Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 13

Bunge la Kimataifa; ni fursa nzuri ya kuwepo fikra za pamoja duniani

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Dakta Ali Larijani Spika wa Majlis ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) jana aliongoza ujumbe wa ngazi za juu wa bunge kwa shabaha ya kushiriki kikao cha 131 cha Muungano wa Mabunge Duniani kinachoanza leo mjini Geneva, Uswisi. Hapo jana, Dakta Larijani alishiriki kikao cha Jumuiya ya Mabunge ya Asia na Pasifiki mjini Geneva.
Kikao cha mwaka huu cha Muungano wa Mabunge Duniani kinafanyika huku ulimwengu ukishuhudia kuongezeka vita, mapigano na harakati za makundi ya kigaidi ambazo zinatishia amani na utulivu duniani. Mabunge yakiwa ni mhimili uliochaguliwa na wananchi, yanaweza kuwa na nafasi kubwa ya kuimarisha mashirikiano kati ya mataifa, utamaduni na dini mbalimbali kwa lengo la kutatua matatizo na kukabiliana na vitisho vilivyopo. Kwa minajili hiyo, masuala kama vile haki za binadamu, ugaidi, ukandamizaji, uchupaji mipaka, amani na usalama duniani ni miongoni mwa ajenda kuu zinazotarajiwa kujadiliwa kwa kina kwenye kikao hicho. Amma swali linalojitokeza hapa ni hili kwamba, je mabunge yanaweza kuwa na uwezo wa kuchukua hatua mwafaka katika kutatua matatizo na kero zilizopo? Au kikao hicho cha Geneva kitaweza kuwa na fikra za pamoja na kuchukua maamuzi yasiyokuwa ya kimaonyesho kwa lengo la kukabiliana na ugaidi na matatizo yanayoukumba ulimwengu kwa hivi sasa?
Bunge la Kimataifa; ni fursa nzuri ya kuwepo fikra za pamoja dunianiHakuna shaka kwamba, sharti la kwanza katika kufanikiwa jambo hilo, ni kwa nchi zote kukiri kwamba zinakabiliwa na tishio la makundi ya kigaidi. Hata hivyo jukumu la mabunge hayo la kukabiliana na ugaidi linakuwa hata gumu zaidi pale tunapotambua kuwa, baadhi ya nchi licha ya kukabiliwa na upinzani wa wananchi wao, zimekuwa zikiyaunga mkono moja kwa moja makundi hayo kwa kisingizio cha eti kupambana na ugaidi. Ukweli huo mchungu unashuhudiwa kwa Marekani na baadhi ya washirika wake kutoka Ulaya pamoja na nchi za Kiarabu ambazo zinatoa bila kusita misaada ya fedha, silaha na uungaji mkono wao kwa makundi ya kigaidi. Na ndiyo maana leo hii tunashuhudia vitisho na harakati za ugaidi zikipamba moto ulimwenguni kote.
Leo hii magaidi wanapanda mbegu za ghasia na machafuko sanjari na kufuta utamaduni na thamani za kidini na kibinadamu duniani. Katika hali kama hii tata na nyeti inatazamiwa kuwa, mabunge yakiwa ni asasi ya wananchi yataweza kulichukulia suala hili kwa uzito mkubwa bila ya kuathiriwa na mirengo ya kisiasa. Hivi sasa ulimwengu unashuhudia raia wa Ulaya wakiwa wamejiunga na makundi ya kigaidi, na kufanya mauaji ya kutisha katika nchi za eneo la Mashariki ya Kati zikiwemo Syria na Iraq. Kuendelea kwa harakati za kigaidi, kunaweza kusababisha majanga na maafa makubwa duniani. Hivi sasa jamii ya kimataifa bado haijaweza kuwa na mtazamo wa pamoja na unaokubalika kuhusiana na maan a halisi ya neno ugaidi, hivyo mabunge yanapaswa kutoa mchango wao mkubwa ili nchi zote zishirikiane katika kutokomeza ugaidi duniani. Muungano wa Mabunge Duniani ikiwa ni asasi huru, unapaswa kuhifadhi uhuru wake na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa bila ya woga.
Mojawapo ya changamoto kubwa zinazozikabili taasisi za kimataifa ni kuwa tegemezi na kukubali kuathiriwa na madola makubwa duniani. Kwa mfano taasisi kama vile Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia zimekuwa zikiathiriwa na mirengo ya kisiasa na kusababisha nguvu na ushawishi wa taasisi hizo kudhoofika. Kwa minajili hiyo tunataraji kuona Muungano wa Mabunge Duniani ukifuata nyayo za hati ya Umoja wa Mataifa katika kusaidia kutatua migogoro kiadilifu na kuchukua hatua madhubuti za kuzuia kuongezeka vitisho; suala ambalo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelipendekeza kwenye kikao cha mwaka huu mjini Geneva. Ujumbe wa Bunge la Iran umetoa pendekezo lijulikanalo; 'Jukumu la Muungano wa Mabunge Duniani ni kufungamana na hati ya Umoja wa mataifa katika kutatua migogoro kwa uadilifu na usawa na kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na ongezeko la tishio la ugaidi duniani'.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com