Sura ya Al Furqan, aya ya 41-44 (Darsa ya 628)
Wasikilizaji wapenzi wa Darsa ya
Qur'ani, Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh. Bismillahir
Rahmanir Rahim. Hamdu na sifa zote njema zinamstahikia Allah SW, na
rehma na amani zimshukie Mtume wake Mtukufu na Aali zake watoharifu. Kwa
taufiki yake Mola Karima aliyetupa uhai na uzima tumekutana tena katika
mfululizo mwengine wa Darsa ya Qur'ani. Hii ni darsa ya 628 na sura
tunayoizungumzia hivi sasa ni ya 25 ya Al Furqan. Tunaianza darsa yetu
hii kwa aya ya 41 na 42 ambazo zinasema:
وَإِذَا رَأَوْكَ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلاَّ هُزُوًا أَهَذَا الَّذِي بَعَثَ اللَّهُ رَسُولا
Na wanapokuona hawakufanyii ila kejeli tu, (kwa kusema): Ati huyu ndiye Mwenyezi Mungu aliyemtuma kuwa Mtume?
إِن كَادَ لَيُضِلُّنَا عَنْ آلِهَتِنَا لَوْلا أَن صَبَرْنَا عَلَيْهَا وَسَوْفَ يَعْلَمُونَ حِينَ يَرَوْنَ الْعَذَابَ مَنْ أَضَلُّ سَبِيلا
Kwa hakika alikuwa karibu kutupoteza tuiache miungu yetu, kama tusingelishikamana nayo kwa kuvumilia. Na karibu watajua watakapoiona adhabu, ni nani aliyepotea njia.
Aya tulizozitolea ufafanuzi kwenye darsa
iliyopita zilizungumzia muamala wa washirikina kwa Bwana Mtume Muhammad
SAW. Aya hizi tulizosoma zinaendelea kuzungumzia maudhui hiyo kwa
kusema: wakati watu hao walipokuwa wakikutana na Bwana Mtume, badala ya
kuyasikiliza maneno yake ya haki na ya mantiki, na kuyataamali na
kuyatafakari maneno hayo, kitu pekee walichokuwa wakifanya ilikuwa ni
kusema kwa kejeli na istihzai kwamba Mwenyezi Mungu ndo amemfanya mtu
huyu awe Mtume wetu? Mtu ambaye hana mali wala cheo, na tangu utotoni
mwake amekulia katika uyatima? Ikiwa sisi hatutoshikamana na masanamu
yetu atatupotosha mara moja na kutuweka mbali na dini ya wazee wetu
waliotutangulia.
Mwenyezi Mungu SW akayajibu maneno hayo yasiyo na mantiki wala nadhari ya waabudu masanamu kwa kusema: mtakapoziona ishara za adhabu, wakati huo ndipo mtapofahamu kama ni Mtume au nyinyi ndio mliokuwa katika upotofu! Hivi kweli mnamwita kuwa ni mtu aliyepotoka, Mtume ambaye ameishi pamoja nanyi kwa miaka na miaka, hali ya kuwa hamjawahi kuona chochote kwake yeye ghairi ya ukweli na uaminifu? Kisha nyinyi wenyewe ambao hamna hoja yoyote ya kukufanyeni muabudu masanamu ghairi ya kusema mnafuata dini ya waliokutangulieni, ndio mnajiona ni watu mlioongoka?
Baadhi ya mafunzo tunayopata kutokana na aya hizi ni kwamba wale ambao si wenye hoja na mantiki huwa hawana njia nyengine ya kufanya isipokuwa kuwakejeli na kutaka kuwadunisha waja wema wa Allah, na hii ndio mbinu ya kudumu ya makafiri. Funzo jengine tunalopata kutokana na aya hizi ni kuwa mtu mkaidi na mwenye ghururi hawi tayari kuikubali haki. Na ndiyo maana chanzo cha ukafiri na ukanushaji wa watu wengi ni ukaidi wao na si udhaifu wa hoja zinazotolewa na wafuasi wa tauhidi na Mola mmoja wa haki. Kadhalika tunajielimisha kutokana na aya hizi kwamba kusimama imara na kudumu katika njia ya haki ndilo jambo lenye thamani, si kuwa mshupavu katika njia ya batili ambako ni kuwa mkaidi na kufanya taasubu zisizo na msingi.
Ifuatayo sasa ni aya ya 43 ambayo inasema:

أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَهَهُ هَوَاهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلا
Je! Umemwona aliyeyafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake?
Aya hii inamhutubu Bwana Mtume kuwa
washirikina na makafiri hawayakubali maneno yako kwa sababu hayaafikiani
na hawaa, utashi na matamanio yao ya nafsi. Wao wanataka wafanye kila
kile zinachotaka na kutamani nafsi zao wala hawajali uzuri na ubaya wa
kitu hicho. Lililo muhimu kwao wao ni kukidhi matamanio ya kighariza, na
si hata kile kinachofahamika na kukubaliwa na akili zao. Kwa hiyo wewe
Mtume usiwe na tamaa kwamba watu walioamua kukinzana na akili, fitra na
maumbile yao, watakubali kusikiliza na kuyakubali maneno yako na
kuufuata uongofu unaowafikishia. Miongoni mwa mafunzo tunayopata
kutokana na aya hii ni kwamba chanzo cha ukafiri na shirki ni kuabudu
hawaa na matamanio ya nafsi na si mantiki na hoja za kiakili. Funzo
jengine tunalopata kutokana na aya hii ni kuwa kiu ya kumjua Mungu imo
ndani ya fitra na maumbile ya kila mtu, lakini baadhi ya watu hukosea
katika kufikia kwenye misdaqi na kielelezo chake halisi ambacho ni Allah
SW, Mola pekee wa ulimwengu. Aidha aya hii inatuonyesha kuwa imani huwa
na thamani inapotokana na hiyari; na si kwa kulazimishwa na kutezwa
nguvu. Kwa hivyo Mitume si mawakili na wasimamizi wa watu; na kwa hivyo
hawawezi kutumia mbinu ya ulazimishiaji na utezaji nguvu kwa ajili ya
kuwaelekeza watu hao kwenye njia ya uongofu.
Darsa yetu ya leo inahatimishwa na aya ya 44 ambayo inasema:
Darsa yetu ya leo inahatimishwa na aya ya 44 ambayo inasema:
أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ إِنْ هُمْ إِلاَّ كَالأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلا
Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanatumia akili? Hao hawakuwa ila ni kama wanyama hoa tu; bali wao wamepotea zaidi njia.
Aya hii inamliwaza Bwana Mtume na
waumini kwa kuwaambia kwamba msiudhike kwa maneno na mwenendo muovu wa
washirikina na wala msiwasikitie bure watu hao kwa sababu wao
hawazirejei akili zao ili waweze kuifahamu haki na wala hawana masikio
ya kusikia, kuwafanya wawe tayari kusikiliza maneno ya haki na
kuyakubali. Katika hali hiyo, wao ni mithili ya wanyama hoa wa miguu
minne ambao si maneno ya wamiliki wao ambayo wanayafahamu, wala si hisi
ambazo wanazo za kuwawezesha kuchukua uamuzi na kufanya jambo kutokana
na hisi hizo. Ukweli ni kwamba kama tutalizingatia hilo kwa makini, wao
ni watu waliopotea zaidi kuliko hata wanyama. Kwa sababu wanyama
wanaishi namna hivyo kwa kutokuwa na nyenzo za hisi na ufahamu, na wala
hawana uwezo wa kujitutumua zaidi ya vile walivyo. Lakini kinyume chake,
wanadamu wamejaaliwa fitra na akili, na suhula na nyenzo za kuukuza
uwezo wao wa kuelewa na kufahamu mambo lakini baadhi yao hawazitumii
neema hizo. Katika kuamiliana na makafiri na wapinzani wa haki, Qur'ani
tukufu inaonyesha kuwa na insafu kwa kueleza kwamba akthari ya watu hao
wako hivyo lakini si wote, ili kupambanua hukumu ya wale wanaopotoka kwa
kuhadaika na kudanganyika na wengineo wasiokuwa hao. Baadhi ya mafunzo
tunayopata kutokana na aya hii ni kwamba wanyama hawana akili ya
kufahamu na kupambanua baina ya jema na baya au kati ya haki na batili;
lakini watu wanaopotoka, licha ya kujaaliwa kuwa na akili ima
hawashughuliki kuitafuta na kuifahamu haki na batili au wanaijua haki ni
ipi lakini wanaikengeuka na kuipa mgongo. Funzo jengine tunalopata
kutokana na aya hii ni kuwa njia ya kuufikia uongofu ni kusikiliza wito
wa haki na kuutafakari. Wahyi ni hoja na mwongozo wa nje ambao kama
utapenya ndani ya sikio la mtu utakamilisha nafasi ya hoja ya ndani
ambayo ni akili aliyopewa mtu. Kadhalika aya hii inatuelimisha kwamba
mtu anayeukubali uongofu wa Allah huwa na heshima ya utu na ubinadamu,
na mtu anayeamua kuipinga haki huwa duni mbele ya Mola kuliko hata
mnyama. Kwa haya machache wapenzi wasikilizaji tunaifunga darsa yetu
hii. Tunamwomba Mola atuonyeshe haki na atupe taufiki ya kuifuata, na
atuonyeshe batili na atuwezeshe kuiepuka.
Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh...
0 toamaon yako: