Tarehe 30 Septemba miaka 29
iliyopita alifariki dunia mvumbuzi wa kipimo kinachotumiwa kupimia nguvu
ya mitetemeko ya ardhi Charles Richter. Charles Richter alishirikiana
na mhakiki mwingine kusanifu nguvu ya mitetemeko kwa mujibu wa nishati
inayotokana na mawimbi ya mitetemeko hiyo toka daraja moja hadi 9 na
kusajili kipimo cha Rishta. Kabla ya hapo wataalamu walikuwa wakipima
mitetemeko ya ardhi kwa mujibu wa athari zake, kipimo ambacho hakikuwa
cha kuaminika.
Siku kama ya leo miaka 48
iliyopita nchi ya Botswana ilifanikiwa kupata uhuru kutoka kwa mkoloni
Mwingereza. Mwaka 1885 Botswana iliwekwa katika himaya ya mkoloni
Mwingereza. Tangu mwaka 1920 mapambano makali ya wapigania uhuru nchini
humo yalishadidi na Botswana ikapata uhuru mwaka 1966 na kukaundwa
serikali ya jamhuri. Botswana inap
atikana kusini mwa bara la Afrika na
inapakana na nchi za Afrika Kusini, Zimbabwe na Namibia.
Na siku kama ya leo miaka 74
iliyopita, alifariki dunia huko Najaf, Iraq Allamah Muhammad Hussein
Kampani, mwanafalsafa, faqihi na mwanairfani mkubwa. Alizaliwa mwaka
1296 Hijria mjini Kadhimain nchini Iraq. Msomi huyo mkubwa pia
alitabahari katika elimu za falsafa, tiba, irfan, historia, kijografia,
mashairi na fasihi. Mbali na hayo Allamah Hussein Kampani alikuwa na
fikra pevu na uwezo mkubwa wa kubainisha mambo. Msomi huyo ameandika
vitabu kadhaa katika nyanja mbalimbali ikiwemo diwani ya mashairi
akisifu viongozi wa Uislamu
0 toamaon yako: