Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, September 28

Jumapili, 28 Septemba Ghandour: Wakazi wa Darfur wajiepushe na maadui

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Ghandour: Wakazi wa Darfur wajiepushe na maaduiMakamu wa Rais wa Sudan amewataka wakazi wa eneo lililogubikwa na ghasia na machafuko la Darfur kuwa macho na njama za maadui za kuzusha mifarakano.
Ibrahim Ghandour amesema kuwa, maadui wa Sudan wanafanya njama za kuibua mifarakano na hitilafu kati ya wakaazi wa eneo la Darfur na kusisitiza kwamba, wakazi wa eneo hilo wanapaswa kuwa macho na kuimarisha umoja na mshikamano wao kwa lengo la kuzima njama hizo za maadui.
Makamu wa Rais wa Sudan amesema kuwa, chimbuko la ghasia na machafuko katika eneo hilo ni uungaji mkono wa baadhi ya madola ya kigeni kwa vibaraka wao na kusisitiza kwamba baadhi ya mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi yanafanya njama za kuzusha mapigano ya kikabila na kikoo katika eneo hilo, ili yaweze kufikia malengo yao machafu. Makamu wa Rais wa Sudan ameyataka makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha katika eneo hilo kuweka chini silaha zao na kuketi kwenye mazungumzo ya amani na serikali ya Khartoum.
Eneo la Darfur lililoko magharibi mwa Sudan linajumuisha majimbo matano na tokea mwaka 2003 hadi sasa linasumbuliwa na mapigano kati ya makundi ya waasi na wanajeshi wa serikali.
     

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com