Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 13

Sudan Mbili kujadili amani katika mipaka yao

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Sudan Mbili kujadili amani katika mipaka yaoKamati ya pamoja ya kisiasa na kiusalama ya Sudan na Sudan Kusini imetangaza kwamba, Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan na mwenzake Salva Kiir wa Sudan Kusini watakutana wiki hii kwa minajili ya kujadili kwa kina masuala ya kiusalama na mashirikiano ya pande hizo mbili. Duru za habari kutoka Khartoum zinasema kuwa, viongozi hao watajadili suala la kuainishwa mpaka wa pamoja, kutangaza eneo linalopaswa kutokuwa na silaha na vilevile kuwaondoa wanamgambo wanaobeba silaha katika e neo hilo. Wakuu wa nchi za Sudan na Sudan Kusini watajadiliana kwa kina pia suala la kuimarishwa usalama na kufunguliwa vivuko kwenye mpaka wa nchi hizo mbili. Imeelezwa kuwa, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini siku ya Alhamisi ataelekea Khartoum kwa minajili ya kukutana na Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan. Inafaa kuashiria hapa kuwa, licha ya pande hizo mbili kutiliana saini utekelezwaji wa makubaliano ya mashirikiano ya pande mbili mwezi Machi mwaka jana, amma  bado zinahitilafiana kuhusiana na umiliki wa eneo Abyei, ambalo lina utajiri mkubwa wa mafuta.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com