
Shirika la Msamaha Duniani la
Amnesty International limeukosoa Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kulinda
raia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku machafuko yakiendelea nchini
humo. Amnesty imesema licha ya kuwepo mpango mpya wa UN katika nchi
hiyo, lakini makumi ya raia wakiwemo watoto wameuawa na maelfu ya
wengine kuhama makazi yao katika wiki za hivi karibuni. Shirika hilo la
kutetea haki za binadamu pia limekitaka kikosi cha kulinda amani cha
Umoja wa Mataifa kilichopo Jamhuri ya Afrika ya Kati kuchukua hatua
madhubuti za kuwalinda raia katika wimbi jipya la mashambulio
yanayowalenga Waislamu nchini humo.
Ripoti zinasema kuwa zaidi ya watu
5,000 wameuawa katika nchi hiyo ya katikati mwa Afrika tangu Disemba
mwaka jana, nchi hiyo ilipotumbukia kwenye machafuko. Machafuko hayo
yalianza baada ya genge la Kikristo la Anti Balaka kuanza kuwashambulia
Waislamu.
0 toamaon yako: