Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 13

Prof. Mazrui, msomi mashuhuri Afrika afariki dunia

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Prof. Mazrui, msomi mashuhuri Afrika afariki duniaProfesa Ali Mazrui, msomi mashuhuri wa Afrika na duniani kwa ujumla wa nchini Kenya amefariki dunia leo. Profesa Mazrui msomi mtajika, aliyekuwa na umri wa miaka 81, amefariki dunia leo Jumatatu nchini Marekani alikokuwa akiishi baada ya kuugua kwa muda wa miezi kadhaa. Khelef Khalifa Mwenyekiti wa Shirika la Kiislamu la Kutetea Haki za Binadamu nchini Kenya (MUHURI) amesema kuwa, mwili wa marehemu Profesa Ali Alamin Mazrui utasafirishwa na kupelekwa Kenya kwa ajili ya mazishi. Alamin Mazr ui ambaye ni mpwa wa mwendazake Profesa Ali Mazrui amethibitisha kwamba, marehemu alipenda azikwe nchini Kenya. Profesa Mazrui alikuwa msomi wa masuala ya kisiasa, utamaduni wa Kiafrika na masuala ya dini ya Kiislamu na alisifika sana kwa kuangazia utamaduni wa Kiafrika kwa walimwengu. Alizaliwa Februari 24 mwaka 1933 huko Mombasa, Kenya na hadi anaaga dunia alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Binghamton huko New York Marekani. Msomi huyo alikuwa pia mwandishi na ameandika vitabu visivyopungua 30. Marehemu amaecha mke na watoto sita

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com