Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, October 2

Jeshi Syria lakomboa mji mwengine wa kistratijia

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Jeshi Syria lakomboa mji mwengine wa kistratijiaKatika mfululizo wa operesheni zinazotekelezwa na jeshi la Syria za kuyakomboa maeneo yanayodhibitiwa na makundi ya kigaidi, jeshi hilo limefanikiwa kuukomboa mji wa kistratijia wa Ladhiqiyyah ulioko magharibi mwa nchi hiyo. Jeshi la Syria limeidhibiti kikamilifu miji ya Ainul-Jauzah, Ruwaisatul-Jaurah na miinuko ya kistratrijia ya mji huo wa Ladhiqiyyah sanjari na kuwaangamiza makumi ya magaidi wengi wao wakiwa na uraia wa kigeni. Aidha jeshi hilo limezidi kusonga mbele katika miji kadhaa ya Hama ambapo linatumia vifaru na silaha nyingine nzito na kuteketeza ngome za kuhifadhia silaha za makundi hayo. Aidha jeshi la Syria limeendelea na operesheni zake dhidi ya magenge hayo ya kigaidi katika mkoa wa Rif Dimashq. Hayo yanajiri katika hali ambayo John Allen, afisa wa jeshi la Marekani katika Shirika la Kijeshi la NATO, amesema kuwa nchi yake imeanza shughuli za kuyapa mafunzo makundi aliyoyaita kuwa ni ‘wapinzani wa serikali wenye siasa za wastani’ na kusisitiza kuwa, shughuli hizo zitaendelea kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa afisa huyo wa kijeshi wa Marekani, shughuli hizo zitadumu kwa miaka kadhaa

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com