Jeshi la Libya limewataka raia wa wilaya ya kati ya mji wa
Benghazi kuondoka katika makazi yao ili kupisha operesheni inayofanywa
na vikosi vya jeshi dhidi ya wanamgambo kwenye mji huo. Ahmed al Mesmari
msemaji wa vikosi vya jeshi la Libya amesema kuwa, wakazi wote wa
wilaya ya Assabri wanatakiwa kundoka eneo hilo leo Jumatatu.Hayo yanajiri huku shirika la misaada la Hilali Nyekundu likiwaondosha wagonjwa katika hospitali kuu ya wazazi ya mji wa Benghazi baada ya mapigano kukaribia. Jeshi la Libya likisaidiwa na askari watiifu kwa jenerali mstaafu Khalifa Haftar linafanya operesheni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo waliokuwa wakiudhibiti mji huo.
Zaidi ya watu 200 wameuawa mjini humo tangu jeshi lilipoanza operesheni za kuudhibiti mji huo kutoka kwa wanamgambo mwezi uliopita.

Facebook
Twitter
RSS
0 toamaon yako: