
Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema kuwa, kuna udharura wa kuweko vita vya kimataifa dhidi ya magaidi. Rais Assad amesisitiza kwamba, kwa sasa eneo la Mashariki ya Kati linapitia kipindi nyeti mno lakini kile ambacho kitaainisha njia ya marhala hii ni kusimama kidete taifa la Syria. Ameongeza kuwa, mustakabali wa Mashariki ya Kati utaainishwa kwa kusimama kidete wananchi wa Syria katika kupambana na makundi ya kigaidi sambamba na himaya kwa taifa hilo ya nchi marafiki na Syria. Rais wa Syria amebainisha kwamba, ili ugaidi na makundi ya kigaidi vitokomezwe kuna haja ya kuweko vita vya kimataifa tena vyenye nia safi na ya dhati ya kupambana na ugaidi.
Rais Bashar al-Assad amesisitiza kwamba, taifa la Syria halitasalimu amri, bali litaendelea kupambana na makundi ya kigaidi katika nchi hiyo ambayo mbali na kuhatarisha usalama wa nchi yametenda jinai kubwa dhidi ya binadamu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Wakati huo huo ripoti kutoka Syria zinaonesha kuwa, jeshi la nchi hiyo limeendelea kupata mafanikio katika operesheni zake za kijeshi za kupambana na makundi ya kigaidi.
0 toamaon yako: