IQRA FM RADIO
Friday, November 7
Browse: Home
» Habari za kitaifa na kimataifa
» Radiamali ya Wapalestina kwa hujuma za Wazayuni dhidi ya Masjid al-Aqswa
Radiamali ya Wapalestina kwa hujuma za Wazayuni dhidi ya Masjid al-Aqswa
Posted by mkachu |  Tagged as: Habari za kitaifa na kimataifa
Kushtadi uvamizi na hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Masjid al-Aqswa ambazo katika siku za hivi karibuni zimechukua mkondo hatari zaidi kuliko huko nyuma, kumekabiliwa na radiamali za makundi ya Wapalestina katika uga wa kimuqawama na kisiasa. Katika mazingira kama haya, sanjari na malalamiko ya wananchi dhidi ya utawala wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu, makundi ya mapambano ya Palestina yamebainisha kwamba, muqawama na mapambano ndilo chaguo pekee la kuuhami na kuulinda msikiti wa al-Aqswa na uvamizi mtawalia wa utawala haramu wa Israel. Katika uwanja huo, siku ya Jumatano Khalid Mash’al, Mkuu wa Ofisi ya Kis iasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS alisisitiza kwamba, machaguo na mikakati yote ya kuuhami msikiti wa al-Aqswa inazingatiwa, lakini muqawama ndilo chaguo linaloongoza machaguo yote. Katika mazingira kama haya, balozi na mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa, amelitaka Baraza la Usalama la Umoja huo liushinikize utawala vamizi wa Israel ukomeshe vitendo vyake vya utumiaji mabavu huko Baytul Maqaddas na katika Masjid al-Aqswa, kibla cha kwanza cha Waislamu. Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano baada ya kikao cha faragha cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Riyadh Mansour alisema, wanachama 15 wa baraza hilo wanapaswa kuchukua msimamo wa kuitaka Israel ikomeshe harakati zozote zile za siasa za kichochezi na vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Wapalestina. Mwakilishi huyo wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, hatua ya Wazayuni wenye kufurutu ada wanaoingia na viatu katika msikiti wa al-Aqswa ni ya kichochezi na imekuwa ikipelekea kutokea rangaito, vurugu na mapigano. Ombi la Wapalestina kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuitaka asasi hiyo iingilie kati kuhusiana na uvamizi na vitendo vya kuuvunjia heshima msikiti wa al-Aqswa vinavyofanywa na Wazayuni linatolewa katika hali ambayo, vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu vinavyofanywa na utawala huo vimeshadidi mno katika eneo hilo takatifu, kongwe na la kihistoria, hali ambayo imepelekea mgogoro wa Palestina kuingia katika marhala hatari zaidi. Hapana shaka kuwa, hujuma na hatua za utawala vamizi wa Israel zimehatarisha amani na usalama wa kimataifa. Hii ni katika hali ambayo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lina jukumu la kushughulikia masuala kama haya limeamua kukaa kimya na kutochukua hatua yoyote ile ya maana. Hatua za utawala ghasibu wa Israel katika msikiti wa al-Aqswa mbali na kukabiliwa na malalamiko ya wananchi zimeandamwa pia na upinzani wa Waislamu katika pembe mbalimbali ulimwenguni. Katika anga kama hii, fikra za waliowengi ulimwenguni nazo zinafuatilia kwa hisia na unyeti maalumu duru mpya ya hujuma za Wazayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa na zinataka Baraza la Usalama lichukue hatua za maana dhidi ya utawala huo. Katika mazingira kama haya, Wapalestina wanataka kuchunguzwa haraka vitendo vya utawala bandia wa Israel katika Masjid al-Aqswa na kuchukuliwa hatua za maana na madhubuti za kusitisha hujuma za utawala huo ghasibu. Hii ni katika hali ambayo, ripoti zinaonesha kuwa, Marekani inapinga vikali kuzungumziwa suala la uvamizi wa Israel katika Masjid al-Aqswa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Jambo lililo wazi ni kuwa, katika hali ambayo utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea na hatua na hujuma zake huko Quds katika anga ya kimya cha jumuiya za kimataifa, hatua bora, ya maana na yenye taathira ni kuendelezwa muqawama sambamba na kushadidishwa mapambano ya wananchi dhidi ya utawala huo ghasibu; na huu ndio ukweli ambao umeashiriwa na Khalid Mash’al, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Matukio ya Palestina yanaonesha juu ya kuingia Wapalestina katika marhala mpya ya muqawama na mapambano dhidi ya utawala vamizi wa Israel. Katika mazingira kama haya, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaamini kwamba, uvamizi na hujuma za Israel dhidi ya msikiti wa al-Aqswa ni kitendo cha kuwasha moto ambao utawala huo ghasibu utatumbukia wenyewe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Andika Maoni
add
LEO KATIKA HISTORIA
TANGAZANASI
kwama Matangazo wasiliana nasi kupitia anuani zifuataz
Email:
iqrafmradio@gmail.cm
contact us:
0752925259
0762118805
infohttp:iqrafmradio.blogspot.com
uimara wa redio iqra upo mikononi mwako
>>Wote mnakalibishwa.....................................
Email:
iqrafmradio@gmail.cm
contact us:
0752925259
0762118805
infohttp:iqrafmradio.blogspot.com
uimara wa redio iqra upo mikononi mwako
>>Wote mnakalibishwa.....................................
ZILIZO SOMWA ZAIDI
-
Mwenyezi Mungu anasema: Niombeni nitakupeni. Zifuatazo hapa ni dua za baada ya nyakati mbalimbali za sala. Tunamuomba Mwenyezi Mung...
-
Mwenyezi Mungu anasema: Niombeni nitakupeni. Zifuatazo hapa chini ni dua 25 za Qur'ani Tukufu tulizozinukuu kutoka katika...
-
RATIBA YA VIPINDI KWA JUMA ZIMA RATIBA - JUMATATU MUDA KIPINDI MUHUSIKA 06:30-07:00 M...
-
Sura ya Al Furqan, aya ya 41-44 (Darsa ya 628) Wasikilizaji wapenzi wa Darsa ya Qur'ani, Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wa...
MITANDAO YA KIJAMII
TAFUTA HABARI ZILIZO SOMWA NYUMA
Powered by Blogger.
Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...
0 toamaon yako: