Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iraq
amesema kuwa magaidi 200 wa kundi la kitakfiri la Daesh wamekamatwa
katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris. Adnan al Assadi ameeleza kuwa
magaidi hao wametiwa mbaroni kutokana na ushirikiano kati ya Iraq na
shirika la upelelezi la Ufaransa n
a kwa kufuatilia mazungumzo ya simu ya
magaidi hao kati ya nchi mbili hizo.
Katika upande mwingine Iraq imesema
kuwa, kikosi chake cha anga kimeshambulia maeneo kadhaa ya magaidi wa
Daesh katika mikoa ya Salahuddin na Anbar kaskazini mwa mji mkuu
Baghdad. Hayo yanajiri huku jeshi la Iraq likifanikiwa kukomboa vijiji
kadhaa vilivyokuwa vimetekwa na waasi wa Daesh huku mapigano yakiendelea
ili kuzuia magaidi hao wasidhibiti mji wenye utajiri wa mafuta wa
Baiji.
Siku ya Jumatatu Waziri Mkuu wa Iraq
Haidar al Abadi alisema kuwa, mafanikio ya jeshi la nchi hiyo
yaliyopatikana hivi karibuni dhidi ya kundi la kitakfiri la Daesh
hayakusaidiwa na mashambulizi ya anga ya Marekani.

Facebook
Twitter
RSS
0 toamaon yako: