Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 13

Mashabane:Kadhia ya Palestina itatuliwe haraka

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Mashabane:Kadhia ya Palestina itatuliwe harakaWaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Afrika Kusini amesema kuwa, kupatiwa ufumbuzi mgogoro wa Palestina ni jukumu la kimataifa. Maite Nkoana-Mashabane amesema hayo katika hotuba yake kwenye mkutano wa kukarabati Gaza, huko Cairo Misri na kusisitiza kwamba, kumefanyika makongamano na mikutano mingi kuhusiana na kadhia ya Palestina, lakini pamoja na hayo Wapalestina wangali wanataabika na kuteseka kutokana na kuishi katika mazingira magumu mno.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Afrika Kusini amesisitiza kwamba, Wapalestina wanaitaka jamii ya kimataifa iandae mazingira ya kubo reshwa miundo mbinu. Amesema, ni makumi ya miaka sasa ambapo Wapalestina wamekuwa wakiendesha mapambano ya kukomboa ardhi zao na kuongeza kuwa, serikali ya Afrika Kusini itaendelea kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina mpaka litakapofanikiwa kufikia malengo yake. Bi Mashambane amesisitiza kuwa, serikali ya Afrika Kusini inasisitiza juu ya kusitishwa mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com