Mabaki ya utawala wa zamani wa dikteta aliyepinduliwa Tunisia
Zainul Abidin Bin Ali wanapanga kurejea katika ulingo wa kisiasa nchini
humo kwa kugombea katika uchaguzi ujao wa bunge na rais, licha ya
kukataliwa na wananchi.
Nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika yenye karibu watu milioni 5.2 waliotimiza masharti ya kupiga kura ina wagombea 13,000 wa viti 217 vya bunge kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba. Uchaguzi huo wa bunge utafuatiwa na wa rais utakaofanyika mwezi Novemba, ambapo Watunisia watapata fursa ya kumchagua rais moja kwa moja kwa mara ya kwanza tangu dikteta Zainul Abidin bin Ali apinduliwe.
Wafuasi waliobakia wa utawala wa zamani wa Tunisia wameunda chama cha kisiasa kiitwacho Desturian Movement kinachodai kwamba wafuasi wake wana uwezo wa kutosha na tajruba ya kuongoza nchi hiyo.

0 toamaon yako: