
Chama cha Upinzani cha Zimbabwe cha
Movement for Democratic Change (MDC) kimetaka kuwafukuza bungeni
wawakilishi 18 ambao si wabunge tena wa chama hicho. Wabunge hao ni
pamoja na Tendai Biti katibu mkuu wa zamani wa MDC na waziri wa fedha
ambaye amefukuzwa chamani na mkuu wa chama hicho Morgan Tsvangirai.
Chama hicho kimeliambia bunge kuwa wawakilishi hao 18 ambao
walichaguliwa kama wabunge wa MDC hawakiwakilishi tena chama hicho. Biti
na wenzake walikuwa wakijaribu kumuuzulu Tsvangirai chamani kwa
kushindwa kumuangusha Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe katika uchaguzi wa
rais.
Mpasuko huo umekidhoofisha chama hicho
cha upinzani kinachompinga Mugabe ambaye yupo madarakani tangu nchi hiyo
ilipojipatia uhuru mwaka 1980.
Wiki iliyopita Tsvangirai alichaguliwa tena bila kupingwa kukiongoza
chama cha MDC.
0 toamaon yako: