Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 13

Wazazi wa wasichana waliotekwa Nigeria waja juu

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Wazazi wa wasichana waliotekwa Nigeria  waja juuWazazi na familia za wasichana wasiopungua 250 wa shule ya sekondari ya bweni ambao walitekwa nyara miezi sita iliyopita na wanamgambo wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria, wametaka kutosahauliwa hatima ya watoto wao. Wazazi na familia za watoto hao ambao wameunda harakati waliyoipa jina la 'Warejesheni watoto wetu' walikusanyika jana na kuitaka serikali ya Nigeria kuongeza juhudi za kuwakomboa wasichana hao. Mratibu wa harakati hiyo ameeleza kwenye mjumuiko huo  na hapa tunamnuku u:' Leo hii tunawaombeni mufanye jitihada zote za kuhakikisha watoto wetu wanarudi wakiwa salama', mwisho wa kunukuu. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kundi la Boko Haram liliwashikilia mateka wasichana wapatao 270 wa shule ya sekondari ya bweni ya Chibok iliyoko katika jimbo la Borno na hadi sasa haijajulikana hatima yao. Kundi la Boko Haram lilitoa masharti ya kuwaachia wasichana hao mkabala wa kuachiliwa huru wanamgambo na baadhi ya viongozi wa kundi hilo la kigaidi wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama vya Nigeria. Serikali ya Nigeria ilitupilia mbali takwa la kundi hilo, na kusisitiza kuendeleza operesheni za kuwakomboa wasichana hao

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com