Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, October 12

Jumapili, Oktoba 12, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Jumapili, Oktoba 12, 2014Leo ni Jumapili tarehe 17 Mfunguo Tatu Dhul-Hijja mwaka 1435 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 12 Oktoba mwaka 2014 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 482 iliyopita wakoloni wa Kihispania walianzisha mashambulizi chini ya uongozi wa Francois Pizarro dhidi ya ardhi inayojulikana hii leo kwa jina la Peru. Wakati huo kaumu ya Inka ambayo ni moja kati ya kaumu za America ya Latini ndiyo iliyokuwa ikitawala eneo hilo. Viongozi wa kaumu hiyo hawakutilia maanani uvamizi wa Wahispania huku wakisalia bila kuchukua hatua zozote za kukabiliana na wavamizi hao. Baada ya kudhibitiwa ardhi ya Peru na wavamizi hao, Pizarro alimtaka mtawala wa Inka kuwa chini ya himaya ya Uhispania lakini akakataa pendekezo hilo. Pizarro alitoa amri ya mauaji ya umati dhidi ya watu wa kaumu hiyo mauaji yanayohesabiwa kuwa makubwa na mabaya zaidi katika historia ya America ya Latini. Ukubwa wa mauaji hayo ndio uliopelekea kuporomoka ustaarabu na utawala wa miaka mingi wa Inka.
Siku kama ya leo miaka 46 iliyopita, Guinea ya Ikweta (Equa torial Guinea) ilifanikiwa kupata uhuru wake kutoka kwa mkoloni Muhispania, na siku hii hutambuliwa kama siku ya kitaifa nchini humo. Equatorial Guinea iligunduliwa na mabaharia wa Ureno katika karne ya 15 Miladia. Ureno ulikikabidhi kisiwa hicho kwa Uhispania hapo mwaka 1778 Miladia, huku ukoloni wa Wahispania dhidi ya Equatorial Guinea ukiendelea hadi mwaka 1968 ambapo nchi hiyo ilijipatia uhuru wake. Equatorial Guinea inapakana na nchi za Gabon na Cameroon.
Siku kama ya leo miaka 15 iliyopita, Jenerali Parviz Musharraf, mkuu wa majeshi ya Pakistan alifanya mapinduzi yasiyo ya umwagaji damu na kumuondoa madarakani Muhammad Nawaz Sharrif Waziri Mkuu wa Pakistan wa wakati huo. Baada ya mapinduzi hayo Musharraf ambaye alichukuwa wadhifa wa urais wa nchi hiyo, alivifanyia mabadiliko baadhi ya vipengee vya katiba ya nchi hiyo, na kuongeza nguvu za rais wa nchi. Lakini kutokana na kuongezeka mashinikizo ya ndani na nje, Musharraf alisalimu amri mwezi Novemba 2007 na kuamua kung'atuka kwenye wadhifa huo. Hata hivyo ilipofika mwezi Julai 2008, aliondoka kikamilifu madarakani ikiwa ni baada ya kushika kasi vyama vya upinzani na kushinda uchaguzi wa rais.
Leo ni tarehe 20 mwezi wa Mehri kwa mujibu wa kalenda ya Kiirani, ambayo inasadifiana na maadhimisho ya Khoja Shamsuddin Muhammad Hafez Shirazi, mshairi na malenga mkubwa wa Kiirani. Hafez alizaliwa mwaka 727 Hijiria Shamsia, mjini Shiraz moja ya miji ya kusini mwa Iran. Alikuwa mtaalamu katika Tafsiri ya Qur'an, falsafa na fasihi ya Kiarabu huku akiwa mashuhuri kwa jina la Hafez kutokana na kuhifadhi kwake Qur'an Tukufu kwa visomo tofauti. Mbali na elimu hizo, Khoja Shamsuddin Muhammad Hafez, alikuwa mtaalamu mkubwa wa elimu ya Irfan.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com