Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, October 12

Makumi wauawa katika milipuko iliyojiri Baghdad

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Makumi wauawa katika milipuko iliyojiri Baghdad Watu wasiopungua 50 wameuwa na wengine karibu 100 wamejeruhiwa kufuatia milipuko kadhaa iliyotokea kwenye mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Maafisa wa tiba na polisi wa Iraq wameripoti kuwa, milipuko hiyo ilitokea kwa kufuatana katika maeneo yenye wakazi wengi wa madhehebu ya Shia mjini Baghad jana usiku. Kuna uwezekano kuwa, mashambulizi hayo yamefanywa na wafuasi wa kundi la Daesh ambalo linapigana na jeshi la Iraq magharibi mwa nchi hiyo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani milipuko hiyo ya kigaidi iliyopelekea kuuawa raia wasio na hatia. Marzie Afkham amesema, matukio maovu ya kigaidi nchini Iraq na katika eneo zima la Mashariki ya Kati ni matokeo ya siasa za kimakosa za baadhi ya madola na pia kung’ang’ania kutumia ugaidi kama wenzo wa kisiasa. Ameongeza kuwa, Iran ina matumaini kwamba serikali na taifa la Iraq litaushinda ugaidi kwa kuimarisha umoja na mshikamano na kwa kutumia uwezo wa nchi hiyo.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com