Siku kama ya leo miaka 58 iliyopita vita
vya mfereji wa Suez vilimalizika baada ya uingiliaji kati wa Umoja wa
Mataifa. Vita hivyo vilianza baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni
wa Israel kushambulia jangwa la Sinai na kufuatia mashambulizi ya askari
wa miavuli wa Uingereza na Ufaransa katika eneo la mfereji huo.
Serikali hizo tatu zilizotajwa zilianzisha vita hivyo kufuatia hatua ya
rais wa wakati huo wa Misri, Jamal Abdulnassir, kuutaifisha mfereji huo.
Miaka 147 iliyopita katika siku kama ya
leo Madam Escudo Doska ambaye baadaye alikuwa maarufu kwa jina la Marie
Curie alizaliwa huko Warsaw mji mkuu wa Poland. Baba
yake alikuwa
profesa wa fizikia na baadaye Madam Curie pia alielekea Paris, Ufaransa
kwa ajili ya kuendeleza masomo yake katika taaluma hiyo hiyo ya baba
yake. Madam Curie alifunga ndoa na Pierre Curie mwanafikizikia wa
Ufaransa wakati alipokuwa masomoni katika Chuo Kikuu cha Sorbonne.
Hatimaye mwanamama huyo alifanikiwa kuvumbua mada ya radium baada ya
utafiti miaka mingi. Ni vyema kuashiria hapa kuwa Madam Curie
alitunukiwa tuzo ya Nobel mara mbili katika taaluma za fizikia na kemia
na aliaga dunia mwaka 1934.
Na siku kama ya leo miaka 36 iliyopita
wananchi kote nchini Iran walifanya maandamano makubwa wakipinga kuja
madarakani serikali ya kijeshi ya Jenerali Azhari aliyekuwa kibaraka wa
utawala fasidi wa Kipahlavi. Katika maandamano hayo wananchi Waislamu wa
Iran walitangaza azimio wakisema kuwa mabadiliko ya kimaonyesho na
kubadilisha nafasi za vibaraka wa Marekani hakuwezi kuzuia mapambano yao
kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiislamu. Siku hiyo pia Kiongozi wa harakati
za Mapinduzi hayati Imam Khomeini alitoa ujumbe kwa mnasaba wa mauaji
yaliyofanywa na utawala wa Shah dhidi ya wanafunzi wa vyuo vikuu
akiwaambia wananchi kwamba: “Ninyi taifa shujaa, mumethibitisha kwamba
vifaru, mitutu ya bunduki na mikuki imeota kutu na kwamba haiwezekani
kukabiliana na irada ya chuma ya wananchi.”
0 toamaon yako: