Mamilioni ya wapenzi na wafuasi wa Imam Hussein bin Ali (A.S) nchini Iran na sehemu mbalimbali duniani wameshiriki katika maombolezo ya Tasua, siku ya 9 ya masaibu yaliyompata mjukuu huyo wa Bwana Mtume SAW na wafuasi wake katika jangwa la Karbala huko Iraq ya leo. Maombolezo ya Tasua hufanyika siku moja kabla ya siku ya Ashura, ambayo Imam Hussein (A.S) aliuawa kikatili na jeshi la Yazid bin Muawiyyah katika mapambano yake ya kulinda dini ya Mwenyezi Mungu. Hii ni katika ha li ambayo mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekusanyika katika mji mtukufu wa Karbala iliopo Haram tukufu ya Imam Hussein AS, kwa ajili ya maadhimisho ya Tasua na Ashura.
Mbali na Iran na Iraq maombolezo ya Tasua pia yamefanyika kwa wingi katika nchi za Pakistan, Jamhuri ya Azerbaijan na Lebanon huku hafla kama hizo pia zikifanywa na waumuni wa madhehebu ya Kiislamu ya Shia duniani kote.
0 toamaon yako: