Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, October 2

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataka mzingiro wa Ghaza uondoshwe

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataka mzingiro wa Ghaza uondoshweBan Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekutana na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel mjini New York, ambapo sanjari na kumtaka asimamishe ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina, amesisitiza juu ya kuondoshwa mzingiro wa kidhuluma wa Israel dhidi ya eneo la Ukanda wa Ghaza. Zikiwa zimepita siku kadhaa tokea yalipofikiwa makubaliano ya usitishaji vita huko Ghaza chini ya upatanishi wa serikali ya Misri, utawala wa Israel hadi sasa bado haujaheshimu na kutekeleza vipengee vya makubaliano hayo. Taarifa zinasema kuwa, utawala huo ghasibu bado unaendeleza sera za kiadui dhidi ya Wapalestina ikiwemo kuendeleza mzingiro dhidi ya Ghaza. Utawala wa Israel ulianza kulishambulia eneo la Ukanda wa Ghaza tarehe 8 Julai na mashambulio hayo yalidumu hadi tarehe 26 Agosti, lakini utawala huo ghasibu ulishindwa kufikia malengo yake haramu. Licha ya kutiwa saini makubaliano ya usitishaji vita, utawala wa Israel bado unaendeleza mbinyo dhidi ya Wapalestina wa Ghaza. Kuhusiana na suala hilo, Wizara ya Vita ya Israel imeeleza azma ya kujenga eti 'ukuta wa kiusalama' katika mpaka na Ukanda wa Ghaza. Duru hizo zimedai kuwa, ukuta huo utasaidia kupunguza vitisho vya Wapalestina katika vitongoji vya Wazayuni vinavyopakana na Ghaza. Taarifa zinasema kuwa, ukuta huo utakuwa na nyaya zitakazotoa indhari pindi mtu yeyote atakapojaribu kuuvuka ukuta huo na kuingia kwenye vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. Duru hizo zimeeleza kuwa, ujenzi wa ukuta huo umeshaanza na utafanana na ule wa Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan. Ripoti kutoka vyombo vya usalama vya Israel zinaeleza kuwa, mtu yeyote atakayejaribu kuvuka ukuta huo atahesabiwa kuwa ni adui na kufyatuliwa risasi. Vitendo vya kichokozi vya utawala wa Israel kama vile upanuzi wa vitongoji ni miongoni mwa ajenda za viongozi wa utawala huo haramu. Hakuna shaka kuwa, uungaji mkono wa kibubusa wa madola ya Magharibi kwa utawala huo khabithi na uzembeaji wa jamii ya kimataifa katika kukabiliana na utawala huo, vimeifanya Israel ivimbe kichwa na kuendeleza siasa zake za ukandamizaji dhidi ya Wapalestina. Ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa, wakaazi wa eneo la Ghaza wanakabiliwa na hali mbaya ya kimaisha na kiuchumi iliyosababishwa na mzingiro wa kidhuluma. Utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia sera mbalimbali zilizo dhidi ya ubinadamu kama vile kuyazingira maeneo ya Wapalestina na kuyageuza maeneo hayo kuwa gereza kubwa kwa wananchi hao madhulumu. Mamia ya wananchi wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza wamefariki dunia katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mzingiro huo. Hii ni katika hali ambayo, idadi kubwa ya Wapalestina na hasa wagonjwa wanakabiliwa na hatari ya kifo, suala  ambalo limeitia wasiwasi kubwa jamii ya kimataifa akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com