Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, November 3

Polisi ya Burkina Faso yaanza kusafisha mji mkuu

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Polisi ya Burkina Faso yaanza kusafisha mji mkuu Polisi ya Burkina Faso imeanza shughuli ya kulisafisha jiji la Ouagadougou, mji mkuu wa nchi hiyo. Katika operesheni hizo zilizoanza leo, polisi wametumia gesi ya kutoa machozi na risasi kwa lengo la kutawanya mabaki ya waandamanaji sambamba na kuwaonya wapinzani wasiendelee na maandamano yao. Polisi wametangaza kuwa, uamuzi huo umechukuliwa kwa ajili ya kurejesha usalama na amani mjini humo baada ya kufanyika maandamano na machafuko yaliyopelekea kujiuzulu Rais Blaise Compaore wa nchi hiyo. Hiyo ni baada ya kuripotiwa mapigano na vitendo vya ukatili katika maeneo tofauti ya Burkina Faso hususan mji mkuu wa nchi hiyo, Ouagadougou. Baada ya kujiuzulu Compaore, uongozi wa nchi umechukuliwa na jeshi. Tayari jeshi hilo limeahidi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kusimamia mchakato wa kisiasa ndani ya taifa hilo

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com