Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 13

Maradhi ya kipindupindu yaua watu 72 Congo DR

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Maradhi ya kipindupindu yaua watu 72 Congo DRKwa akali watu 72 wamefariki dunia baada ya kukumbwa na maradhi ya kipindupindu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Dakta Mathilde Kisungi amesema kuwa, ukosefu wa huduma za vyoo na kuoga  kwenye mito na maji yaliyotuama kumechangia kwa kiasi kikubwa kusambaa maradhi ya kipindupindu nchini humo. Naye Dakta Adalbert Ngandwe Manda Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika iliyoko kusini mashariki mwa Kongo amesema kuwa, idadi ya watu waliokumbwa na maradhi ya ki pindupindu imeongezeka kwa kasi katika eneo hilo. Dakta Manda ameongeza kuwa, tokea mwezi Agosti hadi sasa, jumla ya watu wasiopungua 72  tayari wameshafariki dunia kutokana na maradhi hayo.  Hii ni katika hali ambayo, idadi ya watu waliofariki dunia katika wilaya ya Tanganyika kutokana na maradhi ya Ebola katika kipindi hichohicho ni  arubaini na tatu. Inafaa kuashiria hapa kuwa, zaidi ya watu 4,000 wameshafariki dunia kutokana na maradhi ya Ebola barani Afrika na hasa katika nchi za Guinea, Liberia, Sierra Leone, Senegal, Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com