Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, September 28

Jumapili, 28 Septemba 2014 09:24 Rais Samba ataka vikwazo vya silaha viondolewe CAR

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Rais Samba ataka vikwazo vya silaha viondolewe CARRais Catherine Panza –Samba wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameutaka Umoja wa Mataifa kuangalia upya na hatimaye kuviondoa vikwazo vya silaha vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo. Akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Panza- Samba amesema kuwa, iwapo vitaondoshwa vikwazo vya silaha dhidi ya nchi hiyo, majeshi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kushirikiana na Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa yataweza kurejesha amani kwa kiasi fulani nchini humo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Disemba mwaka jana liliweka vikwazo vya silaha dhi di ya nchi hiyo baada ya kushadidi ghasia na mapigano kati ya makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha. Mwezi Mei mwaka huu, Baraza la Usalama pia liliwawekea vikwazo Francois Bozize rais aliyeondolewa madarakani pamoja na viongozi wawili wa makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha kwa kuhusika na machafuko ya nchini humo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha maelfu ya watu kuuawa na wengine zaidi ya milioni moja kuwa wakimbizi.
     

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com