Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, October 12

Matukio ya Yemen; kukaririwa ya Iraq kwa usukani wa Saudi Arabia

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Matukio ya Yemen; kukaririwa ya Iraq kwa usukani wa Saudi ArabiaKatika hali ambayo, ilikuwa ikitarajiwa kwamba makubaliano ya kisiasa ya Septemba 21 kati ya Wahuthi na Rais wa muda wa Yemen, yangepelekea nchi hiyo kurejea katika amani na utulivu wa kiwango fulani, hali ya mambo haijawa kama ilivyotarajiwa, kwani nchi hiyo imeendelea kushuhudia vurugu na machafuko hususan katika siku za hivi karibuni. Kutokea milipuko kadhaa iliyopelekea kuuawa na kujeruhiwa makumi ya raia ni mfano wa wazi wa kuzorota amani na usalama wa Yemen. Baada ya mlipuko wa siku ya Alkhamisi katika mji mkuu San’aa ambao ulipelekea kuuawa na kujeruhiwa zaidi ya watu 120, Jumamosi ya jana pia wanajeshi wawili waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa kigaidi uliotokea katika eneo la Shibam huko Hadhramaut. Swali la kimsingi la kujiuliza ni kwamba, kwa nini licha ya kuweko makubaliano ya kisiasa ya Septemba 21 kati ya wapinzani na serikali ya muda ya Yemen, lakini nchi hiyo ingali inashuhudia vurugu na machafuko?
Tukitupia jicho historia ya matukio ya Yemen katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, bila shaka tunaweza kupata jibu la swali hilo. Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, serikali ya Yemen imepigana vita sita na Wahuthi na vya mwisho kabisa ni vile vya mwaka 2010 vilivyofikia tamati kwa upatanishi wa Qatar. Nukta muhimu na ya kuzingatiwa katika vita hivyo, ni msaada wa serikali ya Saudi Arabia kwa utawala wa Yemen dhidi ya Wahuthi. Katika duru ya sita ya vita dhidi ya Wahuthi huko Yemen, serikali ya Saudia ilitoa misaada ya moja kwa moja kwa utawala wa zamani wa Yemen ili uikandamize na kuisambaratisha kabisa harakati ya al-Houthi. Nchi ya Saudi Arabia ambayo ina mipaka ya pamoja na Yemen imefanya kila iwezalo kuhakikisha kwamba, upatanishi wa Qatar kwa serikali na wapinzani nchini Yemen unashindwa kuzaa matunda. Sambamba na hayo, vyombo vya habari vya Saudia vimedai kwamba, upatanishi wa Qatar nchini Yemen ni hatua zinazoongozwa na Iran. Ukweli wa mambo ni kuwa, baada ya makubaliano ya kisiasa ya Septemba 21, Saudia inajiona kuwa, imekwama na imeshindwa kufikia malengo yake huko Yemen na katu haiwezi kuvumilia ushindi wa Wahuthi mkabala na serikali ya muda ya Yemen. Ni kwa kuzingatia ukweli huo ndio maana utawala wa kifamilia wa Al-Saud umo mbioni kutekeleza nchini Yemen mtindo kama ule wa miaka ya hivi karibuni kule Iraq. Mkakati huo ni kwamba, baada ya Saudia kushindwa kuwa na ushawishi katika matukio ya Iraq na hata kutoweza kuzuia kuchukua hatamu za uongozi Waislamu wa madhehebu ya Kishia, ilianza kuendesha operesheni za mashambulio ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Mipango hiyo michafu ya Saudi huko Iraq ilikabidhiwa  baadhi ya shakhsia vibaraka. Kwa sasa Saudia inataka kutekeleza pia mipango hiyo huko nchini Yemen. Operesheni za milipuko ya mabomu ambazo zimekithiri katika masiku ya hivi karibuni nchini Yemen, lengo lake ni kusitisha na hatimaye kuzuia kabisa utekelezwaji wa makubaliano ya kisiasa ya Septemba 21 kati ya serikali ya San’aa na Wahuthi.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com