Wananchi waliotimiza masharti ya kupiga kura nchini Nigeria leo wameelekea kwenye vituo vya kupigia kura kwa lengo la kumchagua rais, wabunge na maseneta wa maeneo yao. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Nigeria imetangaza kuwa, karibu watu milioni 68 na laki nane kutoka jumla ya watu milioni 173 wa nchi hiyo walijiandikisha kwenye daftari la kupiga kura nchini humo. Kwenye uchaguzi wa rais, kuna shakhsia 14 watakaochuana vikali kwenye uchaguzi huo ulioanza leo. Duru za habari zinasema, mchuano mkali utakuwa kati ya Rais Goodluck Jonathan kutoka chama tawala cha People's Democratic Party PDP na Jenerali mstaafu Muhammadu Buhari kutoka chama cha All Progressives Congress 'APC'. Rais Jonathan aliyeingia madarakani mwaka 2011, anahesabiwa kuwa rais wa kwanza kutoka kabila la Ijaw na pia ni kiongozi wa kwanza anayetoka eneo la kusini mwa Niger Delta. Buhari aliwahi kuiongoza Nigeria kuanzia mwaka 1983 hadi 1993 wakati nchi hiyo ilipokuwa ikitawaliwa na majenerali wa kijeshi. Buhari ameikosoa serikali ya Jonathan kwa kushindwa kulitokomeza kundi la kigaidi la Boko Haram pamoja na kuongezeka vitendo vya ufisadi wa kiserikali, umasikini na ukosefu wa ajira nchini humo. Taarifa zinasema kuwa, wasimamizi kutoka Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa wako nchini Nigeria kwa lengo la kusimamia zoezi hilo
IQRA FM RADIO
Saturday, March 28
Browse: Home
» Uchaguzi mkuu wafanyika leo nchini Nigeria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Andika Maoni
add
LEO KATIKA HISTORIA
TANGAZANASI
kwama Matangazo wasiliana nasi kupitia anuani zifuataz
Email:
iqrafmradio@gmail.cm
contact us:
0752925259
0762118805
infohttp:iqrafmradio.blogspot.com
uimara wa redio iqra upo mikononi mwako
>>Wote mnakalibishwa.....................................
Email:
iqrafmradio@gmail.cm
contact us:
0752925259
0762118805
infohttp:iqrafmradio.blogspot.com
uimara wa redio iqra upo mikononi mwako
>>Wote mnakalibishwa.....................................
ZILIZO SOMWA ZAIDI
-
Mwenyezi Mungu anasema: Niombeni nitakupeni. Zifuatazo hapa ni dua za baada ya nyakati mbalimbali za sala. Tunamuomba Mwenyezi Mung...
-
Mwenyezi Mungu anasema: Niombeni nitakupeni. Zifuatazo hapa chini ni dua 25 za Qur'ani Tukufu tulizozinukuu kutoka katika...
-
RATIBA YA VIPINDI KWA JUMA ZIMA RATIBA - JUMATATU MUDA KIPINDI MUHUSIKA 06:30-07:00 M...
-
Sura ya Al Furqan, aya ya 41-44 (Darsa ya 628) Wasikilizaji wapenzi wa Darsa ya Qur'ani, Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wa...
MITANDAO YA KIJAMII
TAFUTA HABARI ZILIZO SOMWA NYUMA
Powered by Blogger.
Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...
0 toamaon yako: