Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Friday, November 21

Rais wa Somalia: al-Shabab watasambaratishwa

Rais wa Somalia: al-Shabab watasambaratishwaRais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia ametangaza kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa 2014, kundi la wanamgambo wa al-Shabab litalazimika kuondoka katika maeneo na miji linayoidhibiti katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. Mtandano wa Habari wa al-Yaum Sab’i umemnukuu Rais Hassan Sheikh Mohamoud akisema kwamba, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba ujao jeshi la Somalia na vikosi vya kusimama amani vya Umoja wa Afrika AMISOM vitakuwa vimefanikiwa kuwafurusha wanamgambo wa al-Shabab na kuwalazimisha kuondoka katika maeneo wanayoyadhibiti.
 Rais wa Somalia ambaye kwa sasa yuko nchini Denmark alikokwenda kushiriki mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia amesema kuwa, wanamgambo wa al-Shabab watalazimika kurejea nyuma na kwenda katika vijiji vya mbali na hivyo mashambulio yao baada ya hapo yatakuwa ya hapa na pale. Rais Mohamoud amebainisha kwamba, serikali ya Somalia inafanya kila iwezalo ili kuhakikisha kwamba, hadi kufikia miezi mitatu ya awali ya mwaka ujao wa 2015 kusiweko  eneo lolote nchini humo ambalo linadhibitiwa na wanamgambo wa al-Shabab.
Read more »

Friday, November 7

Ban atakiwa kufuatilia jinai za utawala wa Bahrain

Ban atakiwa kufuatilia jinai za utawala wa BahrainChama cha upinzani cha al Wefaq nchini Bahrain kimemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon afuatilie jinai za utawala wa al Khalifa.  Sheikh Ali Salman, Katibu Mkuu wa chama hicho amesema, kukamatwa tena Nabil al Rajab na viongozi wengine wa upinzani wa Bahrain na kupigwa marufuku shughuli za chama cha la Wefaq ni sawa na kushindwa uchaguzi wa Bunge la nchi hiyo hata kabla ya kufanyika. Katika barua yake kwa Ban Ki-moon ameeleza kuwa, vikosi vya utawala wa Bahrain vinawatesa hadi kufa wapinzani huku kuvunjwa haki za binadamu na kukandamizwa watu likiwa ni jambo la kawaida nchini humo. Ameongeza kwamba, utawala wa Aal Khalifa mbali na kubomoa misikiti, umeshadidisha sera za ubaguzi wa kidini na kutumia gesi za sumu dhidi ya waombolezaji wa Imam Hussein (A.S).
Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha la Wefaq sambamba na kusisitiza kuendelea harakati za kimapinduzi za wananchi amemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ashughulikie jinai zinazofanywa na utawala wa Manama.
Read more »

Radiamali ya Wapalestina kwa hujuma za Wazayuni dhidi ya Masjid al-Aqswa

Radiamali ya Wapalestina kwa hujuma za Wazayuni dhidi ya Masjid al-Aqswa jumaa, 07 Novemba 2014 09:23

Kushtadi uvamizi na hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Masjid al-Aqswa ambazo katika siku za hivi karibuni zimechukua mkondo hatari zaidi kuliko huko nyuma, kumekabiliwa na radiamali za makundi ya Wapalestina katika uga wa kimuqawama na kisiasa. Katika mazingira kama haya, sanjari na malalamiko ya wananchi dhidi ya utawala wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu, makundi ya mapambano ya Palestina yamebainisha kwamba, muqawama na mapambano ndilo chaguo pekee la kuuhami na kuulinda msikiti wa al-Aqswa na uvamizi mtawalia wa utawala haramu wa Israel. Katika uwanja huo, siku ya Jumatano Khalid Mash’al, Mkuu wa Ofisi ya Kis iasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS alisisitiza kwamba, machaguo na mikakati yote ya kuuhami msikiti wa al-Aqswa inazingatiwa, lakini muqawama ndilo chaguo linaloongoza machaguo yote. Katika mazingira kama haya, balozi na mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa, amelitaka Baraza la Usalama la Umoja huo liushinikize utawala vamizi wa Israel ukomeshe vitendo vyake vya utumiaji mabavu huko Baytul Maqaddas na katika Masjid al-Aqswa, kibla cha kwanza cha Waislamu. Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano baada ya kikao cha faragha cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Riyadh Mansour alisema, wanachama 15 wa baraza hilo wanapaswa kuchukua msimamo wa kuitaka Israel ikomeshe harakati zozote zile za siasa za kichochezi na vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Wapalestina. Mwakilishi huyo wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, hatua ya Wazayuni wenye kufurutu ada wanaoingia na viatu katika msikiti wa al-Aqswa ni ya kichochezi na imekuwa ikipelekea kutokea rangaito, vurugu na mapigano. Ombi la Wapalestina kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuitaka asasi hiyo iingilie kati kuhusiana na uvamizi na vitendo vya kuuvunjia heshima msikiti wa al-Aqswa vinavyofanywa na Wazayuni linatolewa katika hali ambayo, vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu vinavyofanywa na utawala huo vimeshadidi mno katika eneo hilo takatifu, kongwe na la kihistoria, hali ambayo imepelekea mgogoro wa Palestina kuingia katika marhala hatari zaidi. Hapana shaka kuwa, hujuma na hatua za utawala vamizi wa Israel zimehatarisha amani na usalama wa kimataifa. Hii ni katika hali ambayo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lina jukumu la kushughulikia masuala kama haya limeamua kukaa kimya na kutochukua hatua yoyote ile ya maana. Hatua za utawala ghasibu wa Israel katika msikiti wa al-Aqswa mbali na kukabiliwa na malalamiko ya wananchi zimeandamwa pia na upinzani wa Waislamu katika pembe mbalimbali ulimwenguni. Katika anga kama hii, fikra za waliowengi ulimwenguni nazo zinafuatilia kwa hisia na unyeti maalumu duru mpya ya hujuma za Wazayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa na zinataka Baraza la Usalama lichukue hatua za maana dhidi ya utawala huo. Katika mazingira kama haya, Wapalestina wanataka kuchunguzwa haraka vitendo vya utawala bandia wa Israel katika Masjid al-Aqswa na kuchukuliwa hatua za maana na madhubuti za kusitisha hujuma za utawala huo ghasibu. Hii ni katika hali ambayo, ripoti zinaonesha kuwa, Marekani inapinga vikali kuzungumziwa suala la uvamizi wa Israel katika Masjid al-Aqswa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Jambo lililo wazi ni kuwa, katika hali ambayo utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea na hatua na hujuma zake huko Quds katika anga ya kimya cha jumuiya za kimataifa, hatua bora, ya maana na yenye taathira ni kuendelezwa muqawama sambamba na kushadidishwa mapambano ya wananchi dhidi ya utawala huo ghasibu; na huu ndio ukweli ambao umeashiriwa na Khalid Mash’al, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Matukio ya Palestina yanaonesha juu ya kuingia Wapalestina katika marhala mpya ya muqawama na mapambano dhidi ya utawala vamizi wa Israel. Katika mazingira kama haya, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaamini kwamba, uvamizi na hujuma za Israel dhidi ya msikiti wa al-Aqswa ni kitendo cha kuwasha moto ambao utawala huo ghasibu utatumbukia wenyewe
Read more »

Ijumaa, 07 Novemba 2014 09:23 Ijumaa, Novemba 7, 2014


Ijumaa, Novemba 7, 2014Leo ni Ijumaa tarehe 13 Mfunguo Nne Muharram 1436 Hijria sawa na tarehe 7 novemba 2014.
Siku kama ya leo miaka 58 iliyopita vita vya mfereji wa Suez vilimalizika baada ya uingiliaji kati wa Umoja wa Mataifa. Vita hivyo vilianza baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia jangwa la Sinai na kufuatia mashambulizi ya askari wa miavuli wa Uingereza na Ufaransa katika eneo la mfereji huo. Serikali hizo tatu zilizotajwa zilianzisha vita hivyo kufuatia hatua ya rais wa wakati huo wa Misri, Jamal Abdulnassir, kuutaifisha mfereji huo.
Miaka 147 iliyopita katika siku kama ya leo Madam Escudo Doska ambaye baadaye alikuwa maarufu kwa jina la Marie Curie alizaliwa huko Warsaw mji mkuu wa Poland. Baba yake alikuwa profesa wa fizikia na baadaye Madam Curie pia alielekea Paris, Ufaransa kwa ajili ya kuendeleza masomo yake katika taaluma hiyo hiyo ya baba yake. Madam Curie alifunga ndoa na Pierre Curie mwanafikizikia wa Ufaransa wakati alipokuwa masomoni katika Chuo Kikuu cha Sorbonne. Hatimaye mwanamama huyo alifanikiwa kuvumbua mada ya radium baada ya utafiti miaka mingi. Ni vyema kuashiria hapa kuwa Madam Curie alitunukiwa tuzo ya Nobel mara mbili katika taaluma za fizikia na kemia na aliaga dunia mwaka 1934.
Na siku kama ya leo miaka 36 iliyopita wananchi kote nchini Iran walifanya maandamano makubwa wakipinga kuja madarakani serikali ya kijeshi ya Jenerali Azhari aliyekuwa kibaraka wa utawala fasidi wa Kipahlavi. Katika maandamano hayo wananchi Waislamu wa Iran walitangaza azimio wakisema kuwa mabadiliko ya kimaonyesho na kubadilisha nafasi za vibaraka wa Marekani hakuwezi kuzuia mapambano yao kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiislamu. Siku hiyo pia Kiongozi wa harakati za Mapinduzi hayati Imam Khomeini alitoa ujumbe kwa mnasaba wa mauaji yaliyofanywa na utawala wa Shah dhidi ya wanafunzi wa vyuo vikuu akiwaambia wananchi kwamba: “Ninyi taifa shujaa, mumethibitisha kwamba vifaru, mitutu ya bunduki na mikuki imeota kutu na kwamba haiwezekani kukabiliana na irada ya chuma ya wananchi.”  
Read more »

Upinzani Zimbabwe wataka wabunge 18 wafukuzwe

Upinzani Zimbabwe wataka wabunge 18 wafukuzweChama cha Upinzani cha Zimbabwe cha Movement for Democratic Change (MDC) kimetaka kuwafukuza bungeni wawakilishi 18 ambao si wabunge tena wa chama hicho. Wabunge hao ni pamoja na Tendai Biti katibu mkuu wa zamani wa MDC na waziri wa fedha ambaye amefukuzwa  chamani na mkuu wa chama hicho Morgan Tsvangirai. Chama hicho kimeliambia bunge kuwa wawakilishi hao 18 ambao walichaguliwa kama wabunge wa MDC hawakiwakilishi tena chama hicho. Biti na wenzake walikuwa wakijaribu kumuuzulu Tsvangirai chamani kwa kushindwa kumuangusha Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe katika uchaguzi wa rais.
Mpasuko huo umekidhoofisha chama hicho cha upinzani kinachompinga Mugabe ambaye yupo madarakani tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru mwaka 1980.
 Wiki iliyopita Tsvangirai alichaguliwa tena bila kupingwa kukiongoza chama cha MDC.
Read more »

Waislamu 14,000 walazimishwa kuondoka Myanmar

Waislamu 14,000 walazimishwa kuondoka MyanmarMakundi ya kutetea haki za binadamu yamearifu kuwa, Waislamu wa jamii ya Rohingya wamelazimishwa kuondoka nchini Myanmar katika wiki 3 ziliopita kutokana mpango mpya wa serikali uliozusha mjadala. Kwa mujibu wa mpango huo unaoitwa Rakhine Action Plan, zaidi ya Waislamu milioni moja wa kabila la Rohingya watafukuzwa nchini humo iwapo watashindwa kuthibitisha kwamba familia zao zimeishi nchini Myanmar kwa zaidi ya miaka 60 iliyopita. Waislamu hao wa Mynamar pia wanaweza kufungwa jela kwa muda usiojulikana kwa mujibu wa mpango huo wa kibaguzi, ambao unawataka wakubali kupangwa tena kimakabila na kuandikishwa kuwa ni Wabengali au kufungwa jela.
 Makundi ya kutetea haki za binadamu yameitaka jamii ya kimataifa iishinikize serikali ya Myanmar kufuta mpango huo na kuutaja kuwa hauna maana yoyote zaidi ya kuthibitisha kuendelea ubaguzi wa rangi.
 Jamii ya Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakikabiliwa na ubaguzi, manyanyaso na kupuuzwa tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1948. Katika miaka miwli iliyopita Waislamu wengi wa Myanmar wameuawa huku zaidi ya laki na nusu wakikimbia makazi yao kutokana na mashambulizi yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali.
Read more »

Kesi za Ebola zaongezeka nchini Sierra Leone

Kesi za Ebola zaongezeka nchini Sierra LeoneUmoja wa Mataifa umetangaza kuwa kesi za maambukizi ya ugonjwa wa Ebola zimeongezeka nchini Sierra Leone huku nchi hiyo ikikabiliwa na tatizo la ukosefu wa vituo vya matibabu. Mpango wa Dharura wa Kukabiliana na Ebola wa Umoja wa Mataifa (UNMEER) umesema wiki hii kuwa, mfumuko wa ugonjwa wa Ebola umesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,060 nchini Sierra Leone huku maeneo yaliyoathiriwa zaidi yakiwa ya magharibi mwa mji mkuu Freetown.  Mpango huo aidha umesema, ukosefu wa vitanda katika vituo vya kutibu Ebola umesababisha familia kuangalia zenyewe wagonjwa majumbani, ambako waangalizi huwa hawana uwezo wa kutosha wa kujilinda wasiambukizwe virusi vya ugonjwa huo, na kwa sababu hiyo maambukizo yameongezeka.
Jumatano Shirika la Afya Duniani (WHO) liliripoti kuwa, idadi ya kesi za maambukizo ya Ebola zinaongezaka nchini Sierra Leone, ingawa ugonjwa huo umepungua katika nchi ya Liberia huku nchini Guinea maambukizo yakiwa ya wastani.
Read more »

NAM yalaani kushambuliwa Wapalestina na Israel

NAM yalaani kushambuliwa Wapalestina na IsraelJumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) imelaani mashambulio ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina. Ghulam-Hussein Dehqani, mwakilishi wa Iran katika Jumuiya hiyo amesema kwamba, mashambulio ya kila siku, kubomolewa nyumba na miundombinu katika Ukanda wa Gaza na kushambuliwa vituo vya umeme, hospitali na vyanzo vya maji na pia maeneo ya Umoja wa Mataifa sio tu ni janga kubwa bali ni ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu. Ameongeza kuwa, Israel pia inakiuka haki za raia wa Palestina na hasa huko Quds Mashariki na kutaka utawala huo ghasibu uchukuliwe hatua kimataifa.
 Katika upande mwingine Mussa Abu Marzuq mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Hamas ametahadharisha juu ya kukaririwa njama za kuugawa msikiti mtukufu wa al Aqswa. Amesema kuwa, Israel inataka kuugawa msikiti mtukufu wa al Aqswa kati yake na Palestina kama ulivyofanya katika msikiti wa Nabii Ibrahim (A.S). Ameongeza kuwa Wapalestina na Waislamu duniani watachukua hatua dhidi ya njama za kuugawa msikiti huo na Israel haipaswi kusahau matukio ya hivi k aribuni yaliyojiri katika mji wa Quds.
Read more »

UN yakosolewa kushindwa kuwalinda raia CAR

UN yakosolewa kushindwa kuwalinda raia CARShirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limeukosoa Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kulinda raia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku machafuko yakiendelea nchini humo. Amnesty imesema licha ya kuwepo mpango mpya wa UN katika nchi hiyo, lakini makumi ya raia wakiwemo watoto wameuawa na maelfu ya wengine kuhama makazi yao katika wiki za hivi karibuni. Shirika hilo la kutetea haki za binadamu pia limekitaka kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilichopo Jamhuri ya Afrika ya Kati kuchukua hatua madhubuti za kuwalinda raia katika wimbi jipya la mashambulio yanayowalenga Waislamu nchini humo.
 Ripoti zinasema kuwa zaidi ya watu 5,000 wameuawa katika nchi hiyo ya katikati mwa Afrika tangu Disemba mwaka jana, nchi hiyo ilipotumbukia kwenye machafuko. Machafuko hayo yalianza baada ya genge la Kikristo la Anti Balaka kuanza kuwashambulia Waislamu. 
Read more »

Magaidi 200 wa Daesh wakamatwa nchini Ufaransa

Magaidi 200 wa Daesh wakamatwa nchini UfaransaWaziri wa Mambo ya Ndani wa Iraq amesema kuwa magaidi 200 wa kundi la kitakfiri la Daesh wamekamatwa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris. Adnan al Assadi ameeleza kuwa magaidi hao wametiwa mbaroni kutokana na ushirikiano kati ya Iraq na shirika la upelelezi la Ufaransa n a kwa kufuatilia mazungumzo ya simu ya magaidi hao kati ya nchi mbili hizo.
 Katika upande mwingine Iraq imesema kuwa, kikosi chake cha anga kimeshambulia maeneo kadhaa ya magaidi wa Daesh katika mikoa ya Salahuddin na Anbar kaskazini mwa mji mkuu Baghdad. Hayo yanajiri huku jeshi la Iraq likifanikiwa kukomboa vijiji kadhaa vilivyokuwa vimetekwa na waasi wa Daesh huku mapigano yakiendelea ili kuzuia magaidi hao wasidhibiti mji wenye utajiri wa mafuta wa Baiji.
Siku ya Jumatatu Waziri Mkuu wa Iraq Haidar al Abadi alisema kuwa, mafanikio ya jeshi la nchi hiyo yaliyopatikana hivi karibuni dhidi ya kundi la kitakfiri la Daesh hayakusaidiwa na mashambulizi ya anga ya Marekani.
Read more »

Monday, November 3

Viongozi wa ECOWAS wakutana Ghana kujadili Ebola

Viongozi wa ECOWAS wakutana Ghana kujadili EbolaViongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS wanakutana nchini Ghana kwa ajili ya kujadili njia za kupambana na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola. Kikao hicho kinachowajumuisha pia viongozi wa nchi mbalimbali za dunia kinafanyika leo Jumatatu ambapo pamoja na mambo mengine kitajadilia njia zitakazoweza kusaidia kupambana na ugonjwa huo. Baada ya kikao hicho Mawaziri wa Afya kutoka nchi 47 za dunia wataelekea nchini Benin kwa ajili ya kushiriki katika kikao kingine cha 64 cha Afrika kilichoitishwa na kamisheni ya kieneo chini ya Shirika la Afya Duniani nchini Benin. Kwa mujibu wa shirika hilo la Afya WHO, hadi sasa zaidi ya watu elfu 13 na 567 wamekwisha ambukizwa virusi vya ugonjwa huo hatari katika nchi za Sierra Leone, Liberia na Guinea, huku karibu watu wengine 5000 wakiwa wamekwishapoteza maisha yao kwa ugonjw a huo Read more »

Polisi ya Burkina Faso yaanza kusafisha mji mkuu

Polisi ya Burkina Faso yaanza kusafisha mji mkuu Polisi ya Burkina Faso imeanza shughuli ya kulisafisha jiji la Ouagadougou, mji mkuu wa nchi hiyo. Katika operesheni hizo zilizoanza leo, polisi wametumia gesi ya kutoa machozi na risasi kwa lengo la kutawanya mabaki ya waandamanaji sambamba na kuwaonya wapinzani wasiendelee na maandamano yao. Polisi wametangaza kuwa, uamuzi huo umechukuliwa kwa ajili ya kurejesha usalama na amani mjini humo baada ya kufanyika maandamano na machafuko yaliyopelekea kujiuzulu Rais Blaise Compaore wa nchi hiyo. Hiyo ni baada ya kuripotiwa mapigano na vitendo vya ukatili katika maeneo tofauti ya Burkina Faso hususan mji mkuu wa nchi hiyo, Ouagadougou. Baada ya kujiuzulu Compaore, uongozi wa nchi umechukuliwa na jeshi. Tayari jeshi hilo limeahidi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kusimamia mchakato wa kisiasa ndani ya taifa hilo Read more »

Wakazi wa Benghazi Libya watakiwa kuondoka

Wakazi wa Benghazi Libya watakiwa kuondokaJeshi la Libya limewataka raia wa wilaya ya kati ya mji wa Benghazi kuondoka katika makazi yao ili kupisha operesheni inayofanywa na vikosi vya jeshi dhidi ya wanamgambo kwenye mji huo. Ahmed al Mesmari msemaji wa vikosi vya jeshi la Libya amesema kuwa, wakazi wote wa wilaya ya Assabri wanatakiwa kundoka eneo hilo leo Jumatatu.
Hayo yanajiri huku shirika la misaada la Hilali Nyekundu likiwaondosha wagonjwa katika hospitali kuu ya wazazi ya mji wa Benghazi baada ya mapigano kukaribia.  Jeshi la Libya likisaidiwa na askari watiifu kwa jenerali mstaafu Khalifa Haftar linafanya operesheni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo waliokuwa wakiudhibiti mji huo.
Zaidi ya watu 200 wameuawa mjini humo tangu jeshi lilipoanza operesheni za kuudhibiti mji huo kutoka kwa wanamgambo mwezi uliopita.
Read more »

EU yakosoa ugomvi wa madaraka nchini Somalia

EU yakosoa ugomvi wa madaraka  nchini SomaliaUmoja wa Ulaya (EU) umesema kuwa ugomvi wa kuwania madaraka nchini Somali unatishia kuimarishwa amani nchini humo. Alexander Rondos mwakilishi maalumu wa Umoja wa Ulaya katika eneo la Pembe ya Afrika leo ameelezea wasiwasi wake mkubwa kutokana na hitilafu kati ya Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somali na  Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdiweli Shekh Ahmed. Amesema kuwa hitilafu kati ya viongozi hao zinatishia jitihada zinazofanywa kwa lengo la kuimarisha amani na utulivu nchini Somalia. Ameongeza kuwa Somalia inahitajia amani na kwamba ugomvi wao wa madaraka tayari umeshaathiri utendaji wa taasisi za nchi hiyo na serikali kwa ujumla.
Waziri Mkuu wa Somalia mwezi uliopita alifanyia mabadiliko Baraza lake la Mawaziri na kuwaondoa mawaziri kadhaa mbao wapo karibu na rais wa nchi hiyo. Mabadiliko hayo yamepelekea viongozi wawili hao waingie katika mzozo na mvutano mkubwa wa kisiasa.
Read more »

Mashia ulimwenguni waomboleza siku ya Tasua

Mashia ulimwenguni waomboleza siku ya Tasua
Mamilioni ya wapenzi na wafuasi wa Imam Hussein bin Ali (A.S) nchini Iran na sehemu mbalimbali duniani wameshiriki katika maombolezo ya Tasua, siku ya 9 ya masaibu yaliyompata  mjukuu huyo wa Bwana Mtume SAW na wafuasi wake katika jangwa la Karbala huko Iraq ya leo.  Maombolezo ya Tasua hufanyika siku moja kabla ya siku ya Ashura, ambayo Imam Hussein (A.S) aliuawa kikatili na jeshi la Yazid bin Muawiyyah katika mapambano yake ya kulinda dini ya Mwenyezi Mungu. Hii ni katika ha li ambayo mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekusanyika katika mji mtukufu wa Karbala iliopo Haram tukufu ya Imam Hussein AS, kwa ajili ya maadhimisho ya Tasua na Ashura.
Mbali na Iran na Iraq maombolezo ya Tasua pia yamefanyika kwa wingi katika nchi za Pakistan, Jamhuri ya Azerbaijan na Lebanon huku hafla kama hizo pia zikifanywa na waumuni wa madhehebu ya Kiislamu ya Shia duniani kote.
Read more »

Monday, October 20

Jumatatu, Oktoba 20, 2014

Leo ni Jumatatu tarehe 25 Mfunguo 3 Dhilhija mwaka 1435 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 20 Oktoba mwaka 2014 Miladia.
Jumatatu, Oktoba 20, 2014Siku kama ya leo miaka 1400 iliyopita, Imam Ali (as) alianza kipindi cha uongozi wake wa miaka minne na miezi tisa. Imam Ali alishika hatamu za uongozi huo, baada ya uasi wa Waislamu na kuuawa khalifa wa tatu Othman bin Affan, tarehe 18 Dhulhija mwaka 35 Hijiria. Waislamu walimtaka Imam Ali (AS) ashike hatamu za uongozi huo bila ya yeye mwenyewe kutaka, lakini kutokana na mashinikizo ya Waislamu mtukufu huyo akakubali wadhifa huo mkubwa. Hata hivyo juhudi za Imam Ali (as) za kutaka kutekeleza na kueneza uadilifu na usawa katika utawala wake, zilisababisha baadhi ya watu wapenda dunia kumpinga Imam huyo.   
Miaka 62 iliyopita muwafaka na leo, Jomo Kenyatta mwanaharakati, mwanasiasa na mpigania uhuru mashuhuri barani Afrika na Rais wa Kwanza wa Kenya alitiwa mbaroni kufuatia amri ya utawala wa kikoloni nchini Kenya. Mzee Kenyatta alikuwa miongoni mwa watu 100 mashuhuri nchini humo waliotiwa mbaroni katika kipindi cha masaa 24 ikiwa ni katika fremu ya mpango wa kuibana Mau Mau, kundi la wapiganaji wa Kenya waliokuwa wakiupinga utawala wa kikoloni wa Waingereza. Siku hii inajulikana nchini humo kuwa Siku ya Mashujaa.
Miaka 216 iliyopita kama leo, wananchi Waislamu wa Cairo waliendesha mapambano ya ukombozi dhidi ya maghasibu wa Kifaransa. Mapambano ya wananchi dhidi ya jeshi la Ufaransa yalianza huko Cairo baada ya Napoleon kuikalia kwa mabavu Misri. Siku hiyo wananchi wa Cairo sambamba na wanazuoni wa dini waliandamana na kukusanyika katika Chuo Kikuu cha Al Azhar. Vita vilianza kati ya wakazi wa Cairo wasio na silaha na askari jeshi wa Ufaransa waliokuwa wamejizatiti kwa silaha kufuatia amri iliyotolewa na Jenerali De Boer, kamanda wa kijeshi wa Ufaransa aliyetaka kukandamizwa wananchi. Baadaye wananchi wa Misri waliwaua wanajeshi wengi wa Ufaransa, akiwemo Jenerali De Boer.
Na miaka 187 iliyopita kama leo vita vya majini vya Navarino au The Battle of Navarino vilitokea katika ghuba ndogo ya Navarino kwenye bahari ya Mediterranean. Katika vita hivyo, meli za kivita za Uingereza, Russia na Ufaransa zilizishambulia meli za kivita za utawala wa Othmania kwa lengo la kuihami Ugiriki. Vita hivyo vilifikia tamati kwa kushindwa vibaya utawala wa Othmania.
Read more »

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com