Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Saturday, April 1

Mali ya Ivanka Trump na mumewe yafichuliwa

Mali ya Ivanka Trump na mumewe yafichuliwaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMali ya Ivanka Trump na mumewe yafichuliwa
Ikulu ya Marekani, imetoa maelezo kuhusu mali ya binafsi ya watu waliomo katika serikali ya Rais Donald Trump.
Mali hiyo imedhihirishwa kama sheria inavyoelekeza, na inaonyesha kuwa mtoto wa rais wa kike, Ivanka pamoja na mumewe, wana kama dola milioni 740.
Piya imetangazwa kuwa mshauri mkuu wa rais kuhusu uchumi, Gary Cohn, ana kama dola robo bilioni.
Read more »

Saturday, August 8

Babake mtoto Mpalestina aliyechomwa, ameaga











Babake mtoto wa kipalestina aliyechomwa moto hadi akafa juma lililopita na walowezi wa kiyahudi katika maeneo yaliyokaliwa ya ukingo wa magharibi (West Bank) ameaga dunia.

Sa'ad Dawabsheh ameaga dunia katika hospitali ya Soroka iliyoko Israeli.

Babake mtoto Mpalestina aliyechomwa moto akafa ameaga dunia 


Bwana Dawabsheh alipelekwa Israeli ilikupata matibabu baada ya kuungua katika shambulizi
lililoteketeza mtoto wake mchanga wa mwaka mmoja u nusu.

Shambulizi hilo lililotekelezwa na walowezi wa Kiyahudi lilimuacha bwana Dawabsheh mke wake na mwana wao mwenye umri wa miaka 4 wakiuguza majereha mabaya.

Mke wake bi Riham na mwana wao Ahmad bado wako katika hali mahututi.

Nyumba yao ilichomwa moto katika shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na walowezi wa kiyahudi 

Shambulizi hilo lililotokea mwisho wa mwezi Julai liliibua hasira miongoni mwa Wapalestina na wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu ambao waliilaumu Israeli kwa kukosa kuwajibikia
usalama wa Wapalestina mikononi mwa Walowezi wa kiyahudi.

Wakati wa shambulizi hilo,Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon alitaka wale waliohusika kwenye shambulizi la kumchoma mtoto Mpalestina katika eneo linalokaliwa na Israel la ukingo wa magharibi kufikishwa mbele ya sheria.

Kifo cha mtoto huyo kiliibua hasira na maandamano 

Waziri mkuu wa Israel Benjamin aliahidi kuwa wale waliotekeleza kitendo hicho alichokitaja kuwa cha kigaidi wangechukuliwa hatua za kisheria.
Netanyahu alielezea mshangao wake kutokana ni kile alichokitaja kuwa mauaji ya kikatili alipowatembelea wazazi wa mtoto huyo na nduguye hospitalini.
Afisa wa Palestina, Ghassan Daghlas, alisema walowezi wa Israil, walichoma moto nyumba nyengine katika kijiji cha Duma hii leo, lakini hakuna mtu aliyeumia vibaya.
Umoja wa Mataifa unasema walowezi wa Israil wamefanya mashambulio kama 120 mwaka huu, katika Ufukwe wa Magharibi uliokaliwa.
 

 
 
Read more »

Hali ni tete Kabul mabomu yameua watu 41
















Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani anaongoza kikao maalum cha usalama baada ya mashambulizi 
kadha ya kujitolea muhanga yaliyopelekea watu 41 kufa.
Mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, umekumbwa na milipuko kadhaa



Miongoni mwa maeneo yaliyolengwa ni chuo cha maafisa wa polisi, ambapo mtu mmoja aliyekuwa amevalia sare za polisi alijilipua na kuwaua zaidi ya watu 25.
Washambuliaji hao pia walivamia kituo cha wanajeshi wa shirika la kujihami la NATO kilichoko karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa.



Inadaiwa kuwa wawili kati ya washambuliaji hao waliuawa.
Mapema siku ya Ijumaa lori moja lililokuwa limetegwa bomu lililipuka karibu na afisi za serikali na kuwaua watu 15.



Rais Ashraf Khan alisema kuwa mashambulizi hayo yalikuwa ni lengo la Wapiganaji wa Kiislamu wa Taliban kujaribu kuwasahaulisha watu misukosuko inayokumba kundi lao kufuatia tangazo la juma lililopita kuwa mwanzilisi wa kundi hilo,Mullah Omar,alifariki



Read more »

Saturday, March 28

Uchaguzi mkuu wafanyika leo nchini Nigeria

Uchaguzi mkuu wafanyika leo nchini Nigeria
Wananchi waliotimiza masharti ya kupiga kura nchini Nigeria leo wameelekea kwenye vituo vya kupigia kura kwa lengo la kumchagua rais, wabunge na maseneta wa maeneo yao. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Nigeria imetangaza kuwa, karibu watu milioni 68 na laki nane kutoka jumla ya watu milioni 173 wa nchi hiyo walijiandikisha kwenye daftari la kupiga kura nchini humo. Kwenye uchaguzi wa rais, kuna shakhsia 14 watakaochuana vikali kwenye uchaguzi huo ulioanza leo. Duru za habari zinasema, mchuano mkali utakuwa kati ya Rais Goodluck Jonathan kutoka chama tawala cha People's Democratic Party PDP na Jenerali mstaafu Muhammadu Buhari kutoka chama cha All Progressives Congress 'APC'. Rais Jonathan aliyeingia madarakani mwaka 2011, anahesabiwa kuwa rais wa kwanza kutoka kabila la Ijaw na pia ni kiongozi wa kwanza anayetoka eneo la kusini mwa Niger Delta. Buhari aliwahi kuiongoza Nigeria kuanzia mwaka 1983 hadi 1993 wakati nchi hiyo ilipokuwa ikitawaliwa na majenerali wa kijeshi. Buhari ameikosoa serikali ya Jonathan kwa kushindwa kulitokomeza kundi la kigaidi la Boko Haram pamoja na kuongezeka vitendo vya ufisadi wa kiserikali, umasikini na ukosefu wa ajira nchini humo. Taarifa zinasema kuwa, wasimamizi kutoka Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa wako nchini Nigeria kwa lengo la kusimamia zoezi hilo
Read more »

Takwa la nchi za Amerika ya Latini la kuondolewa vitisho vya Marekani dhidi ya Venezuela

Takwa la nchi za Amerika ya Latini la kuondolewa vitisho vya Marekani dhidi ya VenezuelaKufuatia kuwekwa vikwazo vipya dhidi ya shakhsia kadhaa wa Venezuela na halikadhalika vitisho vya kiusalama vya 
Rais Barack Obama dhidi ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini, raia na serikali kadhaa za eneo hilo zimekosoa vikali siasa za rais huyo wa Marekani. Jamii ya nchi za Amerika ya Latini na zile za Bahari ya Caribbean kwa pamoja, zimepinga hatua na amri ya Rais Obama aliyeitaja Venezuela kuwa ni tishio la kiusalama dhidi ya Washington. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ecuador Ricardo Patino ambaye nchi yake inashikilia uogozi wa Jumuiya ya nchi za Amerika ya Latini na visiwa vya Caribbean, ametangaza kuwa wanachama wote 33 wa jumuiya hiyo wanataka kuondolewa amri hiyo na badala yake kufanyike mazungumzo yatakayozingatia misingi ya kimataifa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ecuador ameongeza kuwa, mbali na wanachama wa jumuiya hiyo iliyotajwa, Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote kwa kifupi (NAM) siku ya Jumatano iliyopita, iliitaka pia Washington kubatilisha hukumu yake hiyo dhidi ya taifa la Venezuela. Kwa upande wake Rais Juan Evo Morales wa Bolivia ameelezea hatua ya Rais Barack Obama kuitaja Vinezuela kuwa tishio kwa nchi yake, kuwa ni kosa kubwa. Amesema kuwa hatua hiyo ni sawa na kuzitaja nchi zote za Amerika ya Latini kuwa tishio kwa maslahi ya Marekani na mfumo wake wa kibepari kutokana na nchi hizo kupinga kuporwa utajiri wao na Washington. Katika kikao cha mwisho cha nchi wanachama wa muungano wa ALBA kilichofanyika tarehe 18 mwezi Machi mwaka huu, washiriki walimtaka rais huyo wa Marekani kufutulia mbali amri hiyo iliyoitaja serikali ya Caracas kuwa tishio lisilo la kawaida kwa usalama wake. Ripoti hiyo ilieleza kuwa, Venezuela sio tishio kwa nchi yoyote na kinyume chake wananchi wake wameonyesha irada thabiti kwa ajili ya kuendeleza ushirikiano na mataifa mengine kieneo na kimataifa kwa ujumla. Muungano wa ALBA unaundwa na nchi za Amerika ya Latini ikiwemo Cuba, Venezuela, Bolivia, Ecuador, Nicaragua, Jamhuri ya Watu wa Dominican, Saint Vincent na Granadyn, St Lucia, Granada, Antigua na Barbara, St. Christopher na Saint Kitts na Nevis. Kabla ya hapo pia na katika kikao kilichofanyika mjini QuitoEcuador muungano huo ulizitaka nchi wanachama wa mataifa ya Amerika ya Kusini unaofahamika kwa jina la Union de Naciones Suramericanas (UNASUR) kufanya juhudi za kuhakikisha vikwazo walivyowekewa shakhsia kadhaa wa Vinezuela vinaondolewa. Itakumbukwa kuwa tarehe Ttisa mwezi huu wa Machi, Rais Barack Obama alitoa amri ambayo iliitaja Venezuela kuwa tishio kwa usalama wake, amri ambayo iliambatana na kuyaweka katika orodha ya vikwazo, majina kadhaa ya viongozi wa nchi hiyo. Katika kujibu hatua hiyo, Caracas iliwaita maafisa wa ubalozi wake mjini Washington, huku Baraza la Kitaifa la Venezuela likimpa rais wa nchi hiyo uwezo maalumu kwa ajili ya kukabiliana na hujuma za ubeberu wa Marekani. Kufuatia amri hiyo wanaharakati wa asasi za kiraia nchini humo walianzisha kampeni iliyopewa jina la 'Venezuela sio Tishio' kampeni ambayo kwa muda wa siku nne tu zilizopita tayari imetiwa saini na watu milioni moja, katika kupinga siasa za rais wa Marekani dhidi ya taifa lao
Read more »

Wednesday, March 25

Majaribio ya kombora la balestiki nchini Marekani

Majaribio ya kombora la balestiki nchini Marekani

Jeshi la Anga la Marekani limetangaza kuwa limefanyia majaribio kombora la balestiki linaloweza kuvuka mabara na kwamba majaribio hayo ni ujumbe kwa walimwengu kuhusu uwezo wa silaha za nyuklia wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Anga la Marekani, kombora la Minuteman-III lilifanyiwa majaribio mapema Jumatatu katika kituo cha Jeshi la Anga cha Vandenberg huko California. Taarifa ya Jeshi la Anga la Marekani imesema: Majaribio hayo ya kombola la balestiki la nyuklia yanaonesha picha ya wazi kwa walimwengu kuhusu uwezo wa kombora ya Minuteman-III ambalo linaweza kulenga mahala popote.
Kwa kutilia maanani kwamba Jeshi la Anga la Marekani haliwezi kutumia makombora ya Peace Keeper kwa mujibu wa makubaliano ya silaha ya START II (Strategic Arms Reduction Treaty), kombora la Minuteman-III  litakuwa kombora pekee la balestiki linaloweza kuvuka mabara la jeshi la Marekani. Kombora hilo linavishwa kichwa cha silaha ya nyuklia aina ya W87 ambacho kina uwezo mkubwa wa uharibifu. Majaribio hayo yamefanyika sambamba na mazoezi ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na majeshi ya shirika la NATO huko Ulaya mashariki.
Inaonekana kuwa kwa majaribio ya kombora hilo la nyuklia, jeshi la Anga la Marekani linafuatilia malengo kadhaa.
Kwanza ni kuwa Marekani inataka kuonesha misuli na uwezo wake wa silaha za nyuklia kwa wapinzani wake wakubwa hususan Russia. Katika kipindi cha miaka kama miwili iliyopita jeshi la Russia limefanya majaribio mtawalia ya makombora yanayoweza kuvuka mabara (Intercontinental Ballistic Missile au IBM) na hata kurusha makombora kama hayo kwa kutumia nyambizi. Kwa msingi huo Marekani ilikuwa ikinyemelea fursa ya kukabiliana na majaribio hayo ya silaha za nyuklia ya Russia.
Suala la pili ni kushadidi mivutano baina ya Russia na NATO huko Ulaya Mashariki ambako kumezifanya pande hizi mbili zijizatiti kwa silaha na majeshi katika eneo hilo na katika Bahari Nyeusi. Kwa msingi huo Marekani inataka kumuonesha adui wake yaani Russia, kwamba iwapo mgogoro huo utaendelea inaweza kutumia silaha zake za nyuklia.
Marekani ni miongoni mwa wamiliki wakubwa zaidi wa silaha za nyuklia duniani na ndiyo nchi pekee ambayo hadi sasa imetumia silaha hizo kuua watu wa taifa jingine. Nchi hiyo kinyume na ahadi zake za kupunguza maghala yake ya silaha za nyuklia, ingali inastawisha na kupanua zaidi silaha hizo na kuzifanyia majaribio. Marekani pia inasasisha na kuziboresha zaidi silaha zake za zamani za nyuklia licha ya harakati za kimataifa za kupunguza silaha hizo husuan mkataba wa NPT unaosisitiza kupunguzwa na hatimaye kuangamizwa kabisa silaha hizo. Katika uwanja huo Washington imetenga bajeti ya dola bilioni 355 ambazo zitatumika kusasisha na kuboresha mitambo yake ya silaha na kuinua juu kiwango cha majaribio ya silaha za nyuklia. Vilevile Marekani imechukua hatua za kuboresha silaha na maghala yake ya zana za nyuklia barani Ulaya yakiwemo mabomu ya nyuklia ya B-61.
Kwa utaratibu huo, Washington, kinyume na mikataba ya kimataifa ya kuzuia uzalishaji wa silaha za nyuklia, inaendelea kuzalisha na kufanyia majaribio silaha za aina hiyo, suala ambalo linakiuka mkataba wa NPT. 
Read more »

