
Katika barua yake kwa Bani Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, John Kerry Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Sergey Lavrov Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia, Federica Mogherini Mkuu mpya wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya na Tony Blair Mjumbe wa Kamati ya Pande Nne ya Amani ya Mashariki ya Kati, Rais Mahmoud Abbas amewataka shakhsia hao kuulazimisha utawala wa Kizayuni wa Israel uhitimishe jinai zake dhidi ya wananchi wa Palestina. Aidha Mahmoud Abbas amewataka shakhsia hao kuiunga mkono azma ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kutambuliwa nchi ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967 mji mkuu wake ukiwa Baytul Muqaddas. Hayo yanajiri katika hali ambayo, katika siku za hivi karibuni utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na mashambulio yake dhidi ya Wapalestina na katika msikiti wa al-Aqswa huko Baytul Muqaddas.
0 toamaon yako: