Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 13

Velayati: Marekani haitasimama kupambana na ugaidi

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Velayati: Marekani haitasimama kupambana na ugaidiMshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amezikosoa vikali siasa za kindumakuwili za Marekani na kubainisha kwamba, Washington haitasimama na kupambana na ugaidi. Dakta Ali Akbar Velayati amesema bayana kwamba, nchi kama Marekani ambazo zimetanguliza mbele siasa za kindumakuwili katika Mashariki ya Kati, bila shaka haziwezi kuja na kuanza kupambana na ugaidi.
Dakta Velayati ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kiisratijia ya Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo alipokutana hapa mjini Tehran na Ujumbe wa Taasisi ya Utafiti wa Kielimu kutoka Sweden na kueleza masikitiko yake kutokana na uingiliaji kati wa madola ya kigeni katika masuala ya eneo hili la Mashariki ya Kati.
Amesema, madola yanayofanya uingiliaji katika masuala ya Mashariki ya Kati yanalipeleka eneo hili upande wa kuangamia. Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba, madola kama Marekani na waitifaki wake ambao wanapigia upatu suala la kupambana na ugaidi na wakati huohuo kuendesha siasa za kindumakuwili katu hayawezi kuwa na nia ya kweli na ya dhati katika kupambana na ugaidi.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com