Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 13

Rais Evo Morales achaguliwa tena kuiongoza Bolivia

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Rais Evo Morales achaguliwa tena kuiongoza BoliviaRais Evo Morales wa Bolivia amechaguliwa tena kwa mara ya tatu kuiongoza nchi hiyo ya Amerika ya Kusini baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa Rais uliofanyika jana nchini humo. Morales ambaye ni mfuasi wa siasa za mrengo wa kushoto na anayehesabiwa kuwa mpinzani mkuu wa ubeberu amejipatia ushindi wa asilimia 61 ya kura na hivyo kuibuka mshindi wa kiti cha Urais katika duru ya kwanza tu ya uchaguzi huo.

Mfanyabiashara mashuhuri nchini humo Samuel Doria Medina aliyekuwa akichuana na Evo Morales ameambulia asilimia 24 ya kura. Mbali na uchaguzi wa Rais, jana wananchi wa Bolivia waliwachagua pia wawakilishi wa Bunge na wale wa Baraza la Seneti. Matokeo ya awali yanaonesha kuwa, chama cha Morales kimefanikiwa pia kupata wingi wa viti vya Bunge na Baraza la Seneti. Akizungumza kwenye hotuba ya kuwashukuru wapiga kura, Morales alisema ushindi huo mkubwa unamaanisha imani kubwa waliyonayo Wabolivia kwa sera zake dhidi ya ubepari, ubeberu na ukoloni.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com