Umoja wa Ulaya (EU) umesema kuwa ugomvi wa kuwania madaraka
nchini Somali unatishia kuimarishwa amani nchini humo. Alexander Rondos
mwakilishi maalumu wa Umoja wa Ulaya katika eneo la Pembe ya Afrika leo
ameelezea wasiwasi wake mkubwa kutokana na hitilafu kati ya Rais Hassan
Sheikh Mahmoud wa Somali na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdiweli Shekh
Ahmed. Amesema kuwa hitilafu kati ya viongozi hao zinatishia jitihada
zinazofanywa kwa lengo la kuimarisha amani na utulivu nchini Somalia.
Ameongeza kuwa Somalia inahitajia amani na kwamba ugomvi wao wa madaraka
tayari umeshaathiri utendaji wa taasisi za nchi hiyo na serikali kwa
ujumla.Waziri Mkuu wa Somalia mwezi uliopita alifanyia mabadiliko Baraza lake la Mawaziri na kuwaondoa mawaziri kadhaa mbao wapo karibu na rais wa nchi hiyo. Mabadiliko hayo yamepelekea viongozi wawili hao waingie katika mzozo na mvutano mkubwa wa kisiasa.

Facebook
Twitter
RSS
0 toamaon yako: