Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, September 28

Naibu Waziri wa Liberia ajiwekea karantini ya Ebola

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Naibu Waziri wa Liberia ajiwekea karantini ya EbolaNaibu Waziri wa Afya wa Liberia ameamua kujiwekea karantini ya siku 21 kwa hiyari yake mwenyewe, baada ya sekretari wa ofisi yake kufariki dunia kwa maradhi ya Ebola.
Bi. Bernice Danh Naibu Waziri wa Afya wa Liberia amesema kuwa, hana dalili zozote za maradhi ya Ebola lakini anakusudia kujiwekea karantini ya kutokutana na watu ili apate yakini kwamba hana maradhi hayo. Naibu Waziri wa Afya wa Liberia amewataka wafanyakazi wote katika ofisi yake kubaki nyumbani kwa muda wa wiki tatu.
Shirika la Afya Duniani 'WHO' limetangaza kuwa, zaidi ya watu 3,000 wamepoteza maisha yao kutokana na maradhi ya Ebola ambayo yameshambulia zaidi katika nchi za Liberia, Sierra Leone na Guinea. Hadi sasa hakujapatikana dawa wala chanjo inayoweza kutibu maradhi hayo hatari.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com