Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, October 2

Wanamapinduzi Yemen wawanasa mabaathi wa Iraq

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Wanamapinduzi Yemen wawanasa mabaathi wa Iraq Wanamapinduzi wa Yemen wa Ansarullah wanaojulikana pia kama Mahuthi wamewatia mbaroni wataalamu wa kijeshi wa Kibaathi wa Iraq huko mji mkuu wa Yemen San'aa. Ali Qahoom, msemaji rasmi wa Mahuthi wa Yemen ameeleza kuwa maafisa wa ngazi ya juu wa Kibaathi waliingia Yemen wakitokea Iraq kwa lengo la kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Yemen na marubani wa kikosi cha anga cha nchi hiyo. Wataalamu hao wa kijeshi wa Kibaathi wa Iraq walikuwa wakishirikiana na Meja Jenerali Ali Mohsen al Ahmar, kaka wa kambo wa dikteta wa zamani wa Yemen Ali Abdallah Saleh.
Msemaji rasmi wa wanamapinduzi wa Yemen ameongeza kuwa wataalamu hao wa ngazi ya juu wa Kibaathi walikuwa wakishiriki pia katika mapigano dhidi ya wanamapinduzi wa Yemen. Wanamapinduzi wa Yemen waliwatia mbaroni maafisa hao wa Kibaathi wa Iraq baada ya kufanikiwa kuiteka kambi ya kijeshi iliyokuwa ikisimamiwa na Meja Jenerali mtoro Ali Mohsen al Ahmar mwezi uliopita wa Septemba.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com