Chama cha upinzani cha al
Wefaq nchini Bahrain kimemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki-moon afuatilie jinai za utawala wa al Khalifa. Sheikh Ali Salman,
Katibu Mkuu wa chama hicho amesema, kukamatwa tena Nabil al Rajab na
viongozi wengine wa upinzani wa Bahrain na kupigwa marufuku shughuli za
chama cha la Wefaq ni sawa na kushindwa uchaguzi wa Bunge la nchi hiyo
hata kabla ya kufanyika. Katika barua yake kwa Ban Ki-moon ameeleza
kuwa, vikosi vya utawala wa Bahrain vinawatesa hadi kufa wapinzani huku
kuvunjwa haki za binadamu na kukandamizwa watu likiwa ni jambo la
kawaida nchini humo. Ameongeza kwamba, utawala wa Aal Khalifa mbali na
kubomoa misikiti, umeshadidisha sera za ubaguzi wa kidini na kutumia
gesi za sumu dhidi ya waombolezaji wa Imam Hussein (A.S).
Katibu Mkuu wa chama cha
upinzani cha la Wefaq sambamba na kusisitiza kuendelea harakati za
kimapinduzi za wananchi amemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
ashughulikie jinai zinazofanywa na utawala wa Manama.
0 toamaon yako: