Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, November 3

Viongozi wa ECOWAS wakutana Ghana kujadili Ebola

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Viongozi wa ECOWAS wakutana Ghana kujadili EbolaViongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS wanakutana nchini Ghana kwa ajili ya kujadili njia za kupambana na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola. Kikao hicho kinachowajumuisha pia viongozi wa nchi mbalimbali za dunia kinafanyika leo Jumatatu ambapo pamoja na mambo mengine kitajadilia njia zitakazoweza kusaidia kupambana na ugonjwa huo. Baada ya kikao hicho Mawaziri wa Afya kutoka nchi 47 za dunia wataelekea nchini Benin kwa ajili ya kushiriki katika kikao kingine cha 64 cha Afrika kilichoitishwa na kamisheni ya kieneo chini ya Shirika la Afya Duniani nchini Benin. Kwa mujibu wa shirika hilo la Afya WHO, hadi sasa zaidi ya watu elfu 13 na 567 wamekwisha ambukizwa virusi vya ugonjwa huo hatari katika nchi za Sierra Leone, Liberia na Guinea, huku karibu watu wengine 5000 wakiwa wamekwishapoteza maisha yao kwa ugonjw a huo

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com