Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, October 12

Mkutano wa kukarabati Gaza waanza mjini Cairo

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Mkutano wa kukarabati Gaza waanza mjini CairoWafadhili wamekusanyika mjini Cairo, Misri ili kujadili misaada inayohitajika kwa ajili ya kukarabati Ukanda wa Gaza ulioharibiwa katika mashambulizi ya hivi karibuni kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Mamlaka ya Ndani ya Palestina imesema kuwa dola bilioni 4 zinahitajika kwa ajili ya kujenga tena Ukanda wa Gaza.  Wapalestina wasiopungua 100,000 huko Gaza wamebaki bila makazi kutokana na uharibufu mkubwa uliofanywa na jeshi la Israel, huku miundo mbinu ya eneo hilo ikiharibiwa vibaya.
 Wakati huo huo Mkuu wa Kamati ya Wananchi ya Kukabiliana na Mzingiro wa Gaza amesema kuwa, mkutano wa kukarabati Gaza ni fursa kwa ajili ya kuondoa mzingiro wa kidhulma kwenye eneo hilo. Jamal al Khadhwari amesisitiza kuwa, mkutano wa kimataifa unaofanyika Cairo ni fursa nzuri kwa ajili ya kuchukuliwa misimamo ya kimataifa ya kuilazimisha Israel iondoe mzingiro wa miaka 8 dhidi ya Ukanda wa Gaza.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com