Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, October 12

Bisimwa aikosoa vikali ripoti ya UN iliyo dhidi ya M23

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Bisimwa aikosoa vikali ripoti ya UN iliyo dhidi ya M23 Kundi la waasi wa zamani wa M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeikosoa ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa kuhusiana na unyama na ukatili uliofanywa na wanamgambo wa kundi hilo.
Bertrand Bisimwa kiongozi wa kundi la M23 ameitaja ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa kuwa siyo ya kiadilifu na imeandaliwa kiupendeleo. Hivi karibuni, Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti mpya inayolituhumu kundi la waasi wa zamani wa M23 kwa kufanya mauaji, ubakaji na utesaji dhidi ya mamia ya wananchi wa Kongo tokea mwezi Aprili 2012.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, majeshi ya Kongo yakishirikiana na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo MONUSCO yalifanya operesheni kamambe ya kulitokomeza kundi hilo na wanamgambo wa kundi hilo kulazimika kukimbilia k atika nchi za Rwanda, Uganda na Angola

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com