
Makundi ya kutetea haki za binadamu
yamearifu kuwa, Waislamu wa jamii ya Rohingya wamelazimishwa kuondoka
nchini Myanmar katika wiki 3 ziliopita kutokana mpango mpya wa serikali
uliozusha mjadala. Kwa mujibu wa mpango huo unaoitwa Rakhine Action
Plan, zaidi ya Waislamu milioni moja wa kabila la Rohingya watafukuzwa
nchini humo iwapo watashindwa kuthibitisha kwamba familia zao zimeishi
nchini Myanmar kwa zaidi ya miaka 60 iliyopita. Waislamu hao wa Mynamar
pia wanaweza kufungwa jela kwa muda usiojulikana kwa mujibu wa mpango
huo wa kibaguzi, ambao unawataka wakubali kupangwa tena kimakabila na
kuandikishwa kuwa ni Wabengali au kufungwa jela.
Makundi ya kutetea haki za binadamu
yameitaka jamii ya kimataifa iishinikize serikali ya Myanmar kufuta
mpango huo na kuutaja kuwa hauna maana yoyote zaidi ya kuthibitisha
kuendelea ubaguzi wa rangi.
Jamii ya Waislamu wa Rohingya wamekuwa
wakikabiliwa na ubaguzi, manyanyaso na kupuuzwa tangu nchi hiyo
ilipopata uhuru mwaka 1948. Katika miaka miwli iliyopita Waislamu wengi
wa Myanmar wameuawa huku zaidi ya laki na nusu wakikimbia makazi yao
kutokana na mashambulizi yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali.
0 toamaon yako: