtu. Kadhalika aya hii inatuelimisha kwamba mtu anayeukubali uongofu wa Allah huwa na heshima ya utu na ubinadamu, na mtu anayeamua kuipinga haki huwa duni mbele ya Mola kuliko hata mnyama. Kwa haya machache wapenzi wasikilizaji tunaifunga darsa yetu hii. Tunamwomba Mola atuonyeshe haki na atupe taufiki ya kuifuata, na atuonyeshe batili na atuwezeshe kuiepuka.
Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh...
Read more »

Mada


Read more »

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com