Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, October 2

Iraq yakataa ushiriki wa Waarabu dhidi ya Daesh

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Iraq yakataa ushiriki wa Waarabu dhidi ya DaeshHaydar al Abadi, Waziri Mkuu wa Iraq amepinga vikali ushiriki wa nchi za Kiarabu kwenye mashambulio ya anga ya Marekani dhidi ya ngome za matakfiri wa Daesh nchini humo. Matamshi ya Waziri Mkuu wa Iraq yanatolewa katika hali ambayo, nchi za Saudi Arabia, Jordan, Bahrain, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu zinashirikiana na Marekani kwenye mashambulio ya anga dhidi ya wanamgambo wa Daesh nchini Syria. Haydar al Abadi amesisitiza kuwa, hakuna mwanajeshi yoyote wa kigeni atakayeruhusiwa kuingia ndani ya ardhi ya Iraq kwa shabaha ya kupambana na magaidi wa Daesh.
Waziri Mkuu wa Iraq ameongeza kuwa, migongano ya kimataifa na kieneo imesababisha kuibuka kundi la Daesh katika eneo la Mashariki ya Kati. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kundi la kigaidi la Daesh lililoanzishwa na kupata msaada mkubwa wa silaha na kifedha kutoka nchi za Magharibi na za Kiarabu za eneo la Mashariki ya Kati linadhibiti sehemu kubwa ya ardhi za Syria na Iraq, na limetekeleza jinai mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaua kwa umati wananchi wa nchi hizo mbili.
       

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com