Jumatano, Machi 25, 2015

  •  
  • Jumatano, Machi 25, 2015
Leo ni Jumatano tarehe 4 Jamadithani 1436 Hijria sawa na Machi 25, 2015.
Siku kama hii ya leo miaka 21 iliyopita, vikosi vya jeshi la Marekani ambavyo mwezi Disemba 1992 viliivamia Somalia kwa kisingizio cha kukomesha uasi nchini humo, hatimaye vililazimika kuondoka katika nchi hiyo baada ya kushindwa vibaya. Mwaka 1991 makundi mbalimbali ya Somalia yalimpindua dikteta wa nchi hiyo Muhammad Siad Barre. Hata hivyo makundi hayo yalishindwa kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya mseto na mkwamo huo wa kisiasa ukapelekea kuzuka vita vya ndani nchini humo. Marekani ilituma wanajeshi wake huko Somalia katika fremu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa ili kulinda maslahi yake nchini humo, kutokana na nafasi muhimu ya Somalia katika eneo la Pembe ya Afrika. Askari wa Marekani walikabiliwa na mapambano makali ya Wasomali na kupoteza askari karibu 100.


Tarehe 25 Machi miaka 40 iliyopita Mfalme wa wakati huo wa Saudi Arabia, Faisal bin Abdulaziz, aliuawa na mwana wa ndugu yake mwenyewe, Faisal bin Saaid bin Abdulaziz. Faisal bin Saaid alifanya mauaji hayo akilalamikia kupunguzwa kwa mshahara wake. Japokuwa hitilafu katika kizazi cha wafalme wa Saudi Arabia zimekuwepo siku zote na zimekuwa zikipamba moto mara kwa mara lakini mauaji ya Mfalme Faisal yalikuwa ya kwanza ya mfalme wa nchi hiyo kutokana na hitilafu kama hizo. Muuaji wa Mfalme Faisal pia alikatwa kichwa mbele ya umati wa watu tarehe 18 Juni mwaka 1975. Baada ya Faisal, Khalid mwana mwingine wa Abdulaziz alishika kiti cha ufalme wa Saudi Arabia.


Na miaka 58 iliyopita mwafaka na siku hii ya leo mkataba wa kuasisi Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya au kwa jina jingine Soko la Pamoja la Ulaya ulisainiwa huko Roma mji mkuu wa Italia kati ya wawakilishi wa nchi mbalimbali za bara hilo. Jumuiya hiyo iliundwa kwa lengo la kuasisi umoja wa forodha kati ya nchi wanachama ili kufuta ushuru wa bidhaa na baada ya hapo, ubadilishanaji wa bidhaa, nguvu kazi, vitega uchumi na huduma nyinginezo pia ukawa huru kati ya nchi wanachama. Jumuiya hiyo ilikuwa utangulizi wa kuundwa Umoja wa Ulaya mwaka 1992.
Read more »

Monday, March 23

Mvua yasababisha vito vya watu 5 Dar es Salaam

Mvua yasababisha vito vya watu 5 Dar es Salaam  
 Hali tete inatawala katika jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania kutokana na mvua ya masika iliyonyesha kwa siku tatu na kusababisha vifo vya watu watano, huku nyumba nyingi zikiwa zimezingirwa na maji. Maeneo yaliyoathirika zaidi katika mji huo ni Buguruni kwa Mnyamani na eneo la Jangwani katika Manispaa ya Ilala, ambako nyumba nyingi na barabara zimeathirika. Sehemu nyingine za jiji la Dar es Salaam zimezingirwa na maji kutokana na kuziba kwa mitaro na mifereji, ikiwa ni athari ya utupaji taka ovyo na pia miundombinu duni. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), mvua kubwa zaidi zinatarajia kuendelea kunyesha mpaka siku ya Jumatano. Kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha, Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki jana aliongoza kikosi cha uokoaji katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ambako nyumba 250 zilizingirwa na maji, jambo ambalo vikosi vya uokoaji vililazimika kufanya kazi ya kuwanasua watu waliokuwa wamekwama katika nyumba zao. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa, hadi kufikia jana mvua hizo zilikuwa zimesababisha vifo vya watu watano, akiwemo mtu mmoja aliyesombwa na maji, mwingine aliyeangukiwa na ukuta na watatu ambao walinaswa na umeme baada ya nguzo ya umeme kuanguka Mbagala Mzambarauni katika Manispaa ya Temeke.
Read more »

Monday, February 2

nibaada ya kituo cha 100.0 iqra fm elimu na matendo kuto weka hewan kuto kwa sababu za  kifaa ufund kukosekama
nkinacho itwa filta kutua nchin tanzania na tayali kimesha fungwa ka mkao wa kula
Read more »

Thursday, December 4

Jumatatu, Desemba Mosi, 2014

Jumanne, Novemba 25, 2014Leo ni Jumatatu tarehe 8 Safar mwaka 1436 Hijiria, inayosadifiana na tarehe Mosi Disemba mwaka 2014 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 1401 iliyopita, aliaga dunia Salman Farsi, mmoja kati ya maswahaba wakubwa wa Bwana Mtume (SAW). Salman alikuwa Muirani wa kwanza kuingia katika dini ya Kiislamu na kukubali mafundisho ya Nabii Muhammad (SAW). Salman Farsi alifanya jitihada kubwa za kujipamba kwa maadili mema, takwa na ucha-Mungu hadi kuwa miongoni mwa maswahaba wa karibu wa Mtume.  Bwana Mtume Mtukufu (SAW) anamtaja Salman Farsi kuwa miongoni mwa Ahlubaiti wake. Swahaba huyo mwema alikuwa bega kwa bega na Mtume Mtukufu katika vita vya kutetea Uislamu. Swahaba huyo aliendelea kuwa karibu na Ahlulbait wa Mtume (SAW) baada ya mtukufu huyo kuaga dunia.
Miaka 117 iliyopita  muwafaka na leo, yaani tarehe Mosi Disemba mwaka 1897 Miladia, ulitiwa saini mkataba wa kihistoria mashuhuri kwa jina la mkataba wa "Kutokuweko Mapigano" kati ya Italia na mojawapo ya jamhuri ndogo zaidi duniani kwa jina San Marino, ambayo inazungukwa na Italia kusini mwa bara Ulaya. Kwa mujibu wa mkataba huo, Jamhuri ya San Marino iliahidi kutoishambulia Italia na Italia pia kuahidi kuheshimu uhuru wa nchi hiyo ndogo.
Miaka 189 sawa na leo, Muungano wa kihistoria wa nchi za Ulaya ulisambaratika baada ya kujiengua utawala wa Kikaitsar (Tsarist) wa Russia katika muungano huo. Baada ya kuanguka kwa utawala wa Napoleon, muungano huo ukaunda Congress ya Vienna, kati ya tawala za Russia, Austria na ufalme wa Pros na serikali hizo zikaafikiana kwamba nchi zilizo chini ya utawala wa muungano huo na katika uhusiano wa kimataifa zifuate misingi ya dini ya Kikristo.
Na katika siku kama ya leo kila ifikapo tarehe Mosi mwezi Disemba kila mwaka, nchi mbalimbali duniani huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Ukimwi. Kuweko Siku ya kimataifa ya Ukimwi kulifikiriwa kwa mara ya kwanza mwezi Agosti mwaka 1987 na James W.Bunn na Thomas Netter, maafisa wawili wa habari wa Kitengo cha Kimataifa cha Kupambana na Ukimwi cha Shirika la Afya Duniani (WHO) huko Geneva Uswisi. Maafisa hao wawili waliwasilisha wazo hilo kwa Dakta Jonathan Mann, Mkurugenzi wa Shirika la UNAIDS na baadaye akakubali pendekezo hilo, na kuliidhinisha. Na hatimaye akaafiki siku ya kwanza ya kimataifa ya Ukimwi iadhimishwe duniani kote tarehe Mosi Disemba mwaka 1988. Kuanzia wakati huo kila mwaka siku ya kimataifa ya Ukimwi huadhimishwa duniani kote kila ifikapo tarehe Mosi Disemba.
Read more »

