
Kiongozi wa chama cha upinzani cha FNL nchini Burundi ametahadharisha kuwa, taifa hilo linaweza kutumbukia kwenye ghasia na machafuko iwapo serikali haitowasikiza wadau katika siasa za nchi hiyo. Akizungumza kwenye mahojiano maalum na Idhaa hii, Agathon Rwasa amesema kuwa, mchakato wa kuandaa daftari la wapiga kura kupitia uandikishaji wa raia ni zoezi lililovurugika na ameitaka serikali kusitisha zoezi hilo mara moja. Rwasa amesema uchaguzi mkuu ujao unaweza kuwa nukta ya kuwaunganisha Warundi pamoja au kuwagawanya kwa kutegemea jinsi maandalizi yatakavyofanywa. Mkuu wa FNL amesema mustakabali wa siasa nchini Burundi unakumbwa na hatihati na kusisitiza kuwa serikali itabeba dhima iwapo machafuko yatatokea kutokana na upuuzaji wake wa hali ya mambo kwa hivi sasa.
Tayari muungano wa upinzani wa ADC-Ikibiri umejiondoa kwenye zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kufuatia dosari zilizojitokeza na kutishia kususia uchaguzi mkuu wa rais mwakani endapo serikali haitositisha zoezi hilo
0 toamaon yako: