Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, October 12

Jumamosi, Oktoba 11, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Jumamosi, Oktoba 11, 2014Leo ni Jumamosi tarehe 16 Mfunguo Tatu Dhil-Hija 1435 Hijria mwafaka na tarehe 11 Oktoba 2014 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 115 iliyopita vilianza vita vilivyokuwa na umwagaji damu baina ya wahajiri wa Uingereza na weupe wa Uholanzi waliojulikana kwa jina la Boer waliokuwa wakiishi nchini Afrika Kusini. Vikosi vya Uingereza vikiwa na shabaha ya kulikoloni bara la Afrika viliwasili Afrika Kusini mwaka 1841, na baada ya kujenga makazi vilibaki katika nchi hiyo. Baada ya kugunduliwa ya almasi na dhahabu nchini Afrika Kusini, wimbi la wahajiri kutoka Ulaya hasa Uingereza kuelekea nchini humo lilikithiri. Kutokana na wahajiri wa mwanzo nchini Afrika Kusini yaani wahajiri wa Kiholanzi waliojulikana kwa jina la Boer kupinga kuwasili wahajiri wengine, kulizuka vita baina yao na wahajiri wa Uingereza. Wahajiri wa Kiholanzi walishindwa katika vita hivyo kutokana na serikali ya Uingereza kuwaunga mkono wahajiri wa Kiingereza.***
Miaka 23 iliyopita katika siku kama ya leo, shughuli za Shirika la Ujasusi la Urusi ya zamani (KGB) zilifikia kikomo muda mfupi kabla ya kusambaratika nchi hiyo. KGB iliundwa mwaka 1954 kwa lengo la kukabiliana na harakati zilizokuwa na lengo la kuuangusha mfumo wa Kikomonisti wa Urusi ya zamani. Shirika hilo aidha lilikuwa na majukumu kama vile kuwakandamiza wapinzani wa chama cha Kikomonisti na kuendesha operesheni za kijasusi na zile zilizo dhidi ya ujasusi ndani na nje ya Muungano wa Kisovieti.***
Katika siku kama ya leo miaka 30 iliyopita, Ayatullah Haji Mirza Khalil Kamarei mfasiri wa Qur'ani Tukufu na mhadhiri wa chuo kikuu alifariki dunia. Ayatullah Ka marei alijifunza elimu za fiqih, usul-fiqih na masomo mengine ya kidini katika Hauza ya kielimu ya mji mtakatifu wa Qum nchini Iran na baadaye alianza kufundisha falsafa. Mwaka 1341 Hijria Shamsia alikamatwa na kufungwa jela kutokana na kupinga siasa za kidhalimu na utawala wa Shah. Haji Kamarei ameandika vitabu vingi kwa lugha za Kifarsi na Kiarabu. Miongoni mwa vitabu hivyo ni tafsiri ya Qur'ani, sherhe ya Nahjul Balagha na kitabu cha maisha ya Imam Hussein AS na mashahidi wengine wa Karbala.
Na miaka 99 iliyopita katika siku kama ya leo alifariki dunia Jean Henri Fabre msomi wa elimu ya sayansi na bingwa wa elimu ya wadudu au entomolojia. Fabre alizaliwa mwaka 1823 nchini Ufaransa. Msomi huyo ambaye pia alikuwa mwandishi amefanya utafiti mkubwa na kuandika vitabu kadhaa kwenye uwanja wa elimu ya wadudu.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com