Rwasa aitahadharisha serikali Burundi na machafuko

Rwasa aitahadharisha serikali Burundi na machafukoKiongozi wa chama cha upinzani cha FNL nchini Burundi ametahadharisha kuwa, taifa hilo linaweza kutumbukia kwenye ghasia na machafuko iwapo serikali haitowasikiza wadau katika siasa za nchi hiyo. Akizungumza kwenye mahojiano maalum na Idhaa hii, Agathon Rwasa amesema kuwa, mchakato wa kuandaa daftari la wapiga kura kupitia uandikishaji wa raia ni zoezi lililovurugika na ameitaka serikali kusitisha zoezi hilo mara moja. Rwasa amesema uchaguzi mkuu ujao unaweza kuwa nukta ya kuwaunganisha Warundi pamoja au kuwagawanya kwa kutegemea jinsi maandalizi yatakavyofanywa. Mkuu wa FNL amesema mustakabali wa siasa nchini Burundi unakumbwa na hatihati na kusisitiza kuwa serikali itabeba dhima iwapo machafuko yatatokea kutokana na upuuzaji wake wa hali ya mambo kwa hivi sasa.
Tayari muungano wa upinzani wa ADC-Ikibiri umejiondoa kwenye zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kufuatia dosari zilizojitokeza na kutishia kususia uchaguzi mkuu wa rais mwakani endapo serikali haitositisha zoezi hilo
Read more »

Yemen na ukwepaji jukumu la kulinda maisha ya wanadiplomasia wa Iran

Yemen na ukwepaji jukumu la kulinda maisha ya wanadiplomasia wa IranKatika kuendelea kujiri matukio yanayotokana na kutojali serikali ya Yemen kulinda maisha ya wanadiplomasia na majengo ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, makazi ya balozi wa Iran katika mji mkuu wa nchi hiyo Sana'a jana yalilengwa na shambulio la kigaidi. Kwa mujibu wa duru za Yemen watu wasiopungua watatu akiwemo mlinzi wa nyumba ya balozi ambaye ni raia wa Yemen waliuawa na wengine kumi na saba walijeruhiwa, baadhi yao wakiwa mahututi kutokana na mripuko wa gari lililotegwa bomu ndani yake ambalo lilikuwa limeegeshwa karibu na nyumba ya Sayyid Hassan Niknam, balozi wa Iran mjini Sana'a. Balozi wa Iran hakuwepo nyumbani kwake wakati wa shambulio hilo ambalo lilisababisha pia hasara kubwa kwa nyumba za jirani na magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu na mahali ulipotokea mripuko huo wa bomu. Kufuatia tukio hilo balozi mdogo wa Yemen hapa nchini alitakiwa kufika Wizara ya Mambo ya Nje hapa mjini Tehran. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya nchi za Kiarabu na za Kiafrika, Hussein Amir Abdolahian ameashiria kuitwa balozi huyo mdogo wa Yemen na kueleza kwamba Wizara ya Mambo ya Nje imetoa indhari na sisitizo kubwa kuhusu jukumu la serikali ya Yemen la kulinda usalama wa wanadiplomasia na majengo ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyoko mjini San’aa. Abdolahian ameongeza kuwa balozi mdogo wa Yemen amesisitiziwa kwamba matarajio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuona serikali ya Sana’a inachukua hatua za haraka za kumtambua, kumkamata na kumwadhibu mhusika au wahusika wa shambulio hilo la kigaidi. Shambulio la kigaidi la jana mbele ya makazi ya balozi wa Iran nchini Yemen limetokea katika hali ambayo kabla ya hapo wanadiplomasia wa Iran walishaandamwa na mashambulio kadhaa ya kigaidi ambapo katika kipindi cha karibu mwaka mmoja na nusu uliopita Nour Ahmad Nikbakht, Mwambata wa masuala ya uendeshaji wa ubalozi wa Iran nchini Yemen alitekwa nyara. Na kabla ya tukio la jana, mwanzoni mwa mwaka huu, Ali Asghar Asadi, mwanadiplomasia mwengine wa Iran aliuliwa wakati alipokuwa akikabiliana na magaidi waliokuwa wamedhamiria kumteka nyara. Licha ya ufatiliaji uliofanywa na maafisa wa Iran katika miezi ya hivi karibuni wa kutaka kujua hatima ya Nour Ahmad Nikbakht, Mwambata wa masuala ya uendeshaji wa ubalozi wa Iran mjini San’aa, hadi sasa viongozi wa Yemen hawajatoa jibu la kuridhisha juu ya suala hilo. Nayo Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilishawahi kumwita mara mbili balozi mdogo wa Yemen hapa nchini na kumweleza wasiwasi mkubwa ilionao Tehran juu ya hatima ya mwanadiplomasia wake huyo. Sambamba na hatua hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje Muhammad Javad Zarif alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen pembeni mwa mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, na akasisitiza tena juu ya jukumu ililonalo serikali ya Yemen la kuhakikisha mwanadiplomasia huyo wa Iran anaachiliwa huru haraka iwezekanavyo. Lakini mbali na wanadiplomasia wa Kiiran, wanadiplomasia wa nchi nyengine za kusini mashariki mwa Asia na wa nchi za Ulaya nao pia wamekuwa wakiandamwa na hujuma na mashambulio ya makundi ya kigaidi nchini Yemen. Hata hivyo badala ya viongozi wa serikali ya Yemen kufanya juhudi kwa ajili ya kuachiliwa huru mwanadiplomasia wa Iran aliyetekwa nyara na kuchukua hatua zinazotakiwa ili kulinda maisha ya wanadiplomasia, wamekuwa wakikwepa jukumu lao hilo na badala yake kuituhumu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ati inaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo. Ukweli ni kwamba moja ya sababu kuu za kukosekana amani na usalama nchini Yemen ni udhaifu wa serikali ya muda ya nchi hiyo wa kushindwa kudhamini usalama na kuzuia uingizwaji silaha na makundi yanayobeba silaha nchini humo. Katika hali kama hiyo badala ya serikali ya Yemen kufanya juhudi zaidi za kulinda usalama wa raia wake na wa raia wa kigeni walioko nchini humo inajaribu kukwepa jukumu lake hilo na kuyahusisha matatizo yake ya ndani na nje ya mipaka ya nchi hiyo… Read more »

Friday, November 21

Assad: Viwepo vita vya kimataifa dhidi ya magaidi

Assad: Viwepo vita vya kimataifa dhidi ya magaidiRais Bashar al-Assad wa Syria amesema kuwa, kuna udharura wa kuweko vita vya kimataifa dhidi ya magaidi. Rais Assad amesisitiza kwamba, kwa sasa eneo la Mashariki ya Kati linapitia kipindi nyeti mno lakini kile ambacho kitaainisha njia ya marhala hii ni kusimama kidete taifa la Syria. Ameongeza kuwa, mustakabali wa Mashariki ya Kati utaainishwa kwa kusimama kidete wananchi wa Syria katika kupambana na makundi ya kigaidi sambamba na himaya kwa taifa hilo ya nchi marafiki na Syria. Rais wa Syria amebainisha kwamba, ili ugaidi na makundi ya kigaidi vitokomezwe kuna haja ya kuweko vita vya kimataifa tena vyenye nia safi na ya dhati ya kupambana na ugaidi.
Rais Bashar al-Assad amesisitiza kwamba, taifa la Syria halitasalimu amri, bali litaendelea kupambana na makundi ya kigaidi katika nchi hiyo ambayo mbali na kuhatarisha usalama wa nchi yametenda jinai kubwa dhidi ya binadamu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Wakati huo huo ripoti kutoka Syria zinaonesha kuwa, jeshi la nchi hiyo limeendelea kupata mafanikio katika operesheni zake za kijeshi za kupambana na makundi ya kigaidi.
Read more »

Algeria yataka mahasimu wa Mali wakubaliane

Algeria yataka mahasimu wa Mali wakubalianeSerikali ya Algeria ambayo ni mpatanishi katika mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Mali na makundi ya waasi ya kaskazini mwa nchi hiyo imezitaka pande mbili hizo kutumia vyema fursa ya mazungumzo ya amani na kufikia makubaliano. Takwa hilo limetolewa na Ramtane Lamamra, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Algeria ambaye amesisitiza kwamba, pande hasimu za Mali zinapaswa kutumia vyema na kadiri ziwezavyo fursa ya mazungumzo ya amani. Amesema kuwa, mazungumzo ya amani ya Mali yanayoendelea katika mji mkuu wa Algeria Algiers yanapaswa kutumiwa vyema na pande hizo mbili hasimu na hivyo kutiliana saini makubaliano ya mwisho ya amani.
Duru ya nne ya mazungumzo ya amani ya Mali ilianza jana nchini Algeria ambapo duru mbalimbali za kisiasa zinazitaka serikali ya Bamako na makundi ya waasi kufanya juhudi ili kufikia makubaliano ya mwisho ya amani. Kutofikiwa mazungumzo kati ya pande mbili kumezitia wasi wasi nchi nyingi hasa zinazopakana na Mali ambazo zinahofia kupenya makundi ya waasi na kuingia katika nchi zao. Hivi karibuni Jeshi la Algeria liliimarisha usalama katika mpaka wake na Mali  ili kuzuia upenyaji na uingiliaji wa magaidi kutoka kwa jirani yake huyo.
Read more »

Mahmoud Abbas ataka kusitishwa jinai za Israel

Mahmoud Abbas ataka kusitishwa jinai za IsraelRais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amewaandikia barua shakhsia kadhaa wa kisiasa ulimwenguni akitaka kuweko uingiliaji kati wa haraka ili kukomeshwa hujuma na jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Quds inayokaliwa kwa mabavu.
Katika barua yake kwa Bani Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, John Kerry Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Sergey Lavrov Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia, Federica Mogherini Mkuu mpya wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya na Tony Blair Mjumbe wa Kamati ya Pande Nne ya Amani ya Mashariki ya Kati, Rais Mahmoud Abbas amewataka shakhsia hao kuulazimisha utawala wa Kizayuni wa Israel uhitimishe jinai zake dhidi ya wananchi wa Palestina. Aidha Mahmoud Abbas amewataka shakhsia hao kuiunga mkono azma ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kutambuliwa nchi ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967 mji mkuu wake ukiwa Baytul Muqaddas. Hayo yanajiri katika hali ambayo, katika siku za hivi karibuni utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na mashambulio yake dhidi ya Wapalestina na katika msikiti wa al-Aqswa huko Baytul Muqaddas.

Read more »

Wakimbizi wa Chad wanakabiliwa na hali mbaya

Wakimbizi wa Chad wanakabiliwa na hali mbayaShirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limeelezea wasi wasi wake mkubwa lilionao kuhusiana na hali mbaya wanayokabiliwa nayo wakimbizi wa Chad. Taarifa zaidi zinasema kuwa, baada ya kushadidi machafuko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, raia wengi wa Chad waliokuwa wakiishi nchini humo wamelazimika kuondoka nchini humo na kurejea 

nchini kwao. Aghlabu ya wakimbizi hao wamo katika kambi za wakimbizi zilizoko kusini magharibi mwa Chad. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu hali ya kibinadamu katika kambi hizo ni mbaya mno. Takribani raia elfu saba kati ya wakimbizi hao wana azma ya kurejea katika makazi yao huko mashariki mwa Chad. Ripoti ya 

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu inaeleza kuwa, licha ya kuweko ugawaji misaada kwa wakimbizi hao, lakini misaada hiyo haitoshi kukidhi mahitaji ya wakimbizi hao. Mbali na wakimbizi wa Kichadi waliorejea katika nchi yao, 


Chad kwa sasa inakabiliwa pia na wimbi la wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao wameikimbia nchi yao baada ya kushadidi machafuko na mapigano. Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba serikali ya Chad haina uwezo wa kifedha wa kudhamini mahitajio ya maelfu ya wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati walioko nchini humo.
Read more »

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com