Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Saturday, March 28

Takwa la nchi za Amerika ya Latini la kuondolewa vitisho vya Marekani dhidi ya Venezuela

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Takwa la nchi za Amerika ya Latini la kuondolewa vitisho vya Marekani dhidi ya VenezuelaKufuatia kuwekwa vikwazo vipya dhidi ya shakhsia kadhaa wa Venezuela na halikadhalika vitisho vya kiusalama vya 
Rais Barack Obama dhidi ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini, raia na serikali kadhaa za eneo hilo zimekosoa vikali siasa za rais huyo wa Marekani. Jamii ya nchi za Amerika ya Latini na zile za Bahari ya Caribbean kwa pamoja, zimepinga hatua na amri ya Rais Obama aliyeitaja Venezuela kuwa ni tishio la kiusalama dhidi ya Washington. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ecuador Ricardo Patino ambaye nchi yake inashikilia uogozi wa Jumuiya ya nchi za Amerika ya Latini na visiwa vya Caribbean, ametangaza kuwa wanachama wote 33 wa jumuiya hiyo wanataka kuondolewa amri hiyo na badala yake kufanyike mazungumzo yatakayozingatia misingi ya kimataifa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ecuador ameongeza kuwa, mbali na wanachama wa jumuiya hiyo iliyotajwa, Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote kwa kifupi (NAM) siku ya Jumatano iliyopita, iliitaka pia Washington kubatilisha hukumu yake hiyo dhidi ya taifa la Venezuela. Kwa upande wake Rais Juan Evo Morales wa Bolivia ameelezea hatua ya Rais Barack Obama kuitaja Vinezuela kuwa tishio kwa nchi yake, kuwa ni kosa kubwa. Amesema kuwa hatua hiyo ni sawa na kuzitaja nchi zote za Amerika ya Latini kuwa tishio kwa maslahi ya Marekani na mfumo wake wa kibepari kutokana na nchi hizo kupinga kuporwa utajiri wao na Washington. Katika kikao cha mwisho cha nchi wanachama wa muungano wa ALBA kilichofanyika tarehe 18 mwezi Machi mwaka huu, washiriki walimtaka rais huyo wa Marekani kufutulia mbali amri hiyo iliyoitaja serikali ya Caracas kuwa tishio lisilo la kawaida kwa usalama wake. Ripoti hiyo ilieleza kuwa, Venezuela sio tishio kwa nchi yoyote na kinyume chake wananchi wake wameonyesha irada thabiti kwa ajili ya kuendeleza ushirikiano na mataifa mengine kieneo na kimataifa kwa ujumla. Muungano wa ALBA unaundwa na nchi za Amerika ya Latini ikiwemo Cuba, Venezuela, Bolivia, Ecuador, Nicaragua, Jamhuri ya Watu wa Dominican, Saint Vincent na Granadyn, St Lucia, Granada, Antigua na Barbara, St. Christopher na Saint Kitts na Nevis. Kabla ya hapo pia na katika kikao kilichofanyika mjini QuitoEcuador muungano huo ulizitaka nchi wanachama wa mataifa ya Amerika ya Kusini unaofahamika kwa jina la Union de Naciones Suramericanas (UNASUR) kufanya juhudi za kuhakikisha vikwazo walivyowekewa shakhsia kadhaa wa Vinezuela vinaondolewa. Itakumbukwa kuwa tarehe Ttisa mwezi huu wa Machi, Rais Barack Obama alitoa amri ambayo iliitaja Venezuela kuwa tishio kwa usalama wake, amri ambayo iliambatana na kuyaweka katika orodha ya vikwazo, majina kadhaa ya viongozi wa nchi hiyo. Katika kujibu hatua hiyo, Caracas iliwaita maafisa wa ubalozi wake mjini Washington, huku Baraza la Kitaifa la Venezuela likimpa rais wa nchi hiyo uwezo maalumu kwa ajili ya kukabiliana na hujuma za ubeberu wa Marekani. Kufuatia amri hiyo wanaharakati wa asasi za kiraia nchini humo walianzisha kampeni iliyopewa jina la 'Venezuela sio Tishio' kampeni ambayo kwa muda wa siku nne tu zilizopita tayari imetiwa saini na watu milioni moja, katika kupinga siasa za rais wa Marekani dhidi ya taifa lao

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com