
Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na
Siasa za Upande Wowote (NAM) imelaani mashambulio ya hivi karibuni ya
Israel dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina. Ghulam-Hussein Dehqani,
mwakilishi wa Iran katika Jumuiya hiyo amesema kwamba, mashambulio ya
kila siku, kubomolewa nyumba na miundombinu katika Ukanda wa Gaza na
kushambuliwa vituo vya umeme, hospitali na vyanzo vya maji na pia maeneo
ya Umoja wa Mataifa sio tu ni janga kubwa bali ni ukiukwaji wa wazi wa
haki za binadamu. Ameongeza kuwa, Israel pia inakiuka haki za raia wa
Palestina na hasa huko Quds Mashariki na kutaka utawala huo ghasibu
uchukuliwe hatua kimataifa.
Katika upande mwingine Mussa Abu Marzuq
mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Hamas ametahadharisha juu ya
kukaririwa njama za kuugawa msikiti mtukufu wa al Aqswa. Amesema kuwa,
Israel inataka kuugawa msikiti mtukufu wa al Aqswa kati yake na
Palestina kama ulivyofanya katika msikiti wa Nabii Ibrahim (A.S).
Ameongeza kuwa Wapalestina na Waislamu duniani watachukua hatua dhidi ya
njama za kuugawa msikiti huo na Israel haipaswi kusahau matukio ya hivi
k
aribuni yaliyojiri katika mji wa Quds.
0 toamaon yako: