
Watu wasiopungua 9 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika
maandamano yaliyoshuhudiwa katika miji kadhaa nchini Uturuki. Maandamano
hayo yamefanywa na jamii ya Wakurdi kulalamikia kutochukua hatua
serikali ya Ankara kuwasaidia Wakurdi waliovamiwa na magaidi wa Daesh
katika mji wa Kubani ulioko kwenye mpaka wa nchi hiyo na Syria. Gavana
wa mji wa Istanbul amesema, miji ya Ankara na Istanbul pia ilishuhudia
maandamano na ghasia ambapo zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa wakiwemo
polisi 8. Wakati huo huo miji 6 ya mashariki mwa Uturuki imewekewa
sheria ya kutotoka nje kuhofia uwezekano wa kushambuliwa kutoka upande
wa mpaka wa Syria. Jumatatu Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu
alisema kuwa, wako tayari kufanyakila wawezalo kuhakikisha kuwa mipaka
ya nchi hiyo inalindwa dhidi ya mashambulizi ya kundi la Daesh.
0 toamaon yako: