Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, October 2

Jumatano, Oktoba Mosi, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Leo ni Jumatano tarehe 6 Dhulhija 1435 Hijria inayosadifiana na tarehe Mosi Oktoba 2014.
Jumatano, Oktoba Mosi, 2014Tarehe 6 Dhilhaji mwaka 1407 Hijria yaani siku kama ya leo miaka 28 iliyopita mamia ya mahujaji wa Kiirani na mahujaji kadhaa wa nchi nyinginezo wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu waliuawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa serikali ya Saudi Arabia, walipokuwa wakitekeleza faradhi ya kujibari na kujiweka mbali na washirikina. Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu hutekeleza ibada hiyo kila mwaka wakati wa Hija, kutokana na mafunzo ya Kiislamu na Qur'ani Tukufu, ambapo sambamba na kutoa wito wa umoja na mshikamano baina ya Waislamu, hutoa tangazo la kujiweka mbali na maadui wa Uislamu hasa Marekani na utawala ghasibu wa Israel. Kwa kutilia maanani umuhimu wa suala hiyo mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) daima alikuwa akisisitiza katika ujumbe wake kwa wahujaji juu ya kufanya shughuli hiyo ya kujitenga na washirikina na mabeberu, na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei pia amekuwa akisisitiza sana juu ya umuhimu wa kufanyika kwake na kwamba inawaamsha Waislamu na kudhihirisha uwezo na nguvu zao.
Miaka 29 iliyopita sawa na siku kama ya leo ya tarehe Mosi Oktoba mwaka 1985 ndege za kijeshi za utawala haramu wa Israel ziliyashambulia makao ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) huko Tunisia. Watu wapatao 70 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia mashambulio hayo. PLO ilikuwa imehamishia makao yake Tunisia kutoka Lebanon baada ya mashambulio ya kijeshi ya utawala haramu wa Israel nchini humo mwaka 1982. Hata hivyo uungaji mkono wa Marekani kwa utawala huo ulilifanya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lishindwe kuchukua hatua zozote za maana dhidi ya Tel Aviv.
Na Siku kama ya leo miaka 54 iliyopita, nchi ya Nigeria ilipata uhuru. Wareno waliwasili Nigeria katika karne ya 15 na mkoloni Mwingereza naye akawasili katika nchi hiyo katika karne ya 16. Katika karne ya 17 ardhi ya Nigeria iligeuzwa na kuwa moja kati ya vituo muhimu vya biashara ya utumwa. Mwishoni mwa karne ya 19 vikosi vya jeshi la Uingereza viliidhibiti kikamilifu ardhi ya Nigeria. Mwaka 1914 Uingereza iliziunganisha nchi mbili za Nigeria ya Kaskazini na Kusini zilizokuwa chini ya udhibiti wake na kuunda koloni moja la Nigeria. Miaka 40 baadaye nchi hiyo ilijitangazia  utawala wa ndani. Hatimaye baada ya kupitia misukosuko mingi, Nigeria ilipata uhuru katika siku kama hii ya leo.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com