Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, October 2

Jumatatu, Septemba 29, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Leo ni Jumatatu tarehe 4 Mfunguo tatu Dhil-Hijja mwaka 1435 Hijiria inayosadifiana na tarehe 29 Septemba mwaka 2014 Miladia.

Jumatatu, Septemba 29, 2014
Siku kama ya leo miaka 22 iliyopita, ulifanyika uchaguzi huru wa kwanza nchini Angola. Katika uchaguzi huo chama cha MPLA kilichokuwa kikiongoza nchini humo tangu mwaka 1976 kilipata ushindi na kiongozi wake Jose Edward Dos Santos akachaguliwa tena kuingoza nchi hiyo. Ni vyema kuashiria hapa kwamba, Angola ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya kupata uhuru kutoka kwa mkoloni Mreno hapo mwaka 1975. Vita vya ndani nchini humo vilihitimishwa rasmi mwaka 2002 baada ya kuuawa kiongozi wa chama cha upinzani cha UNITA Jonas Savimbi.
Siku kama ya leo miaka 33 iliyopita, muwafaka na tarehe 7 Mehr 1360 Hijria Shamsia, aliuawa shahidi Hujjatul Islam Sayyid Abdul Karim Hasheminejad mwanachuoni na mwana mapambano shupavu wa Iran katika mji wa Mashhad. Sayyid Hasheminejad aliuawa shahidi baada ya kupigwa risasi na mmoja wa wanachama wa kundi la Munafikiin. Mwanachuoni huyo alikuwa mstari wa mbele katika harakati za mapinduzi nchini Iran dhidi ya utawala wa Shah, na aliwahi kuteswa na kuwekwa gerezani mara kadhaa.
Siku kama ya leo miaka 113 iliyopita, alizaliwa mwanafizikia mashuhuri wa Italia Enrico Fermi katika mji wa Roma. Baada ya kukamilisha masomo ya chuo kikuu aliweza kuvumbua kanuni ya Mwendo wa Molekuli ya Gesi. Fermi alifanya uchunguzi kuhusu mabadiliko ya atomu na akafanikiwa kutengeneza betri ya atomu kwa kuipasua na kutoa nje nishati yake. Mwanafizikia huyo wa Italia alifariki dunia mwaka 1954.
Na miaka 96 iliyopita muwafa na leo, nchi ya Bulgaria ilisalimu amri baada ya kushindwa mara kadhaa katika Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia. Bulgaria ilikuwa pamoja na Ujerumani, utawala wa Othmania, Austria na Hungary na zilikuwa zikipigana dhidi ya Ufaransa, Russia, Uingereza na Italia. Baada ya Bulgaria kushindwa katika vita vya Macedonia, Desemba 15 mwaka 1918 ilitia saini Mkataba wa Salonica katika mji wenye jina hilo nchini Ugiriki ya leo

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com